Pages

Ads 468x60px

Tuesday, April 30, 2013

NEW LOOK

HAIR DO......... niipotezee au iendelee????
muke ya Slay
mdau nimekuelewa lkn sasa mwenzio fashion sizitanipita?????  hebu sema mwenyewe kagauni haka kalivyo katam halafu nikapotezee kisa kata mikono mmmh!!! tuvumiliani  tuuu,but thanks kwa ushauri nimeupokea kwa mikono miwili
mama wawili

Monday, April 29, 2013

MODEL OF THE DAY IS...........

MAMA WAWILI KWI! KWI!! KWI!


Ungebahatika kuniona kitaa leo huo ndo muonekano
muke ya Slay
nyie endeleeni mimi mwenzenu na mpango mwakani wakuwa AUS model kwa condition moja tuuu beach wear lazima nipewe kamtandio otherwise ntabadili uamuzi kwi! kwi! kwi! ushamba mzigo mwenzenu
mama wawili

hichi kiatu ni kipya naninakipendaje?????? msinipige madogo maana ntakivaa mpaka kiombe msamaha... kwani nini si changu bwana nirudie nisirudie .....nimekuwa nawekewa nguo kabatini za kanisani na zakushindia kuanzia namiaka 4 mpaka 7nguo bado inavaliwa nani kakwambia mtoto wa mkulima anaacha asili???????

mama BEYOU
I LOVE MYSELF

Napenda sana kucheka ukiona nimeachilia comment ambayo haibariki  ujue  nimecheka sana ukiona sijairuhusu kiukweli juwa tuu nimekudharau na hujui unachocomment so usiirudie rudie lkn km mpango wako niisome haina shida keep it wangu  mama wawili ntabaki kuwa mama wawili labda Baba wawili atake kuwa Baba watatu na Mungu wetu aruhusu hilo......

Thursday, April 25, 2013

GIRLS DAY

Girls na shughuli za hapa na pale............ tumemaliza mizunguko ya siku nikaamua kumzungusha Mama mjinitukapita eneo jipya heheheheeee mnyalu mie nikapatamanije??????? viwanja vinauzwa mijengo inashushwa watu na pesa zao bwana..... mpendwa mie nikaanza kuiona NDOTO kimoyoni nikajisemea EWE MUNGU ULIENIPA NYUMBA YA KUISHI UNAO UWEZO WAKUNIPA NYUMBA YA INVESTMENT PIA.......nikarudi kwenye gari vuta Camera yangu haya wanangu tupige picha huku kimoyoni na yangu simnajua tumeambiwa tutamke neno????? tuiandike ndoto na tuikumbushe???? kuna watu wananielewa hapa au sio??? ndoto zingine zinaanzaga hivi hivi......unaona, unatamani,unaliweka mezani lijadiliwe,mnapatana nakupigia goti ili kupata kibali then mnalifanyia kazi........hahahaa!!!! km naota vile mama wawili mimi.......EVERYTHING IS POSSIBLE WITH GOD
hapo chacha!!!
mpiga picha wetu waleo mmmh!!! vivuli vya mikono vyake navyo ametaka vitokeee hahahahaaa!!!!
girls
mapozi yetu sasa

hatujielewe Dady angekuwepo angeturudisha kwenye mstari

upendo wa Bwana watuzunguka ...........nahisi huo ndo ulikuwa wimbo hapo
kazi kweli kweli
 story nyingine hii sasa nimechekaje nilivyomwambia Bibi nikupige picha akasema  aaah! bwana ungeniambia km leo utanipiga picha nisingevaa nguo hizi sinilipigia juzi( in my mum voice tena ile yakuchekesha )hahahaaaa!!! akamalizia haya nipige kwenye gari na uhakikishe picha zangu zote umenipa nikawaonyesha Tanzania duuuuu!!! ntammiss sana my mumy aiseee tunachekajeeee???? na hivyo soon ataondoka  mmmh!!!
mama yake mama wawili Binti wa zamani
anakwambia raha ya hili gari ujae sasa we mwanangu sijui upewe nini jamani unenepe mi unaniuzi kweli kwi kwi! kwi!

hili ndo pozi lake akiwa amekuacha ucheke umalize akupe jingine feel so good nikiwa na my mumy...

