Pages

Ads 468x60px

Tuesday, March 3, 2015

MAMA WAWILI....................................

Muke ya Slay.......

 Mambo mengine majanga yaani...... hivi umewahi kutana na yule mtu ambaye stage fulani ya maisha hakupitia  anaanza kuleta fujo uzeeni??? Ahsante Yesu maana aliniacha nichafue chafue huko kwa muda wake akanitoa kabla sijamezwa kabisa mweee!!! ..............kweli ni kwa Neema!! 

Ila, kuna haka kajieneo nahisi sikuingia ndio maana nawaletea shida bloguni ha!ha!ha!  Mambo ya ulimbwende........... hivi nyie hamnistukii??? mi nishajistukia ukifika muda wa kamera....... duu!!! hayo mapozi halafu unaona yakulazimisha kabisa Ki!ki!ki!ki! we niangalie hapo juu huo mnuno na mishipa ilivyonitoka utajua tuu i wish  lakini haikuwa..........Nani alaumiwe eti???

Kwa maneno mengine nasema hivi,

Kuna haja   yakujua kwenye hii mitandao nani kapost,  kwa nini unataka uwe wewe? je kuna haja?? unahisi unachokiona na kukitamani  ndicho kilivyo kwenye uhalisia?? Je unatamani na wewe uonekane? au unataka uonekane kwasababu  ni kweli hicho kipo ndani yako(ndoto)??? 

ntakupa kajimfano 

Kabla ya kutolewa shimoni kuna kitu nilikuwa nafanya kwa sababu walionizunguka wanafanya........ Aisee kilevi mwee!!!!!!  kwanza ulikuwa ukiniuliza natumia kilevi gani?, sijui, Ila nilikuwa na hakikisha kundi ntalokutana nalo linakunywa konyagi na mimi nimo , sijui Serengeti nimo Ha!ha!ha! na mwisho wa siku lazima niwaonyeshe Mimi mlevi zaidi yao yaani... Halafu nikwambie unafikiri ule uchungu nilikuwa siusikii?? Maumivu nilikuwa nayapata pale pale, tatizo watanionaje kama mi mjanja sasa?? 

 Aisee sikumbuki kama kuna siku nilikunywa bila kutapika..... halafu nikigundua washikaji wameniona natapika, Nilikuwa nawambia ujue leo nimeanza kilaji kabla ya kula ha!ha!ha! uongo mtupuuuuu!!! chezea umaarufu wewe???

  Sometime huwa najisemea Labda roho wa Mungu alikuwa ananifanyisha vile, maana alijua sio wa pande ile........   na mara nyine najisemea labda ndo maana haikunichukua muda kuacha, maana hakukuwa na uhusiano mzuri na mwili wangu zaidi yakutaka mahusiano na wale wanaonizunguka............, Lakini pia namshukuru Mungu mnoo kuniruhusu niingie kwa muda sahihi nakunitoa kwa muda sahihi.......kunileta kwenye nafasi yakujitambua na hata leo nina nafasi yakushuhudia kwa mfano halisi................................


 Bora hapa nimelegea kidogo mwee............ ntazoea tuu we ngoja ha!ha!ha!ha!

 Nawapenda

2 comments:

  1. Aiseee kunakitu umegusia (ulevi), its like you were telling my story!!
    Wacha na Mimi ni shuhudie Wengine waokolewe.
    Am married now, ila three four years back nilikua chuo, yaani nilikua binti wa aina hiyo, kwanza nilikua napiga zile pombe kali habari ya bia nilikua naona juice tu, na nilikua natabia kila ijumaa naenda maeneo husika kupata kinywaji, aiseee nilikua mlevi hata offer ilikua ngumu kupewa maana mtu alikua anapigia hesabu ya bei ya kinywaji na kasi ya unywaji ni balaa, aiseee nilikutana na mkaka (who is my hubby now) akanitandika habari za yesu, yaani maisha yangu yalibadilika, watu walishangaa sana, darasani nikaanza kuexcel, walimu wangu hawakuamini, sifa na label mbaya zikabadilika, na mshukuru Mungu kwa kuninasua uko, yaani saivi nikisikia harufu ya pombe nakerekwa too much!! Wakati enzi hizo nilikua nawakimbiza hadi wakaka kwa ulevi!! Jamani Mungu yupo ati. Yaani sijui nisemeje i Wish ningeelezea in details mpate uhalisia. Ila namshukuru Mungu kwa kunitoa huko, and i will never go back in Jesus Name

    ReplyDelete
  2. Asante Anonymous hapo juu ni kweli tumekuwa tukifanya vitu kufuata marafiki majirani kitu ambacho sio kizuri! ni somo zuri mamy!

    Umependeza muke ya Aslay

    ReplyDelete