Pages

Ads 468x60px

Thursday, May 29, 2014

FLASH BACK..............................

Wiki mbili zilizopita mwenzenu nilipata ugeni,  ulioletwa na Christabell wangu (4yrs). Ana mwalimu wake wa daycare ambaye amekuwa akienda kwa miaka miwili sasa. Mwaka  jana alikuwa full time  ila mwaka huu anaenda once a week, kwa sababu sikunyingine anaenda shule........... sasa huyu mwalimu jamani alikuwa gumzo ndani ya nyumba aisee, mtoto ananiuliza maswali  meeengi. Mumy when are you inviting ...........???? ukiwa unamnunulia kitu akimkumbuka tuu, utasikia Mumy can we buy one for ..........., Mumy when she is coming for a sleep over???? hapo mezani tukikaa sometimes utasikia when ........ comes, she will sit here. Jamani kwa mda wa almost miaka miwili!!!! 

Ni kawaida yake aisee huyu mtoto akitaka kitu halafu usimpe majibu yakutosha  humnyamazishi, ni mwepesi kukuelewa kama  jibu lako limejitosheleza........... hata kama hujamruhusu kufanya atakwambia am not doing it coz my mumy doesnt like it, na atarudi kukwambia mumy .......... told me to do this n that but i said my mumy doesnt like it( kwa hapo Dada mtu huwa anakoma dogo anavyo mdispline). hii kitu nimeipata hata kwa walimu wake, mwalimu  asi introduce kitu kipya halafu yeye awe hawezi atamkalisha huyo mwalimu chini mpaka ahakikishe ameweza otherwise ni kilio.Akisha jua hanaga time na mtu.

 Sasa Mama yake nilikuwa nampotezea sana maswali yake ya huyu Mwalimu wake ila nilikuwa namtumia kwenye kumuandaa, ili asijicheleweshe namwambia leo unaenda kumuona mtu fulani weee!!! tutatumia mda mchache sana kujiandaa(kina mama mnanielewa eeh) mpaka hiyo siku ilipofika nimeenda kumpeleka  bwana,!!!!!!! nikamuona huyo mwalimu mie huyo kuogopa maswali nilivyoona anamkimbilia tu nikaomba kiss ya faster faster niondoke , sijafungua mlango wa nje nasikia Mumy,Mumy,Mumy wait ile kugeuka yuko na Mwalimu very serious ananiambia, Mumy now take ..............'s phone number, so you can ring to invite her to our house.(kuumbuana sasa maana sikupewa nafasi yakujitetea zaidi yakutimiza amri mda huo huo?)  na hiyo siku ikawadia  kama mnavyoona.

Hamna haja yakumuona huyo mgeni eti eeeh!! habari kamili ni juu ya mwanangu mie na ndio hiyo................. ntamkumbusha siku moja akikuwa jinsi alivyonishughulisha.
Mama wawili nilipumzika vile vishughuli vya mezani walihudumiana wenyewe kwa wenyewe
no pink plate & cup  kwa siku hii maana nilihisi ningeambiwa  na mgeni nimpe visahani vya kitoto maana nilivyosema leo mnatumia sahani hizi nilimsikia akisema yeah!! we are having the same plate like...........(mwalimu)

Hivi enzi zetu tulikuwa tunawashughulisha hivi wazazi??? hata sikumbuki aiseee lakini nilichojifunza ni hichi hizi nafasi zinasaidia sana kumjua mtoto.............

 ooh!!! sorry nimesema flash back nimejikuta naaandikaaaaaaaaaaaaa.

haya basi nawapenda



6 comments:

  1. i have an obsession for table setting, na hiyo ya kwako imenivutia haswaaaaa!

    Mama C

    ReplyDelete
  2. nje ya mada hucka, mama wawili n wengineo wamuaminio bwana naomba mniaidie kusali kuna roho inaniambia nitakufa pliz nsaidieni nahitaji amani y kristo ndani y moyo wangu inatesa sana hiiiiiiii Roho y ajabu sana nakemea n kusali pia mimi mwenywe nakumbka mwka 2009 ilinitokea mama wa rafki yngu walinisaidia kuomba hyo roho ikasepa kbsa kbsa imerudi tena asante sana n MUNGU awe nanyie....

    ReplyDelete
  3. anonymous please inbox your email.

    ReplyDelete
  4. "zaburi 118:16-17

    16 Mkono wa kuume wa Bwana umetukuzwa; Mkono wa kuume wa Bwana hutenda makuu.

    17 Sitakufa bali nitaishi, Nami nitayasimulia matendo ya Bwana. "


    endele kuamini yesu anaweza yote, kiri na kusimamia huo mstari muda wote!

    ReplyDelete
  5. jamani cjui nitawalipa kitu gn ila Mungu wa Isaka n Yakoba atawalipeni sna n zaidi y sana niko vzr sasa kwa ajili y maombi yenu na huo mstari naendlea kuusema asnteni sana mama wawili nitafanya hvyo kw email mamiii nwe ubarikiwe amani ninayo sasa .....

    ReplyDelete
  6. amen! jina la yesu kristo aliye hai libarikiwe na litukuzwe!

    ReplyDelete