Wednesday, April 24, 2013

TUZUNGUMZE


Namshangaa Mungu jinsi anavyoruhusu jambo na jinsi anavyoweza kukutoa, kama tujuavyo hakuna mteremko kama kuna mtu anaweza kunithibitishia hakuna ups and down in either way sijui huyo ni mwanadam wa aina gani............. naongea km mwanadam wa kawaida ambaye kuna wakati napita haswa mpaka nahisi hakuna mlango wa kutokea LAKINI, Mungu hajawahi kuniacha  ktk kila jambo nimemuona akiniinua nakunitetea nakunipa ushindi nisioutarajia........moja ya Mambo yaliyotokea ndani ya mwezi huu ambayo nimeona nikushirikishe mdau labda inaweza kukuinua kwa namna moja ama nyingine hasa pale unapopoteza tumaini.......

 ilikuwa ni siku ya tarehe 11/04 siku ambayo ni birthday ya mwanangu mdogo Cristabell ( 3yrs old)  na siku inayofuata 12/04 ni birthday ya mume wangu na nisiku niliyotakiwa kupanda pipa kwa ajili ya Vacation ya 5th anniversary ......  unaweza ukaelewa ni jinsi gani hiyo week ilikuwa special ndani ya familia yangu  kwi! kwi!kwi! kwi! adui (Shetani)naye hajalala bwana akuache tuu wewe ule good time kwa lipi unalomfurahisha???????
nikiwa na kawaida yakufanya kitu kwa ajiri ya hiyo vyote ( birthdays) this time niliamua iwe yakifamilia na ilikuwa ni one of the week days Baba watoto yuko mzigoni nikawaza ngoja nifanye suprise fulani kwa ajili ya  mtoto na Baba yake, wakati huo huo jana yake nilijikuta nataka kujua afya ya Mama yangu kabla sijaenda vacation  kwa hiyo nilifanya appointment na Doctor wangu ambayo nilipewa siku ya tar. 11/4.......  plan ilikuwa ni kumpeleka mama  then kuwanunulia zawadi wahusika , kumalizia mikakati ya suprise ambayo nikuwa sijui nitaiandaaje.......

Mama yangu niliambiwa anakisukari lkn hakuwahi kupimwa kuthibitisha, na alipofika kwangu alikula chochote ice cream everyday nawajukuu zake, chocolate ze coca cola,na vitu km hivyo bila tatizo lolote mpaka tukaamini ule ulikuwa uzushi japo maji alikuwa anakunywa sana nilichoamini ni kwa sababu ya joto,  kwa hiyo nilivyomuona  doctor maelezo yangu ya kwanza yalikuwa Mama yangu anakunywa sana maji na pia nataka afanyiwe general check up. Doctor alianza na kipimo cha sukari kwa nini mi sijui na wala sikumwambia km tunahisi anakisukari ile kumpima tuu Doctor anatetemeka  nakusema anatakiwa kupelekwa emergency department huku akiangaika na simu kuwapigia simu kuna mgonjwa analetwa mda huo anatakiwa kushughulikiwa mapema heeee!!! nimebaki nashangaa kumwambia mama ameshastuka lakini haelewi kulikoni ze kingeleza ze issue ha!ha!ha1haaaa!!! i love my Mumy............. mmmh! ikabidi nimwambie alichosema mi siumwi huyu doctor ana matatizo, hata km naumwa   mwambie mi nauwezo wa kusubiri mpaka nyie mrudi ndo tuje tuendelee na matibabu,  nilijikuta nacheka huyo mgonjwa na maneno yake...... Doctor aliniambia hichi kiwango sijawahi kukutana nacho( sukari ilikuwa 30) na anashangaa ni jinsi gani bado kachangamka nikamueleza Doctor idea ya Mumy aliniambia nikikuruhusu urudi ya huyu mgonjwa nyumbani mimi nafungwa hapo ndipo nilipogundua km hiyo ni serious issue 

hapa ndipo tulipoishia .....

