Pages

Ads 468x60px

Thursday, January 30, 2014

TUZUNGUMZE

Haya ndugu zangu leo nilitaka tuzungumzie habari ya maombi ya kufunga kama mdau alivyotaka tulizungumzie, tupeane mawili matata juu ya maombi haya kwa jinsi Mungu atakavyotuongoza. lakini nimepokea e mail tena kwa mdau mwingine anaomba tuzungumzie ni namna gani tunaweza kuachilia hasa tunapokuwa tumebeba mizigo ya makwazo na kujeruhiliwa ndani ya mioyo yetu.................Nimeona bora tuanze na hili la kuachilia maana maombi ya mfungo bila kuachilia bado ni kazi bure, tukijua jinsi ya kuachilia inatupa wepesi tunavyoingia kwenye mafungo yetu.......


 Kwa uelewa wangu huu mdogo wandugu kwangu kuachilia ilikuwa ngumu mno kama nisingezingatia haya  machache nitakayosema hapa chini, na zaidi ya yote  kuomba neema  ya ujasiri  kwa namna yoyote itakayonifanya nikabiliane na hilo suala baada ya kuachilia, nilikuja kugundua kusema nimesamehe ilikuwa nirahisi kwangu lakini nilitaka lile jambo lisijirudie, na kwa sabubu shetani hajalala kila siku alitaka kunikwaza na kunikosesha raha hivyo nikajikuta lile kwazo linakuja mara kwa mara  na sa nyingine kwa namna tofauti  nilijikuta naishia kusema   ( "JAMANI NILIMSAMEHE LILE NA LILE NA HILI TENA??") ilinibidi nitulie nakutafuta njia mbadala yakutokumpa shetani nafasi ( narudia tena NEEMA ya Mungu yakukuwezesha inahitajika sana baada ya kuamua hili) niliamua kujifunza KUSAHAU ,Aisee hii kitu imenisaidia sana yaani ukiona nimelikumbuka nimeligeuza kama utani fulani mfano niliwahi kuandikiwa ujumbe fulani mwishoni uliomaliziwa na ("CHAT YOU LATER NILIKUWA NAKUPA HI TU..") kwa akili ya kibinadam ukiniuliza ntakwambia  ule ujumbe ulijaa makwazo na majeraha ambayo siyakumbuki vizuri ila haka kaneno naweza nikawa na Mume wangu tukaongea utani fulani nikamalizia na hako ka msemo.Hii aimaanishi nimebeba machungu ya ujumbe ila ninamna yakujisahaulisha nakugeza kuwa kama joke fulani na kukusaidia kupotezea. nilizidi kujigundua hili pia mara Mama yangu alipokuja huku kuna mtu nilitakiwa kufanya kitu  sasa nimekaa na Mama tunapanga mikakati nilifanyaje  nasikia ( hivi huyu mtu anakumbuka alivyokufanyia hivi na hivi,anakumbuka....... anakumbuka ......) kila anakumbuka ilikuwa ni machungu na mizigo ambayo kibinadam haibebeki all you can think ni jinsi gani yakumlipa kwa mabaya kama alivyokufanyia, kilichoshangaza siku ile nilianza kumuuliza hivi nakumbuka kama hilo neno lilitokea lakini sikumbuki ilikuwaje???? alianzaje sasa kunitafuta kunirudisha nikumbuke????mpaka alikasirika nakuniambia unajifanya hukumbuki unanienjoy eeeeh!!! ( in my mumy's voice)ha! ha! ha!  i love my Mumy aisee nimeongea mpaka nimemmiss gafla....... anyway tuliishia kubadilisha topic  maana hakukua na maelewano yeye kanibebea mizigo ambayo mimi hata siikumbuki. Nina mifano mingi mnoo kupitia hili lakini nafikiri mpaka hapo tumepata kamuelekeo kidogo.

Namna nyingine niliojifunza jinsi ya kuachilia ni kujipa muda juu ya jaribu lolote  linalonipata  hili ni muhimu mno....... rejea kwenye mfano wangu mimi mwenyewe.......  kama msomaji utanielewa kwazo lilipo nipata sikujipa hata sekunde  ubinadamu ulichukua nafasi kubwa, nilijikuta nimechoka, sikutaka kuruhusu hekima ya kiMungu  Dont you worry hizo zote ni mbinu za shetani aisee baada ya nusu saa ndo akili ya Mama wawili  inakaa sawa nakujiona mkosefu, nimekuwa mjinga nakumpa shetani nafasi . mbaya zaidi  nimepublish kitu ambacho impact yake inaweza kuwa sio nzuri kwa jamii fulani  na nakuwadissapoint. na usione ajabu kwani kupitia ule ujinga  na japokuwa nimeshaachilia na kutubu  bado  zile dakika thelathini zinaweza kuwa kwazo mbeleni kama tuu sitazingatia  hiyo nafasi ya kwanza( kutafuta namna yakujisahaulisha)

kupitia hili pia  hapo mwanzo nilishindwa kuelewa Neno liliponambia  OMBEA ADUI YAKO........  Nilijiuliza nitawezaje kumsamehe nakupiga goti kumuombea tena???? iliniumiza kichwa mpaka hapo nilipopata amani ya jibu hili......... unapopata kwazo jaribu kumuanagalia aliyekukwaza na namna alivyokukwaza, utakachokiona ni majuto,majeraha,kushindwa,wivu,kutokutumia vizuri nafasi aliyopewa,  kutokujitambua na pengine hata kutokujithamini na mwisho anakosa hekima ya namna yakusawazisha hayo anageuka kuwa kwazo kwa kila kitu  na pengine hata kwangu ambako kunanipelekea tuwe maadui. hili limenisaidia sana maana baada yakumwangalia yeye mwisho wake utajikuta kwanza unamuhurumia na kumuhurumia kutakufanya umsamehe  na kumsamehe utajikuta unamaliza na kumuombea tuu bila kutaja lile kwanzo. ambayo moja kwa moja itakuleta kwenye kuachilia.nafikiri mnanielewa vizuri hapa.

