Ads 468x60px

.

Thursday, December 18, 2014

MAMA WAWILI.............

Ee bwana ule mpango wa gym duu una wenyewe aisee!!! masharti yamekuwa magumu  kwanza muda nimejikuta  busy namabox,  trainer wangu naona ameona anipotezee tuu ha!ha!ha! nasahauje sasa hizo  classes?????chezea bills za ulaya wewe???  so najiendea once a week sometimes hata week mbili just for fun, maana  yale malengo yakina minaji figure yamegonga mwamba duuu!!! hivi kumbe sio rahisi eeh????  mbaya zaidi imekula kwangu sinilifanya nao mkataba wa mwaka? so every week wao wanajichukulia hela yao vinginevyo ningetangaza ku resign.............. ujue gym wito!!!! hizo hasira sasa nikiingia gym nataka kushika kila kitu hata ambavyo nimeambiwa havinihusu  mi navuruga tuu nikimuona mtu nacheck move zake akitoka tuu navamia chombo Baba wawili ananichekaje sasa Ha!ha!ha!ha!

tuhamie kwenye magauni marefu eti eeh???

Cristabell ndo camera wetu wa leo anakwambia mumy dont tell me what to do when am taking you a photo(in her voice)


Jamani mwenzenu jirani na mti wake unanifanyiaje fujo eneo la pool yangu???  we ngoja ntaenda kumgongea (sorry ze mti is ze kudondorisharingi ze uchafu Ha! ha!ha! in my Kingas accent) maana  nina kajipool party coming soon, nahitaji kupafanyia usafi halafu hata simjui.

Nawapenda

Tuesday, December 16, 2014

PANDE NYINGINE YA MAMA WAWILI...........................Siku kama hizi unaingia zako mzigoni ukijua unaenda kupiga mdogo mdogo   baada ya weekend yenye mashughuli kibao nakujisahaulisha jumatatu itakuwaje duu!!!maana hata sikutaka kujua booking zimekaajee.........

 Duu ile kufika tuu  unaishia kutabasamu maana kulia huwezi maana ni baraka ila mwili ndo umegoma mbaya zaidi ndani ya masaa 6 wateja wanataka magari yao......... 

Duu!!! unafanyaje sasa zaidi yakuingia mzigoni ????haya ndo nikaamua nakupiga mapicha kuanza kuandaa mwili ukabiliane na yafuatayo..........


nikajikuta naimba ujue guess wimbo gani??? (Zawadi gani mimiii,Nita ,Nitamtolea Bwana Ila, Ila moyo wangu tuux2 Pokeaa,Sifa..............
Check kono hilo weweeee lazima unipende ha!ha!ha!

Monday, December 15, 2014

NANI HUYU?????????


Yupogo hajafulia jamani ha!ha!ha! 

anazidi kuwa binti wa Yesu eti eeeh??? ( nitieni moyo khaa!)
mapozi na yeye

Muke ya Slay 


mama wawili
 na Tabasamu hilo nimewaachia ha!ha!ha! Nawapenda mpaka basiiii

Monday, December 8, 2014

NAWAMISO................. Wapendwa wangu huku mafichoni hakuna jipya, Habari ya mjini ni maproject tuu Ha!ha!ha!  

 Hivi ndugu zangu hii project iliishaje?? maana naona kama hii video ilitoka kama miezi miwili mitatu iliyopita au ilirekodiwa miaka hiyo???? Imekuwaje sasa wameitoa kipindi hichi ?? mbona kama naona uhalisia na video vinanichanganya???? Au mimi ndo sielewe maproject huwa yanakaaje?? kweli ushamba mzigo yaani kama ,maproject ya pande ile ndo yamenimalisa kabisa mwenzenu khaaa!! 

Vinginevyo wimbo mzuri, umebeba ujumbe mzuri,Tatizo ile project yao sijajua ilikuwaje japo hainihusu............. mzigo unakuja pale ninapousikiliza huu wimbo mapokeo yanagoma kabisa.

Hapa ndipo unapokuwaga mtihani kwa watu fulani fulani ,kwa pande hii naweza sema Watumishi,  muimbaji, mchungaji,  ni kweli huwa kuna uvumi, au mara jingine kama wanadamu huwa tunakosea lakini huwa kuna namna fulani huwa tunatakiwa tuifanye.
Ngoja nijisemee kwa mfano Mimi sihitaji kujua ilikuwaje au imeishaje, ili niupate huu ujumbe vizuri labda ningepata suprise moja kali kwenye moja ya media kama nilivyozoea kuwaona na mabig smile yao hata kwenye video wenyewe mjionee............... then ndo ningekuja sasa kuiona hii video duu!! yaani ningemtukuza Mungu mnoo kwa ajili yao, Ningemcheka shetani mpaka angeshangaa kwa ajili yao(Angalizo,Namtukuza MUNGU na Nakumcheka shetani kila siku hapa nazungumzia kwa hili).
 Mbona hii CD kwenye gari isingetoka  ningeisikiliza mchana na jioni.....maana natembea na ushuhuda ulio hai.(After maproject)

Yaani, hili limenifanya nijiwazie mwenyewe hivi YESU alivyofufuka angeamua   aunge zake mbinguni bila kuwatokea wanafunzi wake ili kuthibitisha ufufuo wake kama neno lilivyoandikwaingekuwaje??? hivi sipangetokea kamvurugano fulani japo bado kuna wale ambao ,mpaka kesho hawakuamini kwa maana tangu kabla haijawa walishajipa majibu kuwa ni uvumi................ Nielewe niliposema hapo juu kuna namna fulani yatupasa kufanya...... kwangu mimi achana tuu na ule uthibitisho naamini wanafunzi hapa walifarijiwa, walitiwa moyo,na pia walipata nguvu zaidi yakusonga mbele .

