Pages

Ads 468x60px

Monday, June 9, 2014

CHANGAMSHA GENGE...............

Mwenzenu niliwaza sana nimeona nipige picha kabisaaaaaaa nije nifurahishe genge............... wenyewe msinipige mawe wandugu, si mnajua Mama wawili ushamba  mzigo????.

Ni hivi kama miezi miwili imepita nilipoteza funguo ya hii kitu na spare nayo nahisi ilipotea siku nyingi ila nilikuwa najipa moyo ipo ndani somewhere.......... so nikaamua kwenda kutengeneza nikajua itakuwa labda kadola mia hivi duuuu!!!!!! nikaanza kwenda zile za uchochoroni simnajua tena bei rahisi? kila ninakoenda wananiambia hizo funguo hatutengeneze mpaka uende  original yaani brand ya gari, mwisho wa siku Baba wawili ameenda  hiyo bajeti yake  aliyorudi nayo nilichoka!!!!.........Aisee nikamwambia Baba wawili ngoja kwanza tukaanze kutafuta tena nilipanguaje nakupangua???? hamna kitu last week imebidi tujiongeze tuu tutafanyaje sasa tubaki tumelipaki au tumalizane na hiyo gharama????

Hapo ndipo nilipoanza mawazo haya...............

 Eti hivi kwa nini huwa mnaita magari Baby??? Wandugu sijasema mnakosea ila nataka kujua na mimi yaani  akili  huwa haiclick kabisa!!! (Ushamba eti???)BABY !!!!!!yaani thamani yake inafanana ki hivyo??? kwanza kuipata  hiyo mimba ni neema, pili miezi tisa si mchezo wandugu, then malaika( Baby)   bado huo ulinzi,huduma  kwa ujumla nionavyo mimi haijafikia hata theluthi moja yakufananisha.

 Naelewa mnoo kwamba ni moja ya mbaraka(Baraka) hasa kwa kina sie yaani ni NEEMA!!!  lakini sio kwa kiwango chakunifananishia na mtoto duuu??

 Nikawaza labda sielewi maana na baadhi ya wenzangu na mie tunaendelea kucopy na kupaste??? 
 Nikikangalia hako kafunguo jamani kananitia hasira(najitahidi isiwe ya kumkosea Mungu) ILA  kunivurugia bajeti bila kupenda  ndo nini?????!!!! kinachonikera zaidi saizi nakathaminije sasa kila sa nastuka kama ninanako kwi! kwi !kwi! Na jiuliza labda hii ndo sababu mtu yalimkuta akaona alipe hilo jina??? ( Bado hujanishawishi)
 Kisema na Mama yangu alivyokuja, yaani hii gari ningekuwa  na leseni mimi ndo ningekuwa nakuendesha!!! maana wewe hapo umekaa utafikiri Mimi ndo boss wako,  Mwanangu hivi nini kinakufanya usinenepe??? wananenepa wakina............ wana............ kibaoooo (in her voice)Ha! ha! ha! nimemkumbuka mnooooo!!!!

Wawili nao walikuwa wananisumbua hizo DVD zao zilikuwa zimefungiwa humo ndani. wakiniuliza tunawambia zimefungiwa humo hayo maswali yanayofuatia sasa nyie acheni utoto raha sanaaa. Huyu mdogo siku moja aliniambia Mumy please you need to buy a new key, coz i miss my black car( in her voice) Wamegawana Yellow car ya mkubwa  na Black ya mdogo sie wengine vibaraka wao naona according to wao..........................Je bado hii ni sababu  yakunifanya niite hii kitu Baby????







Nimesema tunachangamsha genge.......... ole wenu mnipige mawe ntajirudishia mjue??? na wengine nikija huko nikakuta mmenichambua kama karanga  kwenye macomment ambayo hata topic hainihusu mnajua ntawaombea mpigwe ububu au mshindwe kuandika  kabisa hiyo comment (Chezea mlokole nyie) Ha! Ha!Ha! joke wapendwa wangu.

3 comments:

  1. Ha ha ha ha ha ha inakera haswaaa lakini utafanyaje sasa! Polee mami! This time tafuta specific place ambayo utakua unaziweka hizo funguo baada ya kulipaki la sivyo jiandae tena madollali kukutoka which i hope it wont happen again!

    ReplyDelete
  2. gari yako nzuri dear...kweli ni Baraka.

    ReplyDelete
  3. kuita baby ni kwa sababu kulipata gari ni ngumu kutokana na hali ya maisha ila haimaanishi kuita gari baby utalinganisha na thamani ya binadamu ambao tumeumbwa kwa mfano wake.kwa iyo isikutishe.

    ReplyDelete