Pages

Ads 468x60px

Friday, June 6, 2014

TUZUNGUMZE..............


 Ni hivi wadau mimi sio mzuri sana wa hii topic ninayoizungumzia hapa (wapo wenye karama zao), ila kuna kauelewa ambako ninako nimetamani kuwasilisha, Ntazungumza na wale tuu wanao amini neno la Mungu, maandiko matakatifu, Biblia. 

Unajua nini????

 Wandugu hebu tutenga muda wakusoma neno la Mungu. Kuna mtu aliwahi kuniambia waamini wengi tunatumia muda mwingi kuomba kuliko kusoma neno, Tunasahau kwamba msingi wa maombi unatoka kwenye neno. Chochote unachoomba ni lazima ujue Neno linasema nini juu ya hilo.

JIFUNZE NENO ILI LIKUWEKE HURU.

Kwa kusema hivi sijasema Mama wawili nalijua Neno kuanzia Mwanzo mpaka Ufunuo BIG NO!!! Ila huwa najitahidi nijue ninavyoomba  au nataka kujua kwa nini imekuwa hivi na vile  na maswali mengi ya utata, Napenda kuelewa Neno la Mungu linasemaje kwa Habari ya hilo.Tena siku hizi kuna google  weee imenirahisishia sana mtu kama mimi.

Ni hivi Wapendwa

Kuna vitu ambavyo vimetendeka sana  kwa habari yetu wapendwa, Ambavyo vimepelekea pande ya pili kupotea kabisa nakutumia kama silaha yakuona kila kitu ni maigizo tuuu(KWA MAANA WAMEPUNGUKIWA NA KWELI , WAMEFUNGWA,HAWAONI)

 Ukisoma kitabu cha Ezekieli 33:12 NA WEWE MWANADAM WAAMBIE WANA WA WATU WAKO,HAKI YAKE MWENYE HAKI HAITAMWOKOA KATIKA SIKU YAKUKOSA KWAKE .NA KWA HABARI YA UOVU WAKE MTU MWOVU HATAANGUKA KWA AJILI YA UOVU HUO,SIKU ILE ATAKAPOGHAIRI NA KUUACHA UOVU WAKE, WALA YEYE ALIYE MWENYE HAKI HATAWEZA KUISHI KWA HAKI YAKE, SIKU ILE ATAKAPO TENDA DHAMBI.................

Tukiwa katika ulimwengu huu ambao wote tupo, usione ajabu siku moja kumsikia Mama wawili / mtumishi/mwimbaji ametenda dhambi labda uwe hujasoma 1Yohana 1:8 au hujaelewa na kama hujaelewa  ndugu  pana shida sehemu fulani ya mwili wako........ yaani kuna kifungo umefungwa ili kweli isiwe ndani yako, adui amekukaririsha uone pande hii ni ngumu kuliko unavyodhani. Wengi wetu ikifikia hapa utasikia ( wanajifanyaga walokole wameumbuka,si tulisema sisi,wametapikwa, yaani bora awe kama sisi tuu, Sikia nikwambie niwe kama wewe unayemkana Bwana kama mwokozi wa maisha yako hadharani????? Tafadhali usinishirikishe hilo Mimi ninatambua kwamba Yesu ni Bwana,mpaka sauti yangu ya mwisho itakiri hivyo maana ndilo ninaloliamini, kama ameweka huduma ndani yangu kwa ajili ya utukufu wake sitasita kutumika. hukumu za wanadamu hazinitii hofu maana ninajua hata nikianguka adhabu itakayonikuta ni namna tuu yakunirudisha kwenye mstari (huniadhibu na kunirudia) lakini huyu ninaye muabudu hata niacha.........................labda hujasoma,Atakayenikana ......................... Mathayo 10:33.Ndugu kama upo hili eneo ambalo kila jambo linalotokea upande fulani wewe hauko positive ni vurugu vurugu tuuu  na kwenye maongezi unamalizia na bado,na bado fulani, Sikia unahitaji toba na kuitia ile nguvu iliyofungua mageti kwenye gereza alilofungwa Paulo na Sila(Matendo 16). Au yale maombi yaliyomfungua minyororo Petro (matendo ya mitume 12:5.......) Niamini hicho ni Kifungo.

otherwise ndugu zangu kila kilichoruhusiwa  kiwe ni sehemu yakujifunza na kujitathimini nafasi yako katika hilo.