natafakari namba za shetani???? ni kweli ameamua kuchukua furaha yangu kuwa huzuni???? ni kweli Mama yangu kipenzi  ni mgonjwa kiasi hiki na angalia hayo mamipira waliyomchomeka mmmh!!!,no birthday imegeuka kuwa huzuni, Doctor kaniambia mama atakuwa hospital for 4night kwa hiyo in any means i cant make my vacation  kwa nini Mungu uliruhusu gharama na unajua  sitaweza kurudishiwa  zaidi ya ticket ambayo ningerudishiwa asilimia fulani baada ya kutoa taarifa in 24 hrs kitu ambacho mpaka sasa hakitawezekana  hiyo walokole tuna sema chuma ulete kwi kwi kwi! ..... na hata km mama akitoka bado sidhani km ntakuwa na amani kumwacha mama nyumbani  pekee yake,.na tena nilimuuliza Mungu hata km nimekukosea hivi ndivyo ulivyoamua kuniadhibu???? ni wapi nilipokukosea ktkt hii furaha niliyokuwanayo mpaka ukaamua kubadili kuwa huzuni??? kwa kweli niliwaza duuu
 wakati huo huo sikutaka kumuonyesha mwanangu kipi kinaendelea siku yake yakuzaliwa japo alimstukia Bibi na hiyo mipira aliyoweka akawa anamuogopa halafu ni ma best hatari akiwa amekaa hapo ananikumbusha mumy is it my Birthday or Careen's birthday?????? let's go buy a present Mumy....... km Mama unanielewa ni jinsi gani utajisikia kwa mazingira hayo....... Bibi naye amekazana mpe mtoto haki yake mimi nipo kwenye uangalizi hapa mchukue mtoto mkafanye km mlivyopanga na safari usiahirishe mwambie doctor wanipe dawa za kunywa kwa kipindi hicho ambacho hampo you can imagine akili yangu ilivyokuwa na mvutano Bibi alikuwa anajitahidi asitoe ile furaha tuliyonayo HOW????? NINGEWEZAJE KUFURAHI HUKU MAMA YANGU YUPO KITANDANI MGONJWA????.na mengine meengi yaliendelea hapo LAKINI, Mungu sio kibuyu wala mwanadamu, Hawezi kukuacha ukaangamia,anauwezo wakuruhusu jaribu na mlango wakutokea lazima atakupa, kama mwanadamu utajeruhika sana lakini, huo ndio mtaji wakukuinua kiimani..........Madokta ri waliendelea na utaratibu wao wakutumika tumelala haturuhusiwi kulala ila niliruhusiwa kwa sababu yakutafsiri lugha hivyo nilibahatika kuona na kujua kila kilichoendelea.Asubuhi sasa taarifa niliyopewa wanashangaa wamefanikiwa kuishusha na kuicontrol vizuri itabidi tulale one more night kwa ajiri ya uangalizi tuu just in case....... Doctor alinipa barua yakuthibitisha kuchelewa ndege kwa sababu ya emergency na book in next two days ambayo nilikubaliwa, taratibu zote za hotelini na sehemu tulizotakiwa kutembelewa zote zilifanikiwa na wakati huo huo nilipata simu 2 weeks before kuna Dada mmoja aliniomba aje akae kwangu anatakiwa kuja chuo kumalizia unit yake hana pa kukaa huyo Dada jamani sijui kwa nini nilimruhusu simjui kihivyo, niMzimbabwe nilimjua kupitia Dada mmoja kanisani  ninachokumbuka siku ya kwanza kuonana naye aliniangalia vibaya mpaka nikajiuliza nimemfanyia nini kumbe alikuwa mjamzito, siku ananipigia simu kunieleza shida yake na ananiambia anamtoto mchanga waje ndani mwangu Bado najiuliza ilikuwaje moyo wangu haukuangalia hayo zaidi yakumkubalia, kumbuka hata habari ya Mama atakuwa anaumwa sina au kipindi hicho ntaondoka sina.........siku anayokuja yeye ndo anaingia  jamani ameishi na mama yangu na watoto vizuri sikutegemea!!!!! tumeshakuwa km ndugu anaishi mbali km 4-5hrs driving. it is amazing Mungu anavyofanya njia na mama mzimaaaa sukari imerudi normal ila tuu ameambiwa acontrol diet yake. na vacation tulienda simmejionea wenyewe shetani alivyokuwa na wivu alijua hilo bata lake kwi! kwi! kwi! na mwanangu baada ya taarifa tuliyopata ilibidi tufanye kitu humo humo Hospital ...........
my Angel

 hide n seek hiyo wanatafuta simu hiyo hata hawaioni mwee
Cristabell alifanikiwa Simu Careen alifanikiwa funguo
hapo chacha
Slay's girls
she is cute hey
poor Dady

tukajikatia keki ALL IN ALL SHETANI ALICHEMKA ALITUPOTEZEA MUDA LAKINI USHINDI TULITOKA NAO 

WATAPIGANA NA SISI LAKINI HAWATA TUSHINDA

Tuesday, April 23, 2013

LA FAMILY

NILIWAMISIJEEEE MY WAWILI......
TWENDE KILIONI BY BIBI
NIKUBOND KWA KWENDA MBELE HAKUNA KUMUONEA AIBU MPITA NJIA
HAPPY GIRLS

YES!! AM BLESSED
YOU CANT CATCH ME....... HUU MCHEZO ALITUFUNDISHA CAREEN  SIJUI ALITOA WAPI

OOYEAH!!!
BIBI BADO TUNAYE BANDUGU

SLAY'S GIRLS

BABA NA WANA
WE LOVE YOU ALL

Monday, April 22, 2013

BYE BYE BANGKOK


NTARUDI TENA HATA BILA KUKARIBISHWA

BINTI MLOKOLE LEO MTAONGEAJEEE????
AUS land knock knock....  niliacha gari yangu hapa ingekuwa bongo vioo vyote vingekuwa vimeshatolewa hahahaaaaa!!!

busy busy
i cant wait to see my wawili....