Pages

Ads 468x60px

Saturday, January 11, 2014

WANADAM....



Huwa napenda sana kujitafakari hasa pale ninapopitia kitu fulani kinachohusu mimi mwenyewe na mwanadam mwingine, mara nyingi kabla yakufanya maamuzi hasa yale ambayo yananitaka nitengeneze kimwili ili kiroho niende sawa. ngoja nikupe mifano inayonihusu uelewe somo.......

Mama wawili anajulikana kwa jina la mlokole , hivyo imefikia hatua binadamu anataka kutumia hilo jina kama ni silaha yakutengenezea majungu, kutaka kubadilisha nakufanya vile aonavyo yeye. na mara nyingi watu wadizaini hii  huwa wanajua ukweli ila hawako tayari kukubali wala jirani,rafiki,au mtu mwingine atambue hilo, na zaidi yeye kazi yake kutafuta  wapi ulipoangua ili aweze kutumia ushahidi na mara nyingine yupo tayari kutumika kwa aina yoyote  isiyo haki na halali, bora mradi nia na kusudi lake litimie........ kama hunielewi nenda kasome story ya JOSEPH  NA MKEWE POTIPHAR ( MWANZO 39) 

Nilichojifunza hapa haikuwa kosa kwa Joseph kuacha nguo mikononi, kwani alijitahidi kufanya awezacho ili awe sawa lakini ilionekana kosa kwa sababu, ndio ilitumika kuwa silaha ya ushahidi juu ya yale yasemwayo na bi mkubwa...................Ngoja nikwambie ujinga wa Bi mkubwa hakujua (kwa sababu ya ujinga wake) kama hilo halitabadilisha uhalisia wa Joseph kwamba hayuko tayari kufanya hilo analomshawishi,na haibadilishiJoseph kuwa na sifa zote ambazo bidada alichanganyikiwa nazo(ule uhandsome boy,biblia yangu inaniambia alikuwa well-built and handsome), alisahau kwamba dhahabu ni dhahabu hata uipige vumbi vipi kitu kinang'ara.......................


Hawa ndo wanadamu ninaowazungumzia leo, tena ukiwakuta wamebahati na baadhi ya maneno ya biblia waliyokaririshwa kama haya....... ndugu yako akikukosea muombe msamaha, hapo ndo huwa wamekariri  mnoo na huwa humuamishi wala huwezi kuwaambia wandugu hilo neno baada ya hapo mwisho baada ya taratibu fulani kushindikana kuna kung'uta mavumbi  hawakuelewi!!!!( "basi muhesabu yeye kama ni mpagani na mtoza ushuru") ("ikiwa mkono au mguu wako utakusababishia utende dhambi............")nimenukuu, kajisomee mwenyewe MATHAYO 18, hawa watu huwa na vimaneno vyao  utasikia nyie si mnasemaga yule mlokole mbona.................. kila ufanyalo litahusianishwa na jina mlokole, tena ndo awapate ndugu wa pande yake weee watasindiliaje!!!!!  na mara nyingi  huwa hata hawajui neno la yale usiyopenda kutendewa wewe usimtendee ndugu yako hata kama wanalijua hilo litafunikwaje sasa!!!???yaani huwezi ukamwambia kama mlokole ni binadamu kama alivyomwanadamu yeyote, na zaidi hawezi kuelewa hakuna aliyemkamilifu na haya yote ni kwa neema  ya roho mtakatifu( pekee yetu hatuwezi bila roho mtakatifu)

 nimejifunza pia kwa sababu ya vazi fulani ulilovaa mfano  kiongozi  kuna jamii fulani haitakuruhusu uonyeshe uhalisia wako wanasahau kama kuna personal life pia, kwa mfano mimi ni mtunza hazina basi natakiwa niangalie hata maisha yangu yasiwe ya makuu fulani kwa sababu watu watajua naiba pesa au najikopesha pesa nilizopewa dhamana yakuzitunza. mfano mwingine labda mimi nikiongozi wa jamii fulani (which is  true kwi! kwi! kwi!)  basi kila ninachofanya lazima hiyo jamii iwe first kwa namna fulani  na kama ndo wapo watu wa namna hii kwenye hiyo jamii ndugu  itatafutwa sababu   kama hujielewi akili yako itayumbishwa mpaka uwe chizi................ ... na hili litakupelekea uwe fake ufanye kwa sababu unataka kutetea ile nafasi,  hivi ?????hujawahi kuwa na mtu lakini hauko comfy kufanya nae vitu fulani au kuwa nae kwenye tukio fulani ili kuepusha kitu fulani( asikukoseshe rejea mathayo), lakini haimaniishi kutokuwa nae comfy kwenye hilo  swala  hakuja badilisha kuwa wa jamii yako?????bila kujali yeye au mimi ni nani katika hiyo jamii???? najua  inahitaji hekima kujua hili  naamini kuna mtu ananielewa na kufunguka juu ya hili.........wandugu mi nilishakataa kuwa fake na huu ndo mpango, nimekataa kutetea jina wakati ndani ya moyo wangu nateseka yaani kama vipi nyie chukueni hayo majini ya mlokole,blogger,kiongozi na mengineyo  let me be myself................ hiyo ni mifano tuu wandugu  hamlengi mtu lengo tujifunze kitu.

 Kwa kusema haya yote natambua kabisa hayo majina niliyopewa ni dhamana hayakuja hivi hivi kuna namna fulani yakipekee ambayo ilionekana kwa wale walioandaliwa kunipa hizo nafasi, na nisinge penda kutumia tofauti na vile ilivyokusudiwa wandugu , naheshimu na kutambua kila kitu kina sababu iliyo njema mbele za Mungu. kama leo naweza kuambiwa mimi ni kioo cha jamii lazima kuna kitu ndani yake  kinachothibitisha hilo, sitaki kulewa sifa na pia sipendi kujibadilisha kwa namna ya kimwili na roho yangu ikateseka ................. niaminivyo mimi kama am  true to myself always huwa kuna namna yakupondeka ili kutengeneza jambo lakini si kwa sababu ya fulani anataka na lazima ufanye

 NO WAY!!!!!!


No comments:

Post a Comment