Pages

Ads 468x60px

Monday, March 30, 2015

TUZUNGUMZE..........

Ndugu zangu, mwenzenu niliachia tuu hii  nilisoma juu juu nilijua itakutana na makamanda huku najipa muda na mimi wakuikalia........ mbarikiwe mnooo wapenzi najuvunia aisee nina  makamanda huu ndani hatariiiii!!!!pia najifunza kitu na mimi kutoka kwenu Mbarikiwe mnoooo............ Naomba na mimi niongezee kidogo mawili matatu 

nimeicopy ili kwa wale ambao hawakuisoma wajue tunazungumzia nini....

Habari rose. Natumaini uko salama na familia yako. Mimi ni mmojawapo wa watu wanaovutiwa sana na blog hii. Kwa kweli nimejifunza vingi. Naomba ikiwezekana hii comment yangu iweke kama topic kabisa ili nipate msaada. 1.Nimekua nikiandamwa na roho ya kudharauliwa na kukataliwa kwa muda mrefu. Mwanzoni nilikua sitilii maanani lakini baadae nikaona kuna tatizo. Mimi ni mama wa watoto wawili nipo tanzania. Nilipomaliza chuo nilipata kazi nzuri kwenye kampuni moja kubwa. Toka nifike pale supervisor wangu akawa anafanya mpango nipelekwe section nyingine lakini ikawa inashindikana. Akawa ananifanya nionekane siwezi kazi, ananipangia kazi ambazo si zangu, hanielekezi kazi, kila mara ananipa kazi za kuniweka kwenye mtego. Baadae niliondoka kwenye hiyo kampuni baada ya kutokea fraud and my name came up, but I swear I didnt have anything to do with it na hiyo ilikua plan ya yule supervisor. Wakwe zangu na wifi ni mojawapo ya watu niliyowajali kipindi nina kazi lakini ni wasengenyaji sijapata kuona. Yaani nikisaidia mimi wanajua ni pesa ya ndugu yao. Nikija na plan nzuri ya biashara wanajua ni ndugu yao, yaani naumia mno. Hata nikichangia mchango wa mawazo ambao ni bora hakuna atakaeutilia maanani ni mpaka madhara yaje yatokee baadae. Yaani hata nikiongea kuchangia kitu hua naonekana kama najisaidia.wakija kwangu ni kukosoa kila kilichopo kwangu, hua siwezi kuongea chochote kwakua mimi hua ni mkimya labda na muoga. Yaani hakuna anayetaka kua karibu na mimi, najiangalia sioni labda nina tatizo, lakini hua nasalimia watu, mtu akiwa na shida nitajaribu kutatatua shida yake. Lakini kwa mara, ara ya kwanza katika maisha yangu nilishangaa inakuwaje uwe unamuwazia mtu mema alafu ghafla unakuja kujua nature yake halisi. Jamani wadau nisaidieni, maana naona kama naanza kubadilika na kua tofauti. Labda ni vile sina kazi now ila roho ya hasira na chuki naona inaninyemelea, hua saanyingine nalia sana. Nimekua na uchungu mwingi sana moyoni. Nisaidieni kwa maombi najua hapa kuna wanawake majemedari wa maombi, rose najua nawe ni muombaji niwekeni kwenye maombi, msinisahau kwenye vikundi vyenu vya maombi. I promise nitakuja kutoa ushuhuda hapa.



  Wadau nafikiri wametumika sawa sawa kikubwa ni maombi hiyo ndio silaha yetu. Tukiwa kwenye maombi pia kuna vitu tunahitaji hekima kuvitambua, au kujua nafasi yako katika hilo huku likiwa ndani ya maombi.

