Pages

Ads 468x60px

Wednesday, March 25, 2015

SEMA TUPONE..........................

Sema neno wandugu mwenzetu apone...

Habari rose. Natumaini uko salama na familia yako. Mimi ni mmojawapo wa watu wanaovutiwa sana na blog hii. Kwa kweli nimejifunza vingi. Naomba ikiwezekana hii comment yangu iweke kama topic kabisa ili nipate msaada. Nimekua nikiandamwa na roho ya kudharauliwa na kukataliwa kwa muda mrefu. Mwanzoni nilikua sitilii maanani lakini baadae nikaona kuna tatizo. Mimi ni mama wa watoto wawili nipo tanzania. Nilipomaliza chuo nilipata kazi nzuri kwenye kampuni moja kubwa. Toka nifike pale supervisor wangu akawa anafanya mpango nipelekwe section nyingine lakini ikawa inashindikana. Akawa ananifanya nionekane siwezi kazi, ananipangia kazi ambazo si zangu, hanielekezi kazi, kila mara ananipa kazi za kuniweka kwenye mtego. Baadae niliondoka kwenye hiyo kampuni baada ya kutokea fraud and my name came up, but I swear I didnt have anything to do with it na hiyo ilikua plan ya yule supervisor. Wakwe zangu na wifi ni mojawapo ya watu niliyowajali kipindi nina kazi lakini ni wasengenyaji sijapata kuona. Yaani nikisaidia mimi wanajua ni pesa ya ndugu yao. Nikija na plan nzuri ya biashara wanajua ni ndugu yao, yaani naumia mno. Hata nikichangia mchango wa mawazo ambao ni bora hakuna atakaeutilia maanani ni mpaka madhara yaje yatokee baadae. Yaani hata nikiongea kuchangia kitu hua naonekana kama najisaidia.wakija kwangu ni kukosoa kila kilichopo kwangu, hua siwezi kuongea chochote kwakua mimi hua ni mkimya labda na muoga. Yaani hakuna anayetaka kua karibu na mimi, najiangalia sioni labda nina tatizo, lakini hua nasalimia watu, mtu akiwa na shida nitajaribu kutatatua shida yake. Lakini kwa mara, ara ya kwanza katika maisha yangu nilishangaa inakuwaje uwe unamuwazia mtu mema alafu ghafla unakuja kujua nature yake halisi. Jamani wadau nisaidieni, maana naona kama naanza kubadilika na kua tofauti. Labda ni vile sina kazi now ila roho ya hasira na chuki naona inaninyemelea, hua saanyingine nalia sana. Nimekua na uchungu mwingi sana moyoni. Nisaidieni kwa maombi najua hapa kuna wanawake majemedari wa maombi, rose najua nawe ni muombaji niwekeni kwenye maombi, msinisahau kwenye vikundi vyenu vya maombi. I promise nitakuja kutoa ushuhuda hapa.

3 comments:

  1. Ma dear pole sanMungu wetu ni mwema naomba mungu akutie nguvu uondokane na hiyo roho ya shetani inayojaribu kukudidimiza , kuhusu kazi hapo juu naomba utafute cd ya mwakasege alifundisha mwaka huu march na maada yake ilikuwa inahusu Kiti cha enzi ni nafasi ya utawala uliyopo katika ulimwengu wa roho ambayo ina mamlaka juu ya muelekeo wa maisha yetu. ( hii itakusaidia pindi utakapoanzisha biashara yako au kupata kazi

    Mimi nilikuwa ninamambo mengi mno mno sijayamaliza lakini kadiri navyoutafuta uso wa bwana kunamabadiliko nayaona katika maisha yangu, ni hii blog ilinisaidia kuanza kujifunza upya , na rafiki yangu na mtaja kwa jina moja tu Rehema alikuwa chachu ya mimi kuliamini neno na mwalimu mwakasege ndo kamalizia kabisa kafanya niipende kusoma biblia na kuielewa maana mwanzo ilikuwa nehi naelewa viseversa.

    na pia jaribu kutafuta hiki kitabu cha battlefield of the mind ( Winning the battle in your mind cha Joyce Meyer mimi kinanisaidia kwa kweli . sorry kwa maelezo mengi i hope kunakitakachokufaa katika haya niloandika japo moja.

    tuendelee kuombeana katika jina la yesu kristu wa nazarethi naamini ipo siku utashinda vita uliyonayo . Rose salimia wanao

    ReplyDelete
  2. Dada mtoa mada i feel you!! Kama mdau hapo juu alichosema, mama shika neno!! Hilo ndo nuru na mwangaza wa njia zetu, hao ndugu, mumeo na your workmates huwezi kuwaface kimwili na kwa akili zako, pambana na hiyo vita kiroho,hakuna jipya duniani, hao wanao kukwaza wanafanya marudio fanya neno lamungu na sala kua kiongozi CHAKO!!
    @anonymous 27march 4:37am,hicho kitabu cha Joyce meyer nikipate wapi?

    ReplyDelete
  3. Mara nyingi huwa vinauzwa kwenye ile mikutano ya mwakasege mi nipo Tz, ila inawezekana kuna pahala pengine wanauza nikipata nitatoa taarifa hapa wapi ukatafute. asante na ubarikiwe

    ReplyDelete