Pages

Ads 468x60px

Sunday, September 29, 2013

EVERYDAY SUPRISE! SUPRISE! SUPRISOOOO......

Anakwambia nataka nimjue HUYU MWANAUME AMBAYE UPEPO NA BAHARI VINAMTII.......MUNGU KUMBE JINA LAKO JINGINE NI REJECTED??????, ...........ADUI UNAOWAONA LEO HUTAWAONA TENA.........ALIPORUHUSU JARIBU HILO ALIJUA UNAWEZA,  ZAIDI NATAKA NIMJUE.........EVERY DAY SUPRISE,SUPRISE SUPRISOOOO......

 nisiwamalizie utamu wandugu sikilizeni.......VERY INSPIRING!!!!!!! GOD BLESS YOU CHRISTINA SHUSHO......... KEEP IT UP MY DADA.........yaani hujui tu jinsi unavyotumika kutibu roho za watu......

Kiroho safi wandugu sina nia yakuuwa soko la mziki wa mtu ila kiukweli nikipita kusikiliza hizo nyimbo zinazosifiwa mdundo huwa nauelewa kidogooo labda kwa sababu napenda midundo......... lakini ujumbe huwa sielewi kabisa hakuna jipya zaidi yanikinywa maji nakuona kwenye glass na hadithi za abunuasi na maneno yakiuchokozi chokozi ambayo yamenia kumfadhaisha mtu................... sasa sijui ndo ushamba wangu au???????kweli ushamba mzigo khaaaa!!! ila ndo nimeridhika nao aisee kama ni maombi naomba mniombee niwe hapa hapa au niingie zaidi shambani ya mujini  yamenishinda mwenzenu.................(msiende kunisemelea tuu nimetoa la moyoni mwenzenu nikilizuia litanikaba)

kama wakunielewa utanielewa tuu we sikiliza hili goma..........Dunia tulionayo wandugu tunataka kutiwa moyo,kuinuka,amani,kurekebishwa kwa nia yakusonga mbele zaidi ya yote KUMJUA HUYU ALIYEKUFANYA WEWE NA MIMI LEO TUWE.


Anajinomaje sasa na mimba yake ?? ujasiri wa kile anachoamini sasa, Mama wawili mbona burudaniiiii.......

Friday, September 27, 2013

HERI WAONGOJEAO MUDA ULIO SAHIHI.................

Swali langu lakizushi........ sasa wandugu siniliwaomba tufanye maombi ya mapatano kwa ajili ya hili????? hamjui kama maombi ya mapatano yanaweza kukausha bahari na kung'oa mlima?????imekuwaje sasa bado tuu tunasubiri???? maana kama ni nyanya zishaoza, mzigo tunao,pesa yakuwalipa watutengenezee website tunayo, nini sasa???? KIBALI......... hapa ndipo ninaposemaga goti ni kila kitu kama unaimani kama yangu ndugu yangu yote yanawezekana kwa KUOMBA ,KUSALI NAKUFUNGA.............unaweza kuwa navigezo vyoooote  bado mambo yakawa sio.......... ilibidi tuwe tunahesabu faida by now eti!!!!!!nimegundua mnanipenda mdomoni tuu utendaji ni zerooo ha!ha!ha!haa  nilidhani mtasugua goti kwa ajili yangu ili website irekebishwe faster kumbe mnanitegea eeeh!!!just a joke wandugu ahsanteni kwa maombi yenu ,ahsante kwa wote mnaonitumia ujumbe kutaka kujua kulikoni maana mmesha jianda kumpa support Mama wawili Mbarikiwe sana sana that is what we call love is blind........... mmetangaziwa tuu hata mzigo hamjui unafananaje bado wengine hamjasita kuanza kuuliza nitawatumiaje???? aiseeee!!!!!!
so far Mungu nimwema nilijua website ni kitu cha siku moja aiseee naukinga ?uhehe?ubena wangu ........mbaya zaidi nchi za watu lazima uwe kwenye foleni na utahudumiwa mpaka foleni yako ifika haijalishi we ni mgodi unaotembea au wakujiongeza kama mama wawili, haki lazima itendeke na bado huwa naamini kila kitu ni kwa muda uliosahihi otherwise huyu Mungu ninaye mwamini asingeshindwa kunipa kibali kwa maana nyingine nafasi ya upendeleo yakuhudumiwa faster faster............ we are not far away..........




check out some of  the KIDISH CLOSET will be available on day one............













