Pages

Ads 468x60px

Thursday, January 30, 2014

UTOTO RAHA NYIE ..............

Basi tuu, kuna mda huwa nikikaa na wanangu kuna vitu fulani huwa vinafanyika mpaka huwa najiuliza hivi na mimi nilikuwa hivi..... yaani hawa wenzetu ni malaika aiseee, huhitaji nguvu  kuwapa furaha.... kama Mama unanielewa we chukua kaji mda kaa na mwanao  kuna vitu vya kipekee vipo ndani yao hasa mnavyofanya mazungumzo, wakitaka kujua kitu wanavyokuuliza hicho kiswali, wakiwa wanataka kitu halafu wewe mzazi hutaki kwa kumaanisha labda hakiwafai kwa muda huo na vitu kama hivi.............

 Leo nimewawaza sana wanangu, kama kawaida mishe mishe za shopping kujiandaa na shule week ijayo, wote tukoje na furahaje sasa....... my Christabell anaanza Kindy na Careen Pre primary duu!!!! kama sio kweli vile Jana tuu vilikuwa vinanyonya mweeee.....(AHSANTE BWANA YESU)
 basi katika hizo shopping Muda wakununua Viatu vya shule umefika mtu kagoma (MUMY I DONT WANT NEW SHOES CAUSE I WANNA WEAR MY PINK SLIPPERS AT SCHOOL in Careen's Voice)  Nikakumbuka juzi naye Christabell alipokuwa analala alisisitiza mtu asitoe slippers zake alipoziweka ile asubuhi  naingia chumbani kwake kumuangalia mtoto kastuka MUMY WHERE ARE MY SLIPPERS??? in Christabell's voice) yaani inanichukua muda sana kuelewa mpango mzima wa hizo slippers  umekaaje, cha ajabu nilishawahi kuwanunulia huko nyuma hakuna aliyezipenda mpaka sasa hazikuvaliwa sana na haziwatoshi tena..... juzi kati baba yao aliwanunulia tu ili aone km this time watazielewa.... mbona zimekuwa gumzo ndani mwetu kila anapoenda huwezi ukawapa story nyingine zaidi ya malapa................ ni hayo tuu yaliyonifanya nitafaaaakaaaariiii   na kujiuliza kulikoni na kujikuta natamani na mimi nirudi utotoni.............

 KITAA NA DAD YAO about to go..........

wandugu hizo nywele za kisharo  kwa Christabell msinipige mawe  anayetoka  nao ndo kataka.

nawapenda mnooo hawa watu mwenzenu mwee
wanavyoondokaga utafikiri, hawa watu kuwaona mpaka jua lizame kwi! kwi! kWi!  kiboko yao niwe nao Mama Shughuli ntawatembezaje kitaa sasa.

 wamerudi nakutafuta vishughuli
The end

7 comments:

  1. If I could turn back the hands of time but RK. Hiyo ndiyo walimu wanaita childhood Psychology.

    ReplyDelete
  2. Baada ya kupiga mkono kutwa nzima unajipumzisha na kujifurahisha na familia. I like it. Happy family is everything to me no matter what.

    ReplyDelete
  3. beautful family myrose'e(in frech accent)
    Mungu awabariki..
    Mmeo gudlooking shosti...Mungu akulindie agaist Pakashume aaaaaaammmeeen

    ReplyDelete
  4. barikiwa sana shosti wee,nice family

    aza

    ReplyDelete
  5. MUNGU Aendelee kuyagusa maisha yako dada yangu atuguse na sisi pia na wengine

    ReplyDelete
  6. Habari dada Rose mie mdau wako wa muda mrefu sana zamani nlikuwa nkicomment as anomnymous baadae nikaja kuwa nacoment as husna lakini sikuhizi kila nkicoment na kuweka jina langu ina kataa kuwa publishd naomba unielekeze labda kuna kiyu nakosea nataka kujiregister in order to be mwanachama wa kudum

    ReplyDelete