Pages

Ads 468x60px

Friday, January 3, 2014

JE WAJUA????


Maisha yako ya  nyuma yanaweza kuwa adui wa maisha yako yajayo??? na  kuanguka sio mwisho wa safari ni namna tu yakukufanya uwe makini  na safari yako............................

Tumekuwa ni watu wakuangalia historia  na kusahau kuwa siku ya leo ni  mpya........ ngoja nikupe mfano: wengi wetu tumekuwa hivi,kama jana tulifanikiwa Mungu alitusaidia kuwa na Nyumba,Gari,au biashara fulani au jambo lolote linalofanana nalo  mara nyingi watu tunalewa  akili zetu zinaangalia kile kilichopatikana na kutengeneza mazingira fulani yakupunguza kiwango cha uwajibikaji na mara nyingine hizo mali zinageuka kuwa anasa na  kuwa tujimiungu fulani  na hapa ndipo ninaposema  maisha yako ya nyuma yanaweza kuwa adui wa maisha yako yajayo.............. zile juhudi tulizozifanya kutufikisha hapo tulipo huwa zimepungua kwa kiasi kikubwa   na zaidi hofu  na unyenyekevu huwa imekwisha , kiburi na kujiinua mwenyewe kunaingilia kati. neno  linasema  NITAKUINUA KUTOKA KIWANGO KIMOJA KWENDA KINGINE  nenda kakazie (Isaya 54:2-3) huu ndo mpango wa Mungu . ukiona akili yako imelewa na hapo ulipo  mmmmh!!!!

 N a pia nimeona tumekuwa ni watu wakuugulia sana maumivu lile jaribu lililotupata mwaka jana bado tunabeba  kwenye maisha yetu ya leo, ni kweli jeraha huwa linabaki lakini huwa alibaki na maumivu ukiona bado unamaumivu  hapo ndipo ninaposema maisha yako ya nyuma yamekuwa adui  wa leo/kesho unashindwa kuachilia ili usonge mbele, tunakumbatia maumivu  nakuyafanya yawe muongozo wetu,na wakati mwingine tunajiuliza uliza sana kwa nini ilitokea  na kulaumu zaidi. nenda kasome  (Yakobo1:2-3)  utaelewa jaribu ni kawaida ya mwanadam wapendwa ila mungu hawezi kukuacha kama utajitambua na sio kunung'unika kiasi kwamba unazuia Mungu kukamilisha kile alichokusudia katika maisha yako..................

Kwa kusema hivyo basi, hayo yote silaha yake kubwa ni kuamini na kushukuru. unapobarikiwa amini Mungu amekupa na ule muda ndo uliofaa kupata kile unachokiona  mshukuru Mungu na kuomba hekima ya namna na jinsi yakukitumia ili ukaongezeke zaidi hapo. Niaminivyo mimi kama ni mtu wakujitathimini  na umekaa sawa sawa lazima utajiona kuna nafasi ya kuongezeka katika maisha yako  kwa namna yoyote ile  utaona jinsi Mungu alivyokuvusha kutoka pahala fulani kwenda kwingine na  HUO NDO MPANGO WA MUNGU............ ukiona kabisa huna hata nafasi yakumshukuru Mungu kwa ajili ya jambo Fulani ndani ya maisha yako MPENDWA KWA NAMNA FULANI mmmmhh!!! HUO SIO MPANGO WA MUNGU KABISA!!!!!!

Na kwa sababu Mungu huruhusu jaribu fulani lipite  kwenye maisha yako kwa ajili ya kazi fulani  ambayo mimi na wewe ni mashahidi ( hujawahi kupita pahala na usiuone mkono wa Mungu ) basi hatuna sababu yakubeba maumivu ambayo tunauhakika  TUNAYE SIMBA WA YUDA ASIYELALA WA KUSINZIA KWA AJILI YETU.

HIVYO BASI KATIKA KILA JAMBO KUWE KUNA NAFASI YA KUJIFUNZA ILI UJUE KESHO YAKO INAANZAJE  KWA MAANA IMEFANYIKA SIKU MPYA YAKUANZA BILA MAKUNYANZI WALA MAJIVUNO NDANI YAKE

Kutambua hili bado ni neema hivyo tuombeane sote tuliokusudiwa kulifahamu hili ili hii neema itufikie 

2014 NI WETU MAANA BWANA AMETUPA, UKAWE NI MWAKA WA USHINDI NA MAONGEZEKO WANDUGU....

1 comments:

  1. rose nakushukuru sana kwa hili uliloliandika hapa yani limenigusa mnoo na ashukuliwe Mungu wetu mwenye nguvu maana alinipa ufaham nikagundua kwamba shetani hapa ndipo aliponikamatia nikakaa kwa miaka miwili bila furaha kwa kumuwazia mtu aliyenikosea na kunitukana sana mpaka nikawa namuuliza Mungu km hapa aliponiweka ni pangu kwl. Lakini kumbe palikua ni pangu na shetani alikua anataka kunipotosha tu ili nione km sio pangu na alinipatia akayakamata mawazo na akili zangu akanipa kutokujiamini namshukuru Mungu alie nitoa huko akanileta hapa. nashukuru rose maana blog yako imekua ni faraja kubwa sana kwangu hujui tu lkn huwa unaupa moyo wangu ujasiri sana ubarikiwe mpendwa na tuombeane

    ReplyDelete