Pages

Ads 468x60px

Friday, June 20, 2014

TUZUNGUMZE..........


Ngoja nikwambie mpendwa wangu, Mwana wa Mungu huwa ni wakipekee, Majaribu na mafanikio yake huwa hayafikiriki kwa namna ya kikawaida, Wakati anapopitia jambo fulani kwa bahati mbaya au nzuri jamii fulani ikalipokea asilimia kubwa ya hilo jambo litapewa sura tofauti na mara nyingi hupoteza uhalisia wa jambo husika.Maumivu na misukosuko yanayoelezwa na ile jamii mara nyingi huwa ni mazito na kukatisha tamaa kuliko muhusika mwenyewe anavyolichukulia ............Na hata kama ni kweli kama wanavyodhani jamii hii huwa wamepigwa upofu wasiione ile amani na tumaini aliyokuwa nayo muhusika. Na hapa ndipo wanapotokeaga na manabii wa uongo (kwi!kwi!kwi!) maana nabii wa uongo huwa lazima awe na chakuanzia halafu yeye anamalizia,Si tulisema sisi, maskini hivi itakuwaje, sasa itabidi wafanye hivi, yaani maneno meengi yafujo fujo............  na wengi wao huwa hawasogei kwa muhusika kuupata uhalisia wa jambo. Ni heri hata yule basi, anayethubutu kusogea kwa muhusika ili apate uhalisia lakini, bado nao lazima kuwe kuna lugha moja ( Mwana wa Mungu) ambayo itafanya muelewane.  Ikiwa sio lugha moja mara nyingi huwa wanafungwa uelewa kwa namna yoyote utakayojieleza wewe wao watakuwa wamekuja na majibu na hayo ndio wanayotegemea uwambie , mara nyingi hawa watu wametengwa na kweli.  Kama hunielewi nenda kamsome Ayubu alipopitia na ashukuriwe huyu Mungu aliyemtoa mwanae wa pekee pale msalabani maana haitatokea pito kama la Ayubu. Na hii ndo tofauti iliyopo kati ya mwana wa Mungu na wa Mataifa.


 Unapokuja kwa habari ya mafanikio. Namna Mwana wa Mungu anapotoka kwenye utukufu mmoja kwenda mwingine. Mara nyingi huwa kuna vitu vinafanyika hapo katikati ambavyo jamii kubwa huwa haielewi na kama jamii imelewe basi  haiko tayari kufanya, kwa sababu labda sio chaguo la wengi anaowaona yeye ( nikimaanisha Mungu ana watu weeengi kuliko unavyodhani wewe ila unachokiona ni kile unachokiona wewe kwa maana ndio mazingira uliyojiweka na kupigwa upofu usione).Mara nyingi huwa kuna namna yakipekee, mfano, Mwana wa Mungu ataamka saa sita za usiku kuomba kwa ajili jambo fulani, Jamii isiyoelewa haitapokea kama ni kawaida, lakini ataona kawaida kwa anayekesha kwenye makumbi ya starehe kwa maana hayo ndo mazingira aliyojiweka nakuamini ndivyo inavyotakiwa iwe, Ukija makazini mara nyingi ukiona mwana wa Mungu ameketishwa na wakuu au yupo kwenye nafasi kubwa kubwa ,mara nyingi sehemu aliyotokea mpaka akafike kwenye hiyo ngazi huwa ya kipekee na hata alipofika, jamii huwa haitaki kuamini au kukubali kama huyo muhusika ndie yeye aliyekaa hapo....... kwa sababu haikufanyika kama ilivyo kawaida ya wengi mfano rushwa,kumfahamu fulani,................... Na ukija kwewnye ulimwengu wa kuwekeza, jicho unaloliona mwana wa Mungu juu ya milango iliyo mbele yako wengi wao hawalioni na kama wameiona hawako tayari kutoa kipaumbele maana hawapendi tofauti, na wengine wanataka short cut, ( Usishangae kuona sasa hivi walio wengi wanatafuta kila namna yakukutana na maboss wa sembe ili na wao wabebeshwe (wawe punda). wakati wewe mwingine unakesha ukiomba hili janga liishe, na usishangae unapokuwa kwenye hatua fulani ukapewa majina fulani fulani mfano mchawi,Sembe,......... kama kweli wewe ni mwana wa Mungu na kweli unayo wewe Hii ndio tofauti na upekee ulionao wewe ( mwana wa Mungu)............Hebu nenda kasome Daniel 1-3 ikiwezekana kasome zaidi kuna vitu vingi sana vya kujifunza kuhusiana na hii topic ya leo na labda utanielewa zaidi.