Nimeelewa hasa kwenye mazingira ya kazi ofisini mara nyingi huwa kuna mipaka. Kuna vitu vingi huwa vinachangia kwenye mazingira ya kazi hivyo mara nyingi huwa ni hekima kuingia kiroho zaidi.........na Wakati mwingine panahitaji watu km wakina Esta na Modekae Esta 2:19-23) ili kutatua tatizo.........Vinginevyo nikukazana maombi kabla hujaingia ofisini.......... ikiwezekana muweke muhusika mbele za Mungu kabla hata hujakutana naye...(Mnajua vyenyewe tunafanyaga wapendwa wangu, ila ujue nini usilaani) 

Mtume Paulo anasema,

2wakorinto 10:2 Nawaomba nitakapokuja kwenu nisiwe na ujasiri dhidi ya watu fulani kama ninavyotazamia kwa wale wanaodhani kwamba tunaishi kwa kufuata namna ya ulimwengu huu. 3Ingawa tunaishi duniani lakini hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo. 4Silaha za vita vyetu si za mwili, Bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome. 

Sasa basi naingalia hii roho tena naona kama inanizoea sana ujue??? maana imekuja mpaka nyumbani kwangu wapenzi unavyosema nyumbani kwangu shetani anatakiwa atambue uko kwenye himaya yako yaani mi nipange kochi langu kulia for no reason we uje unipangie kushoto eti kwa sababu wewe sijui nani yake nani aiseeee!!......... kama zilivyo taratibu zakule kazini  ambazo tumeona kabisa km sio Esta na Modekae ambao ni watu  sahihi wamewekwa ili watumike,  basi ndivyo ilivyo kwenye himaya yangu.........

Hapa wapendwa wengi huwa tunachanganya na shetani anatumia sana sana sana sanaaaaaaaa............. kuna vitu vingi huwa vinazaliwa hapa aisee usipokuwa makini. Ninachosikitika pia km ndo hiyo roho imetumika kwa mda mrefu bila kukemewa huwa inaleta shida sana kuibadilisha........................Wengi wetu tunalia sana kwenye ndoa zetu na mara nyingine tunaona km Mungu hatusikii kumbe ni namna tuu ambayo unaiandaa akili yako jinsi yakukabiliana na jambo. na mara nyingine haipo hivyo unavyofikiri inakuhitaji wewe ufanye kitu.....................

 Ngoja nikupe mfano  ambao nahisi Pia nilikuwa naandaliwa kuja kuuleta hapa (labda ni mawazo yangu tuuu)

 Juzi niliota niko na Dada mmoja hivi namjua ambaye ni mjane. tulikuwa tuna have fun nakusaidia sana, sikumbuki tulisaidiana nini ila kuna kitu nilikuwanamfanyia kwa moyo wote, Sasa tukiwa tunaendelea kuna kitu alikifanya gafla ambacho mimi ndotoni nilihisi hakina upako, sikumpotezea aisee, hapo hapo nilimpa ukweli wake, kiasi kwamba ikaonekana yale yote mazuri sasa tuliyofanyiana yamekuwa zero............ kitu ambacho kikanipelekea hata mimi kuumia moyoni, nakujiuliza kwa nini ameshindwa kunielewa??? yale yote niliyomfanyia yalikuwa kwa moyo wote isipokuwa pale kwenye uovu ilinibidi niseme......... Gafla nikastua usingizini mara nyingi nikiona hivi huwa nakimbilia kwenye biblia  fasta ha!ha!ha!ha! Guess what??? nilikutana na hili neno