Nimejiuliza tuu kama asingefanya vile mbona tungekuwa namaswali mengi sana hivi leo........... na pengine kuamini kwetu kungekuwa kwa mashaka,  labda ndo maana na mimi nimeshindwa kuisikiliza kwa hisia nakutaka kuelewa zaidi (Nawaza tuu wapenzi). Na vipi sasa kwa yule ambaye yupo mlangoni anataka kuingia???? Anaanzaje sasa kutuelewa????Asikwambie mtu wapendwa kuna mahusiano makubwa mnoo kati ya ujumbe na mtoa ujumbe.

 Hee nimeanza sasa.... mtajiju si mmenimiss wenyewe???? ndo nimekuja sasa ha!ha!ha!ha! haya ndo mnijibu na ahsante woooote kwa mainbox yakunikumbuka...........


Penda nyie sanaaaaa

Thursday, November 27, 2014

ENZI ZA MWALIMU VS ENZI ZA SASA..............


 Hapo chacha raha ya picha kumbukumbu badala ya kupost nimeanza kujichungulia weee nikaamua niwashirikishe........Ha!ha!ha!
 Naona hapa niliambiwa niringe mtoto wa kike
Hapa sijui ilikuwa nakimbia au ndo mapozi

hapa ilikuwa mambo ya kimiss miss ha!ha!ha!

nimeboba kihehe chezea mimi nyie....

Mdau wewe ndo umenifanya nikaitafute hii picha ndo na nyingine zooote zikafanyika post Ha!ha!ha!

 Zifuatazo ni zama za sasa

 Kabby kake Slay hako


 miondoko sasaNimemiss mnyama duu hichi kiatu ndo itakuwa habari za hivi karibuni duu nilikisahau eti......
yaani hizi ni juzi juzi tuuu

Nawapendaaaaaa

Monday, November 24, 2014

MDAU..................


 Leo nimefurahishwaje sasa na mdau wangu???? Duu!!! Mnamkumbuka yule mshindi wetu tuliamua tujichange change tupate stationary??? Nguvu haikuwa sana Shukrani  kwa wale mliojitokeza lakini baadae mambo yakawa sio nakushindwa kutimiza ahadi zenu....... Sio nyinyi tuu Hata mimi mahesabu yangu hayakupangika sana kuelekea hiyo project. lakini kikubwa wengi wetu tulionyesha nia,Ninachoweza sema ile nia ulionyesha ilitengeneza kitu katika ulimwengu wa roho. Kile kidogo nilichomtumia kwa kweli amenifanya nitoe machozi kwa jinsi alivyojiongeza kiakili  na hizo breakdown alizozifanya. Amenitia moyo mnooo!!! Ndugu zangu hatuhitaji mamilion ili tufikishe ndoto zetu  amini usiamini senti tano inaweza kuileta ndoto yako kwenye uhalisia ni vile wewe unavyoichukulia hiyo senti tano...........

Mpaka sasa anachohitaji ni kodi tuu....... Ila kanimalizaje sasa kajipanga weeeee huku akiliweka moyoni mama wawili kati ya ahadi yake alipa nusu  kwa hiyo ile nusu yake ndo italipa rent duu!!! mi sinilijua nimesha samehewa??? Ha!ha!ha!ha! Nimeanzaje sasa kujieleza??/ Ndugu yangu nivumilie kidogo hutu tumiezi tugumu mwenzio ukigeuka huku siku kuu, huku ada,huku mgonjwa ,huku.........chezea kudaiwa wewe??? 

Hii pia nikuwakumbusha na wale mlio ahidi mkasajisahaulisha kama mimi hapa leo ndio nimekumbuka heee kumbe na deni??? lakini km mambo bado hayajakaa vizuri usijari............ Mungu akakukumbuke kwa ajili ya nia uliyoweka.Ubarikiwe

 Haya mimi hapa mnionage........
Sura ya kikazi simmeona na vazi lenyewe la leo simmeliona????
Mama yao

Nawapenda......

Friday, November 21, 2014

DINNER OUT...................


The Mbeyela's & Mjema's

The Mbeyela's

The Mjema'sMuwe na weekend njema Wapenzi............

Thursday, November 20, 2014

MBAVU ZANGU.....................


Haya ambao hamjaiona hii clip..... Huyu Dada hadithi nyingine aisee!!! kipaji kipo hapo amenifurahisha alivyomwambia nyumbani kwangu ndo hupiti otherwise mawe yanakuhusu kha!!!


Wednesday, November 19, 2014

MAMA WAWILI.........Sasa hizi nywele tunafanyaje sasa khaa!!! nazipenda ila natamani new look japo ya wiki mbili tatu eti eeeh!!!! mapozi sio mengi nisije nikamwaga radhi  ha!ha!ha!

mazoezi yanaendelea mjue!!!!ila kumbe kweli yanahitaji commitment ya hatariiii.... mmmh!!! na mabox nayo balaa

Kwa heri basi.

Tuesday, November 18, 2014

THE LOOK..................

Pata muonekano wa moja wakaji outing  ya birthday girl.........        wanasema dalili moja ya ukubwa nikupenda rangi nyeupe kama kweli basi nimo  mapenzi ya white naona yamechukua nafasi kumoyo kwangu siku hizi..........
mimi hapa

Nimetoka kuangalia kansiime clip yake moja anasema yeye ana mguu haangaiki kuonyesha ila sie wenye fimbo full kutembea uchi ha!ha!ha! ntashare hiyo clip  this week....
Haya nawapenda......