Bila kuendelea kuwachosha labda nimalizie na hili  nilijifunza kutokukaa ndani ya tatizo,makwazo kwa namna ambayo haitavuruga mahusiano ikitokea imevuruga basi hivyo ndivyo ilivyotakiwa kuwa........  nikimaanisha  hivi kama kila ninapokutana na wewe lazima tukwazane kwa namna moja ama nyingine ambayo inatutengenezea uadui nitajitahidi kwa namna yoyote yale makutano yasiyo ya lazima yasiwepo 
haimaanishi nakuchukia au nina jambo na wewe NO!  bado nakuthamini, nakupenda  nakukuombea kama unavyofanya wewe ( niaminivyo mimi) yawezekana sisi tunajitahidi kuondoa tofauti zetu lakini shetani yuko kazini kututumia pasipo wenyewe kujielewa  kwa hiyo tunapopeana nafasi inaleta uthamani fulani kati yangu na muhusika kama sisi sote tuko kwenye same page. ukiona hii mbinu haijafanikiwa zaidi yakuletea makwazo tena ujue huo uhusiano haukua wa muhimu kwako na sina haja yakujaza huo mzigo ndani yangu zaidi ya kuachilia kusamehe na kusonga mbele bila makunyanzi........


angalizo

nimeongea kwa namna nionavyo mimi inaweza ikakusaidia au isikusaidia kikubwa upate NEEMA YA KWELI NA IKAKUONGOZE. Na pia hili nimelizungumza kwa mtu yeyote yule iwe ndugu,rafiki,au jamii yoyote ambayo wewe kwako imekupa kwazo linalokufanya ushindwe kuachilia.

TAFADHALI USITUMIE HIZI MBINU KWA MUME AU MKE NO! NO! NO!
 ninamtazamo tofauti juu ya hawa watu wawili.

6 comments:

  1. Namuomba mwenyezi Mungu anisaidie maana makwazo niliyonayo bac tu . inakuwa ngumu kusamehe na kusahau mara nasamehe ila kila nikikumbuka naumia kwaiyo bado naendelea kuomba ili nipate neema yake ili niweze kuwa huru

    ReplyDelete
  2. amini inawezekana anza kuchukua hatua...... utakuja kutushuhudia humu ndani

    ReplyDelete
  3. Dada Rose hili ni somo tosha. Nliwai kufundishwa jinsi gani ya kuachilia uchungu katika maisha yaangu yaani kwa kuelezea ni rahisi sana lakini kutenda ni ngumu sana lakini ukiweza ndio mwanzo wa baraka zako. Nakumbuka nlikua na uchungu sana na nilikuwa mwombaji mzuri na nlikuwa naomba sana kupata kazi lakini nilikuwa sipati kutokana na uchungu ulio kwenye moyo wangu na maisha pia kwa hiyo Mungu alikuwa ananizuia baraka. Lakini tangu nilivyofanya maomb hayo ya kuachilia kwa kweli Mungu amefanya maajabu na baada ya miezi mitatu nimeweza kununua kiwanja na mambo mengine mengi na nimemshuhudia sana Mungu na bado ninamshuudia mambo makubwa zaidi ya hayo.
    Rose Ubarikiwe sana yaani umenikumbusha wema wa Mungu mpaka machozi yamenitoka yaani hakuna jambo zuri kama kukaa katika hema la Bwana.

    ReplyDelete
  4. Amina sana kwa kutupa somo.Ubarikiwe sana.Usisahau kuongelea swala la kufunga na maombi ya kuambatanisha plus mistari ya kusimamia eg unaombae kazi,kupata mwenza kutoka kwa Mungu ,Mume,biashara ,Kazi,Familia,upenyo nk manake siku za kufunga zinakaribia kwa sisi wakristo mimi ni mkatoliki.Na huwa nafungaga ile kavu ya masaa kumi na mbili .Mambo ya ohhh nafunga kunywa chai tu au nafunga kula ugali tu mie hiyo kitu siamini kabisa imeandikwa wapi?kwenye biblia tunaona watu walikuwa wanafunga siku 3 kavu .ss hayo mafundisho ya kufunga kunywa bia sijui aliyaleta nani jamani.

    ReplyDelete
  5. Rose kusamehe si jambo rahis hasa kama ishu ni ya kusingiziwa trust me inauma mno!!!!
    Nways God is Good.
    Nilikuwa mgumu mno lazima nilipize kwanza ila nilikaa siku moja nkawaza hiivi Mungu siku akaamua kunilipizia nitabaki kweli?
    Basi these dayz yani napuuza na nasahau!

    ReplyDelete
  6. Mhhh..umenena yoote.MUNGU azidi kukufunulia.

    ReplyDelete