Pages

Ads 468x60px

Monday, January 13, 2014

VIGEZO VYA MSHINDI


 Haya wandugu ahsanteni sana kwa inbox zenu kwa kweli  sijui ni nini Kusudi la Mungu kupitia hii Blog ...........mmenifanya nilie,nicheke, nimechukua dakika kadhaa kuwaza mnoo na pia kuomba....... kila niliposoma inbox ya mtu nilijifunza kitu, na kuzidi kujitambua,  wakati Mwingine huwa na blog kwa kujifurahisha lakini wadau mmenifanya kuona kwamba humu ndani kuna huduma ambayo  Mungu amekusudia kupitia hii Blog. MBARIKIWE MNOOO

Kama nilivyosema this time tufanye kitu cha tofauti ambacho nilikuwa sijui nini,ila nilitegemea kitatokana na inbox zenu, ni kweli, nimejifunza na kugundua hili.....


Mshindi wetu wa mwaka jana tulimpa zawadi yake  nilitegemea atakuja kutupa ushuhuda juu ya kale kambegu lakini haikuwa hivyo kwa sababu ambazo mimi nimezielewa kwa namna hii

1. yawezekana kabisa kile kiwango hakikuwa sahihi kwake labda hitaji lake lilikuwa kubwa sana zaidi ya lile na nimejaribu kukitathimini kile kiwango tulichompa nilazima awe muhitaji wa hali ya chini kabisa  ndo kingemfaa. kwa muhitaji wa kati na wa juu ile ilikuwa ya shopping au  ya kubadilishia mboga kwa siku.

2. nimegundua hata kama alikuwa ni muhitaji wa hali ya chini kabisa basi alikuwa hana plan kama ikitokea gafla amepata  kiwango kile angefanyia nini... hivyo alijikuta anayo mkononi plan nyingi na majukumu yanayomzunguka kwa muda ule ni mengi hivyo kabla hajaamua afanyie nini majukumu yalikuwa yameshamaliza.......... hii inatutokea sana hata mimi inanitokeaga sana tuu.

 3. sikutaka kufatilia sana nani awe mshindi ila nilitoa inbox zote wadau mzipigie kula wenyewe na katika zile kula nilishindwa kujua na nini kapiga mara ngapi na nani hajapiga na  nikisema watu wa email tutakuwa hatujatenda haki maana kuna watu wangependa wapige kula ila  e mail zao ni privacy hivyo wataona heri wapotezee.

 kwa kusema hivyo naomba ruksa yenu nimchague mshindi.................... bila kuwakwaza wote mliotuma na amini nitatoka na kitu hata nyinyi mkisoma mtatoa baraka zenu. ( SISI SOTE NI WAMOJA)

Nitatoa post ya huyo mshindi  zaidi wote mliotuma hamjatofautiana sana  huyu. tofauti itakuwa kajipengele kidogo sana ambako ndo kamemfanya awe mshindi.

MBARIKIWE NAKARIBISHA NA MAONI JUU YA HILI KABLA YAKUMTOA MSHINDI.... MSISAHAU NA KUNIOMBEA JUU YA HILI MAANA DUU!!!!

No comments:

Post a Comment