Pages

Ads 468x60px

Wednesday, March 4, 2015

SEMA TUPONE.............


Haya Wadau  nimeona nianzishe hichi kipengele cha SEMA TUPONE........
  Je una kitu unatamani Dunia ijifunze, Una shuhuda ambayo huwezi kutulia kila upatapo nafasi unatamani umuaibishe Shetani?? Ulikuwa nakifungo ambacho ulivyotoka hujielewi zaidi ya kurudisha utukufu kwa Mungu kwa ajili ya neema aliyoiachilia juu ya kifungo hicho??? Kwenye ulimwengu wetu huu wa social Media labda unaona kuna udanganyifu ambao shetani anatumia kupitia ungependa kusema kitu ili yule aliyekusudiwa aupate ujumbe????

 Wakati wako  ndo huu ifanye Blog hii iwe yako kwa hilo Maana nimejikuta nimekuwa mchoyo kila siku ni juu ya mimi tuu......... Kumbe kuna wakati na mimi nahitaji kujifunza kutoka kwenu.

Naomba Shuhuda iwe ya kweli wadau, ujue hapa dizaini km Madhabahu ha!ha!ha! ningependa kuwe kuna ukweli ndani yake ili mioyo ya watu ipone. Dunia ya sasa tumezukwa namaigizo mengi hebu sisi tuwe tofauti eti eeh!!

 TUNAMSHINDA SHETANI KWA USHUHUDA...... SHUHUDA ZA KWELI UJENGA NA KUINUA....

 Ila usije ukaniambia, shuhuda yangu nilipanda dala dala konda hakuniona nikashuka nakukimbia,  we ushindwa huo wizi usinishirikishe mwenzio.......

 Ngoja niwachekeshe nilikuwa na mpendwa mmoja kiukweli alikuwa wakuonewa huruma kutokana na historia ya maisha yake sasa alivyoanza kuja kanisani watu wakawa wanamuhurumia  wanampa hifadhi hee Mpendwa asianze maombi ya mwenye nyumba asahau nyumba yake na shuhuda anatoa Mungu kampa nyumba, Mwenye nyumba baadae nahisi akahisi kitu akatafuta namna yakumtoa weee, mpendwa aligoma nakufunga juu hiyo ni nyumba yake hatoki ha!ha!ha!ha! Mwisho wa siku alitoka wee Mungu wetu sio wadhuruma, ni Mungu wa haki   hafanyagi vitu kihivyo yaani dizaini hiyo utaipata labda kwa waganga wakienyeji ha!ha!ha!

 Haya nitumie e mail slayros@yahoo.com

Angalizo: nitakapo  publish  huo ushuhuda  usitegemee sana  comments  kikubwa ujumbe umesomwa eti eeh!!
 Blog yangu inasumbua comment nimelalamikiwa sana...........Sema nini???sina hela yakutengeneza website nyingine Ha!Ha!ha! jamani joke, bado sijaona umuhimu labda huko mbeleni tutabadilisha...... tatizo nilishawaona watalaamu ili nibadilishe  waliniambia  hilo jina (BE YOU) lazima libadilike  au kuongezwa ongezwa mavitu Duu!! Mama wawili nalipendaje sasa???

Mbarikiwe

No comments:

Post a Comment