Pages

Ads 468x60px

Wednesday, January 15, 2014

MSHINDI..........

Jamani hapa ndo judge nilipofikia.......

 naomba lidhaa yakuwasiliana na muhusika  halafu ntakuja na kitu.
 mbarikiwe

Nimejifunza mengi sana kupitia wewe ikiwemo, uaminifu kwa Mungu, Upendo, Shukrani, Msamaha, Ibada, Mafanikio na mengine mengi.

Kwanza kabisa nimejifunza kwamba unapopanga jambo lazima umshirikishe Mungu ili akuongoze bila kufuata njia zako mwenyewe. Nimeona post kadhaa umeweka kwamba kuna wakati ulienda kinyume kufuata jinsi unavyotaka na si Mungu akikuongoza na mambo yakawa hayaendi sawa lakini ukimfuata Mungu basi mambo yalienda vizuri.

Pili nilijifunza kwamba kuwa mlokole sio kwamba wewe ni mkamilifu moja kwa moja sababu we ni binadamu tofauti na walokole wengine huku mtaani utasikia mimi nimeokoka siwezi kukosea hata kidogo na kuamini kwamba kama umeokoka basi umkamilika. Kuna post umekua ukiweka na kuomba samahani pale unapokosea kwakuwa sote ni binadamu. Kwaiyo nimejifunza kitu hapo.

Tatu Mavazi: kwakweli hili lilikua linanichanganya sana. Mavazi yako niliona kama hayako kilokole nikajifunza kwamba tusiangalie mavazi ya mtu jamani ndio tuseme ameokoka bali tuangalie na roho yako na matendo yake ni jinsi gani yanaleta ushuhuda kwa Mungu.

Kingine nimejifunza upendo kupendana sisi kwa sisi na kuombeana mema: kupitia familia yako nimejifunza mengi. Upendo na uaminifu kwa Mume kunamfanya ajisikie mwenye furaha katika ndoa bila kujali anacho au hana. Upendo kwa watoto bila kubagua utakuta kuna wazazi wengine wanabagua watoto wao ila kwako nimejifunza mengi mnooo. Kuombeana mema hapa dunia na kupendana sisi kwa sisi basi tutazidi kubarikiwa mana ukimuombea mwenzako limpate baya basi huwa lina kurudi bali ukimuombea mema nawe utafanikiwa.

CHAKUONGEZA
·      Binafsi nitapenda sana kama utakuwa unatuwekea historia ya waimbaji wa  injili walikotoka na walipo hili litazidi kuongeza ushuhuda na utukufu kwa Mungu.

·      Neno la Weekend uwe unatuachia neno kutoka kwenye biblia tuwe tunaita neno la wiki

Mwisho dada yangu Rose, Mimi ni mama wa mtoto mmoja wa kiume ambaye baba yake tuliachana mtoto akiwa na miezi sita na mpaka leo hamfahamu baba  yake na wala hatuna mawasiliano yoyote na mzazi mwenzangu. Nimelea mtoto mwenyewe katika hali ngumu mara sina kazi kwa ajili hata msichana wa kazi kupata ilikuwa ngumu, hata nikiwa na kazi mshahara mdogo sana. Kweli mpaka sasa mshahara wote ninaopokea unaishia kwenye matumizi kama unavyojua mishahara huku kwetu Tanzania hasa sisi tunaofanya kazi na wahindi ni mdogo sana.  Nimejitahidi kukusanya kidogo na nimefanikiwa japo hakitoshi kuanzisha biashara yangu mwenyewe. Hivyo kwa sababu mimi nimesomea mambo ya secretarial na ninaweza kufanya hizo kazi nimepangilia na kwa uwezo wa Mungu nianzishe stationaries & secretarial services ili niweze kujiajiri na kuachana na kazi za kuajiriwa. Kama nikibahatiaka kupata hii zawadi nitaiingiza kuongezea mtaji.

Asante sana na Mungu awabariki





1 comments:


  1. This is so touching.....kulea mtoto bila mwenza nadhani ni tabu sana na |Mungu amsaidie mdau, Ila Rose nadhani pia sasa ifikie wakati humu tuweze kuwatuna changia kidogo kutimiza ndoto za watu kama ya huyu dada sadaka si lazimam ikajenge kanisa au iende kanisani nadhani kufanya hivyo tutakuwa tumeyoa sadaka ya dhati na itamsaidia huyu dada.

    Huu ni mtizamo wangu binafsi.

    QR.

    ReplyDelete