Warumi12: 9 Upendo lazima usiwe wa unafiki. Chukieni lililo ovu, shikamaneni na lililo jema.
Aisee nilipata nguvu hapo kwa maana nyingine nilitambua alienifanya niumie rohoni usingizini ni shetani, kutaka kunifanya nijione yote niliyoyafanya ni zero kumbe nilifanya kwa sababu ya upendo au ndivyo nilivyotakiwa kutumika  bila kucompromise.  kwa maana nyingine tusifunike ovu kwa sababu labda ni mjane, masikini, wifi ,mkwe................................ kwanza dhambi ujue???Ha!ha!ha! sikwambii ulete  timbwili humo ndani No!no!no! hiyo si hekima na wala sikwambii Mimi nafanyaje , mpendwa nyumba zinatofautiana  kikubwa ujue himaya ni yako kwa namna yoyote ile iliyo nzuri, himaya yake inatakiwa ikupe amani ili uweze kuitumikia vizuri......................... Kama wanakusengenye wakiwa huko shida ni nini eti mpendwa wangu??? Binadamu hana jema....... neno la Mungu linasema kila ufanyalo fanya kama unafanya kwa Mungu, usipoteze muda kusubiri shukrani za wanadamu japo kiukweli kuna Muda tunahitaji kutiwa moyo, lakini hilo lisitupelekee tukajikuta tunavaa mabomu ndani ya mioyo yetu kama ujisemeavyo mwenyewe hasira,chuki inakunyemelea....... Nikwambie kitu sometimes huhitaji wewe direct kutoa huo msaada km unajikuta una huo mzigo, unatamani kusaidia  mpe huyo  ambaye wanaona anafanya, sasa yeye ndio atajua anavyopeleka atawaambiaje,kikubwa  ukweli  atabaki nao yeye halafu unajua nini huyo ndo ze big boss........  na hata kesho na kesho kutwa chochote kikitokea, huhitaji kwenda mbele za Mungu kulia lia ukweli ujulikane maana Ze boss ana ukweli  badala yake unaingia mbele za Mungu kwa moyo wa shukrani jinsi anavyokutetea mbele ya watesi wako..........

Hizo Hasira ,chuki, naona shetani alikuwa anakuandaa mpenzi na anataka kukuwin ushindwe kufocus, mbaya zaidi kipindi ambacho unahitaji akili itulie ili uweze kufocus na mambo yako ya kazi ndo yamekuwa yamekutinga............. Nikwambie kitu pia acha kuhusianisha kila unachokikabili mbele yako kina uhusiano na hiyo roho yakukataliwa hizo ni mbinu za muovu.... ni dhahili anataka akuvishe hilo vazi na wewe uridhike nalo . kila ukiamka asubuhi Mwambie wewe ni mwana wa Mungu kila uwekapo nyao zako patabarikiwa, Tangaza roho ya ushindi, ni kweli patakuwa na ushindani na mvutano......... unajua nini????? mwisho wasiku We ni Mwana wa mfalme!!!!!
Malizia hiyo mistari hapo chini na Mungu akusaidie hekima jinsi yakuitumia kwenye uhalisia

Angalizo huo mstari wa 16 kumbuka alikuwa anasema na watu wajamii moja yaani wanaoongea lugha moja kwa namna nyingine anasema na wapendwa sasa tusije tukachanga ukataka kutafuta amani na pepo halafu sometimes yanakujaga na sura ya kipendwa usipokuwa kiroho imekula kwako ha!ha!ha!ha! (from experience you know)



 10Pendaneni ninyi kwa ninyi kwa upendo wa kidugu. Waheshimuni na kuwatanguliza wengine. 11Msiwe wavivu, bali mwe na bidii katika roho mkimtumikia Bwana.12Iweni na furaha katika tumaini, katika dhiki iweni na saburi, dumuni katika maombi. 13Changieni katika mahitaji ya watakatifu, wakaribisheni wageni. 14Wabarikini wale wanaowatesa, barikini wala msilaani. 15Furahini pamoja na wenye kufurahi, lieni pamoja na wale waliao. 16Kaeni kwa amani ninyi kwa ninyi. Msijivune, bali mwe tayari kushirikiana na wanyonge. Wala msiwe watu wenye kujivuna kwamba mnajua kila kitu. 17Msimlipe mtu ye yote ovu kwa ovu. Jitahidini ili mtende yaliyo mema machoni pa watu wote. 

Nawapenda


No comments:

Post a Comment