Pages

Ads 468x60px

Friday, January 17, 2014

KUTOKA KWA MDAU.........

 HAYA WAPENDWA WE UNAONAJE, UNALICHUKULIAJE HILI?? SEMA NA SISI TUPONE MI NAOMBA NIZUNGUMZE BAADA YENU MAANA NIKIZUNGUMZA HAPA WATU TUTACHOKA KUSOMA ..... YANGU NITAIFANYA TOPIC KABISA NA JINSI NILIONAVYO NAKULICHUKULIA KAMA MTAZAMO WANGU BINAFSI.

(MSISAHAU KALE KABAJETI KETU WANDUGU)



Asante sana mama wawili'nafurahi kujibiwa ila jitahidi mpenzi hata kutupa neno tu au hata ushuhuda wako huwa unatufanya tuseme tunaweza pale tunapoona tumeshindwa na nikushuhudie tu;kupitia wewe Rose umenifanya niwe namtegemea Mungu sana yani imani yangu imepanda maradufu na namuomba sana Mungu anisaidie niwe mke mwema kama wewe ulivyo kwa mumeo;nikimaanisha nisiwe mama wa manung'uniko;Ila mama wawili naomba unieleweshe kuhuhu hili tene ikibibidi iwe topic kwenye kile kiwanja chetu.

Mimi nilikuwa ni mvaaji sana wa suruali lakini mume wangu alikuwa hapendi ila hakuwa na jinsi coz me ndo mavazi yangu;ila siku moja tukapata neema ya Mungu na kuingia kwenye wokovu nilifurahi sana;coz kuna vitu nina ushuhuda navyo'nilikuwa mnywaji pombe na sasa sinywi tena'mvaaji mavazi ya wanaume na sasa sivai tena(suruali)yani kwa kifupi naona nimebadilika hata mwenendo wangu'Sasa shuhuda yeneywe inaanzia hapa kwenye mavazi mpenzi'baada ya kuokolewa tukaanza kuhudhuria ibada kila nikienda kwenye ibada utakuta mtumishi wa Mungu anaongolea kuhusu suruali ila kwa ukaidi tu ikawa naikataa ile sauti kwamba kuvaa mavazi ya kiume sio dhambi;na huwezi amini sikuwa hata na sketi ikifika siku ya ibada ni shughuli mapenzi coz Mchungaji wetu anakataza kabisa kwa hiyo mimi nikawa na mavazi mawili nikienda kanisani sketi nikwa kwenye mambo yangu suruali ila Mr.alikuwa ananiambia sasa mama mke suruali mume suruali na watoto suruali huoni kama haipendezi kwa kweli alikuwa akinikwaza sana ila nilikuwa siachi kuvaa;sasa siku moja kanisni kulukuwa na semina kwa hiyo tulialika mtumishi wa Mungu kutoka sehemu nyingine ila nikashangaa sana ujumbe ule kama niliandaliwa mimi nao ni kuhusa mavazi;baada ya semina mume wangu akaniambia sasa unaonaje leo tukichoma zile suruali zako we nikamwambia jaribu;akaniambia au nikununulie pakti nzima ya kiberiti nilikataa kabisa japo ujumbe uliniingia mnoooooo.

Ikafika siku ya mihangaiko asubuhi nikatoa suruali yangu najiandaa sasa lakini mtumishi wa Mungu huwezi amini kila nikijaribisha roho ya Mungu inanikataza kabisa nikajikuta kwa mara ya kwanza nimeend kuhangaika nikiwa nimevaa suruali;sasa siku ya pili nikashindwa nkikavaa suruali yangu kama kawa vile nafika kituoni tu nakutana na Mchungaji kwa kweli nilifadhaika sana nikatoa kitenge changu nikajifunga lakini nafsi ikaniambia gf mana unamwogopa Mchungaji kulliko neno la Mungu lililotoka madhabahuni?nilijifariji lakini moyo ulikataa kabisa kwamba sipaswi kuvaa suruali na kwa kupitia neno hili KUMBKUMBU LA TORATI (22:5)Amini nilipona hiyo sehemu na sijisifu bali kwa neema tu.