Thursday, September 26, 2013

LATE POST

My Careen alivyosherekea birthday party yake darasani..............

puzzle tym
alikuwaje na sifa sasa....... kila anachojua alinionyesha
huyu ndio best yake darasani .......huyu mtoto huwa ananikumbusha enzi hizo nikiwa la kwanza nilikuwa na rafiki yangu alikuwa baunsa kinoma weee ananipa masharti yakuleta vitu shule halafu ananinyang'anya kusema nyumbani naogopa, kumwambia mwalimu nagopa atanipingua urafiki halafu nilikuwa nampenda mnooo............( Sophia  N.yako hiyo ukinisoma)
ndivyo nnavyomuona my Careen hapa haachi kumtaja best yake ukiandaa lunch box atakuuliza Mumy did you put one for ............
nimemkomesha na springles maana aliniambia ameipenda ile Keki ya kanisani kwa sababu ya springles.....
mwalimu akisafisha mikono yao ready for......
ila mwanangu angekuwa ananisikiliza kama anavyomsikiliza huyu mwalimu ningelingaje............mwalimu anamwambia kiupole nakiupendo my Careen anafanya hata akiwa nyumbani atakwambia Mama  my teacher said am not allowed to .............,  halafu wanapendana mnoo .Mama mtu sasa mpaka muda mwingine niongee kihehe au kikinga ndo anielewe hahahahaa!!! au nimwambie your teacher wont be happy if you do that mweee yale yale ntamwambia baba yako akirudi kwani wewe umeshindwa kuwajibikaaa????? hulka ya kina  Mama hiyo
oooyeah!!! she is five................nimekuza mwenzenu Ahsante Mungu

THE END

Wednesday, September 25, 2013

YALIYOENDELEA.........


MR & MRS TUNAELEKEA......
eti nashangilia...........
Mume yake.....
with friends
my girlfriend & shemeji


shughuli yoooote hiyo ilikuwa kwenda kushangaa mafarasi..........
mapozi ndani ya limo
us

dinner tym

picha ya pamoja na waliotuhudumia ndani ya limo
yaliyoendelea.....

Tuesday, September 24, 2013

PATA MUONEKANO.........

MUKE YA SLAY

MAMA WAWILI
MYSELF...

Unataka kujua huu muonekano uliendeleaje?????? stay tune......

Sunday, September 22, 2013

WEWE NI EBENEZA (EBENEZER)................



Miaka mitano iliyopita tarehe na mwezi kama wa leo  ni moja ya sababu kati ya maelfu ++++++++ ambazo moyo wangu unashindwa kutafakari ukuu na uwezo ulionao, NABUBUJIKA NA MACHOZI YA FURAHA  HUKU NIKIIMBA WIMBO WA WEWE NI EBENEZER.............. Ninachokumbuka ni alfajiri na mapema nikipewa kalamu na file  nikiambiwa Mama sign unatakiwa kupigwa nusu kaputi, nikiwa  na amani bila woga na ujasiri huku nikiwa na shauku yakuliona hili zaidi nikiruhusu mpango uliokamili kutoka kwako( wewe ni Mungu utuwaziaye yaliyo mema)  kama mwanadamu wakawaida tu naitafakari ile amani uliyoiweka ndani yangu sipati jibu???????nilichoshudia watu wanne uliowaruhusu kutumika kwa ajili ya hili wakiniongelesha huku wakifanya kazi yao, huku wakinichekesha nakunisahaulisha habari inayoendelea huku wakiwa makini na kazi yao............ ndani ya dakika chache nilisikia sauti ya mtoto ikilia huku nikipewa hongera na kuonyeshwa malaika mrembo,mwenye kilo za kutosha sijui kama ningeweza kumpush wandugu...........nywele nyingiiii, na mengineyo mengi ambayo jicho langu lilipendezwa.......... malaika huyo ambaye leo anaitwa CAREEN................................. baada ya hapo ni mengi umenitendea kwa habari ya ukuwaji wake mpaka hivi leo na mengineyo mengi ninayoyatarajia ni nachoishia kusema...... WEWE NI EBENEZER 


pengo sasa mwanangu anajitahidi kuficha haiwezekani.......
Careen & friends @ kids church

my Angel
msijali huo mdomo ni pozi zakuficha pengo
my wawili( wandugu najua ni special day kwa careen lakini nimeshindwa kujizuia wasivai sare nimeshawazoesha sasa wananipa wakati mgumu mno kutokuwavalisha wanalia kila mtu anataka avae km mwenzeka tofauti wanayoijua wao ni rangi tu....
with Dad
Baba na wanawe
Mama na mwanae........
 katika birthday zote nilizomfanyia hii mwanangu kaenjoy mnooo  ameniambia Mama that was real cool, my cake was yam and i loved the pink sprinkles i wish  i be ten years old next week........... (in careens voice) kwi! kwi! kwi! cha ajabu sijashughulika  sana this year nimepeleka cake kanisani baada ya ibada kasherekea na wenzake na kesho napeleka shule cake akale na wenzake shule.



Thursday, September 19, 2013

MAMA WAWILI

Wapendwa nipo jana, leo na kesho ...............huu ubusy kwa kweli ni dalili za muujiza wangu kha!!! yaani ni mpaka kieleweke, hakuna kukata tamaa hapa  ni mpaka nisimulie matendo makuu ya Bwana............ ombeeni na wala msichoke... ni kweli ukinicheki sura na mwili ni balaaa nimechoka mnooo .......Ahsante Mungu maana ijumaa hiyo ila kiroho hakuna kuchoka ni fire,fire,fire mpaka kilipuke...
mpaka jeans tunachomekea hkwi! kwi! kwi! hapana chezea......
Muke ya Slay




natamani kuzungumza nakosa Muda wakuandika Mungu akipenda nikiwa sawa Kesho tutazungumza............