Ninachotaka kukumbusha ni hivi mpendwa, kama hivi ndivyo ilivyo kwako, UPEKEE HUO ndio unaoleta UTUKUFU KWA BWANA, ndio unakufanya upondeke  maana kila lililotendeka kwako ni NEEMA.Ukisoma Daniel utanielewa pamoja na yote aliyowezeshwa na Mungu kufanya hata siku moja hakuwahi kujinadi, alirudisha utukufu kwa Bwana hata pale mfalme alipotaka  kumkuza Daniel kama Daniel ,bado Daniel alimkumbusha mfalme kwamba, hayo yote sio yeye bali kuna mtu zaidi ya yeye.Na hata alipowekwa mahali pa juu hakulewa na ile nafasi maana aliamini yule aliyemuweka pale si mwanadam.  Hana sababu yakumnyenyekea mwanadam ambaye yeye anatumika tuu kutoa tamko la kuketi mahali pa juu lakini anayemketisha ni yule anayemtumikia................... kasome Daniel mlango wa 4 utanielewa.

UPEKEE HUU unakufanya ufanye vitu visivyoeleweka kwa wengi, nimemsoma Daniel wakati mfalme amekusudia kuwalisha vyakula vinono vya kifalme ili watoke wamenona,Daniel yeye hakuamini kwamba hicho chakula  ndicho kitakacho timiza lengo zaidi yakujitia unajisi ,yeye aliomba mtama na maji (kasome mazungumzo yake na yule mlinzi) lakini mwisho wa siku yeye na wenzake ndio waliotimiza lengo, kuliko chaguo la walio wengi.(anyway haikuwa chaguo maana ilikuwa kama kajiamri fulani lakini kulikuwa kuna hitaji upekee ili kujinasua hapo)

 Nikimsoma zaidi kuna kitu nimejifunza pia wakati Daniel na wenzie wanaomba kwa habari ya Mungu ampe ufunuo wa ndoto ili wajinasue kwenye adhabu ya kifo, CHAKUSHANGAZA!! kumbe huo ndo mlango wa kwenda kuketishwa na wakuu, utanielewa hapa niliposema hapo juu kwa jinsi Mungu anavyokuinua kutoka chini kwenda juuuuu......... kwa kweli niyakipekee na kwa namna yoyote ile utarudisha utukufu kwa Mungu.

HII YOTE NINATAKA KUKWAMBIA HIVI......

MWANA WA MUNGU NI JASIRI, ANAJUA ANACHOKIFANYA,HASHUGHULIKI NA KAWAIDA ZA WENGI,ANALO TUMAINI  NA PALE UVUMI (UONGO AU HABARI ISIYO YA UHAKIKA)  INAPOJADILIWA SANA NA WATU KUHUSU YEYE HUWA HANA MUDA WA KUJITETEA MAANA ANAAMINI HIVI NDIVYO JAMBO LINAVYOTAKIWA KUVALISHWA SURA HIYO ILI MAMBO MENGINE YAENDELEE NYUMA YA PAZIA KWA AJILI YA UTUKUFU  WA BWANA.


HIYO NDIO SIRI YA MWANA WA MUNGU HIYO.........................

Angalizo mtazamo wangu ukinisoma kwa makini nimesema walio wengi, japo kuna walio wachache(baadhi) ambao yawezekana mimi na wewe hatujui wako (tuko)wapi, ama labda ni vuguvugu, na ama labda ni vyovyote vile.... Mama wawili sijaruhusiwa kusema chochote juu ya hilo labda ipo siku nitaruhusiwa kutoa yangu au isiwepo kabisa.

NAWAPENDA

No comments:

Post a Comment