Sasa mwaka jana mwezi kama wa nane nilikutana na Mtumishi wa Mungu akiwa na mke wake wao ni wenyeji wa THAILAND'sasayule mama na mume wake wamealikwa kutua neno j'pili moja kanisa fulani na yule mama akaniuliza naweza kwenda madhabahuni nikwa nimevaa hivi?nikimaanisha alikuwa amevaa suruali we acha niongee hapana mama ukipanda pale watu hawatakuelewakabisa nafikiri mama wawili nikisema hivyo unanielewa'nikamwambia kwanza ni dhambi nikampa na ufunuo kabisa;Basi yule baba akamchukua mewe ikabidi akamnunulie nguo amabazo sio suruali alivaa kiafrika kwa kweli alipendeza sana tofauti na alivyokuwa amevaa suruali'lakini nikashangaa yule baba walivyorudi kwenye ibada siku nyingine akaniita akaniambia wapi imeandikwa mwanamke asivae suruali? we nikamfunilia fasta coz huwa natembea na bible'akaniambia imeandikwa asifae mavazi ya kiume hayakutajwa ni mavazi gani kwa hiyo kuvaa suruali sio kosa nilibisha sana na kumbuka nilikuwa naongea na mtu mkubwa mnoo coz amesoma sana elimu ya dunia na mbinguni.

Nikamwambia hebu nitasfirie hili nene linamaanisha nini?mwisho akaniambia unajua kule kwetu kuna baridi sana na upepo kwa hiyo ukivaa sketi upepo ukija inapanda juu ndio mana watu kule wanavaa suruali na pia kuna baridi sana kwa hiyo ukivaa sketi unaweza ukaganda;hapo nikamwelewa mno kwamba wanavaa hivyo kutokana na mazingira waliyopo.Lakini akaniambia pia mtu anaweza asivae suruali lakini akawa na matendo ya ajabu na mwingine akavaa suruali lakini akawa na hofu na Mungu hapo napo nikamwelewa mnoooooooooo
ila nafsi yangu inakataa kabisa kuhusu hili vazi'na mume wangu sasa anafurahi kuniona niko tofauti si mvaaji tena wa hilo vazi na kuna mtu mmoja nilimshuhudia na yeye ametoka huko nilikokuwa mimi;back to you mama mawili amini ukikutana na neno zaidi ya mara tano linaongelea tu kitu kimoja Mungu anakuwa na mpango na wewe na anakubadilisha kabisa hata wewe ipo siku utakuja kusema mdau kweli ulisema yani inatikea tu kila ukitaka kuvaa roho wa Mungu anakushuhudia au nafsi inakataa kabisa tena unajiona ukivaa suruali hupendezi yan hata sijui nieleze vp.

Swali kwako mpendwa mwenzangu'wewe unavaa hilo vazi kutokana na mazingira uliyopo au  ndio kama kina sie tunaosema Mungu haangalii mavazi bali anaangalia moyo wa mtu?naomba ujibu kwenye blog ili tulio wengi tufunguliwe;au mimi ndo natumia biblia vibaya hasa kwa ufunuo kama huu Kumbkumb (22:5)Barikwa mama na zaidi ya yote kasome  Zaburi (35).nakupenda.

2 comments:

  1. Mada kali kweli lakini labda kwa uelewa wangu tu ni kwamba suruali sio vazi baya isipokua kwa mazingira. kama huku kwetu kwa mwanamke huwezi enda kanisani na jeans sababu wataona huna adabu lakini hiyo ni kutokana na mazingira tu. ulaya wanavaa vimini jeans. Watu wengi wameacha kuuhubiri ufalme wa Mungu wamekazania mavazi kitu ambacho sio sahihi kabisa kikubwa tuangalie kwamba matendo yetu yanamtukuza Mungu mana sidhani kama Mungu ataangalia mavazi yako.

    ReplyDelete
  2. Wakati inaandikwa biblia wanaume walikua wanavaa kanzu( magauni) suruali ni ubunifu wa baadae wa mwanadamu.

    ReplyDelete