Nipo tena na sisi ambao tunapolipokea hili tunataka kulificha ficha kama halipo ukiuliza utasikia tusiliaibishe jina la Bwana.Sikia ndugu yangu kwa upeo wangu huu mdogo  tunachohitaji ni hekima jinsi yakuliweka mbele za mataifa ukisema nilifiche kuna mtu amekusudiwa kupitia hilo ili ajitambue na kusimama.Hivi unafikiri Mungu hakulijua hili kwamba ni aibu mpaka akaliruhusu???? Alijua ila anataka kuangalia nafasi yangu mimi na wewe tunalitumiaje kupitia hili.Hatuwezi kuzuia Tusipolizungumzia mimi na wewe ili tujiweke sawa, ndio maana unakuta adui analizungumzia kwa namna yake kwa namna yakupotosha kabisa na sisi tumekaa kimya badala yakumpa neno,Mwambie mwenye haki akianguka atasimama tena maana analo tumaini lakini ,Ezekieli 33:12 HAKI YAKE MWENYE HAKI HAITAMWOKOA KATIKA SIKU YAKUKOSA KWAKE. Hivyo ajue hicho ni kipindi tuu lakini haijaondoa kwamba huyu  ni mwana wa Mungu.Au kile alichokuwa anahubiri au kuimba hakipo,labda ajivue mwenyewe moja kwa moja baada ya hilo au awe kweli alikuwa changanyikeni( alivaa vazi la.........kumbe ndani.........) Mungu anaweza kumtumia mtu yeyote kama daraja yakupitishia huduma yake mpendwa.................na matokeo yake ndo hayo , hakuna kitakachojificha kisifichuliwe!!!!!. 

  Mimi sio jukumu langu kujua  vazi lako ni lipi na kutoa hukumu juu ya hilo vazi. Ukweli anao mtu binafsi na Mungu ....... nafasi yangu ni kujiuliza kwa nini nimelijua/sikia/ona hili ?????na nina jifunza nini katika safari yangu ya wokovu????? ni wapi nimelala niamke na zaidi kuelewa adui yupo mawindoni haijalishi wewe ni nani...........................

HAYO NDO MAONI YANGU

MBARIKIWE

5 comments:

  1. Namshukuru MUNGU sana! Naibarikiwe siku niliyoigundua hii blogu!! Aisee napiga hatua kila siku sio kiimani tu hata kwenye maisha ya kawaida!!
    Dada rose tetemeka mbele ya Bwana maana kitu alichoweka ndani yako sio cha kawaida!

    ReplyDelete
  2. i wish ungeniona kabla sijaingia katika hii blog nilivyokuwa mnyonge , now nimepata nguvu , barikiwa Rose, Natamani hata ningeweza tu kusoma na kutafakari kama ufanyavyo hata kwa kiwango kidogo Ningefurahije

    ReplyDelete
  3. Mama wawili na wapendwa naomba niwaulize. Nina ujauzito na mwanaume kaniacha tusiwe na mahusiano tena. Nikaapa sitoitoa japo sina kazi maana inanisumbua nashindwa kufanya kazi. Roho inaniuma sana na mara nyingi huwa najikuta nalia nashika tumbo na kuongea na mwanangu kuwa nampenda sana,nitamtumza kwa shida na raha japo hatokuwa na baba. Je ni sawa ninavyofanya?

    ReplyDelete
  4. asante kwa tafakari nzuri

    ReplyDelete
  5. asantea mama asanteeeeeeeeeeeeeeeeeee.(anonymous hapo juu umeoa eee uyu dada ni wa pekee jamani acha tumpende bure tu uko kam mimi natamanije ningeweza tu kusoma na kutafakari kama yeye yaaani cjui tu furaha yangu ingekuwaje)

    ReplyDelete