Pages

Ads 468x60px

Friday, May 31, 2013

TUZUNGUMZE

Nikiwa katika dimbwi la mawazo ndani ya week hii nikitafakari nusu mwaka ushapita kuna vitu fulani bado havija kaa sawa..... ninachomshukuru Mungu nina afya,ninakula, ninaamka nakuendelea kufurahia vyoote alivyonibariki LAKINI, kuna hiki kipengele kinachosema NITAKUINUA KUTOKA KIWANGO KIMOJA KWENDA KINGINE   nielewavyo mimi hapa haijalishi upo katika hali gani.......... cha msingi ni wewe mwenyewe kujielewa na kuamini kuwa inawezekana na pia kufanya nafasi yako.( ninaelewa jinsi ilivyokuwa kazi hasa kwa wale waanzilishi mfano unataka kuwa  mfanyabiashara mkubwa lakini huna babu wala bibi aliyekuachia  hata shilingi yakuanzia mtaji kwi! kwi! kwi! patamu hapo lakini pazuri maana siku utafurahia jasho lako) cha msingi usikate tamaa najifunze kuthubutu, kuna wakati niliwahi kuwaza km labda ndoto ninazoziota sio zangu ni kwa ajili ya watu fulani fulani asikwambie mtu INAWEZEKANA. Ninachoweza kusema ni hichi..., NAMSHUKURU MUNGU SANA TENA SANA KWA HAPA NILIPO  MAANA YEYE PEKEE NDIO ALIYETUTOA NAKUTUFIKISHA HAPA lakini sitaki kuridhika na hapa nilipo nataka nishuhudie na nione kwa macho zile ahadi  NITAKUKETISHA NA WAKUU, UTAJIRI ULIYOFICHIKA NI WANGU,FEDHA NA DHAHABU NI MALI YA BABA NA MIMI NI MRITHI, SITAKUWA MKIA BALI KICHWA...................... inawezekana kabisa mpaka sasa hakieleweki na umeshakata tamaa ukidhani ile ndoto haita tokea tena kwa mwaka huu............. ngoja nikutia moyo  kwakukwambia hivi< ndoto yako inaweza kujibiwa siku moja ndani ya miezi kumi na miwili ya mwaka......... usiache kufanya juhudi na kupiga goti.......kiukweli hapa hata Mama wawili bado hakijaeleweka mwaka huu (material things) lakini naamini ni lazima kieleweke nakitaeleweka tuu....... siku hizi shetani huwa hanisumbui kichwa huwa nampa vithibitisho na kumwambia huyu Mungu wangu aliyenibarikia hivi vitu in 3-4 yrs nilivyomwomba na niliviona vitisho vyako shetani lakini ukachemsha huyu huyu ndie atakae nishindia haya ninayoyaomba sasa.......

joke( nimeamua kuachilia baraka zangu simnajua 2015 ndio hiyo naanza kujinadi mapema mkiniona mjengoni mjue kabisa nimeingiaje  kwi kwi kwi! maana msije mkaniita fisadi mtoto) jamani utani unaruhusiwa ikiwa kweli poua........

back to the topic
tuliomba, tukaamini, na tukauona utukufu wa Bwana....... hatujatulia bado tunakaza buti mpaka kieleweke.........HATUTA KUFA MPAKA TUSIMLIE MATENDO MAKUU YA BWANA

MJENGO TUNAOISHI
UGONJWA WA VIJANA
MJENGO TUNAO MILIKI TZ  HAYA........ HII SIRI SIJAWAHI KUSHUHUDIA KIFUPI NI KWAMBA TUNAMILIKI KAMPUNI KALE KAOFISI NINACHOWAONYESHAGA NDANI MWANGU HABARI NDIO HIYO MABOX YANAONGEZA TUU.............USICHEZEE OPPORTUNITY HATA SIKU MOJA HUWA HAIJIRUDII...........



KUMBUKUMBU LA TORATI

28 “Na itatukia kwamba ikiwa hakika utaisikiliza sauti ya Yehova Mungu wako kwa kuwa mwangalifu kutenda amri zake zote ninazokuamuru leo,+ Yehova Mungu wako atakuweka juu, juu ya mataifa mengine yote ya dunia.+ 2 Nazo baraka hizi zote zitakujia na kukufikia,+ kwa sababu umeendelea kuisikiliza sauti ya Yehova Mungu wako:
3 “Utabarikiwa jijini,+ nawe utabarikiwa shambani.+
4 “Utabarikiwa uzao wa tumbo+ lako na mazao ya udongo wako na uzao wa mnyama wako wa kufugwa,+ mtoto wa ng’ombe wako na uzao wa kundi lako.+
5 “Kitabarikiwa kikapu+ chako na kikandio chako.+
6 “Utabarikiwa unapoingia ndani, na utabarikiwa unapotoka nje.+
7 “Yehova atawafanya adui zako wanaoinuka juu yako washindwe mbele yako.+ Kwa njia moja watakuja juu yako, lakini kwa njia saba watakimbia kutoka mbele yako.+8 Yehova atakuagizia baraka kwenye maghala yako ya chakula+ na kila kazi unayofanya,+ naye hakika atakubariki katika nchi ambayo Yehova Mungu wako anakupa wewe. 9 Yehova atakuweka kuwa kikundi chake kitakatifu cha watu,+ kama vile alivyokuapia,+ kwa sababu uliendelea kushika amri+ za Yehova Mungu wako, nawe umetembea katika njia zake. 10 Na vikundi vyote vya watu wa dunia vitalazimika kuona kwamba jina la Yehova limeitwa juu yako,+ nao kwa kweli watakuogopa wewe.+
11 “Yehova pia atakufanya ufurike kwelikweli kwa ufanisi katika uzao wa tumbo+ lako na uzao wa wanyama wako wa kufugwa na mazao ya udongo wako,+ katika udongo ambao Yehova aliwaapia mababu zako kwamba atakupa wewe.+ 12 Yehova atakufungulia ghala lake zuri, mbingu, ili kunyesha mvua juu ya nchi yako katika majira+yake na kubariki kila tendo la mkono wako;+ nawe hakika utakopesha mataifa mengi, hali wewe mwenyewe hutakopa.+ 13 Na Yehova kwa kweli atakuweka kuwa kichwa wala si mkia; nawe utakuwa juu tu,+ wala hutakuwa chini, kwa sababu unaendelea kutii amri+za Yehova Mungu wako, ambazo ninakuamuru wewe leo ili uzishike na kuzifanya.14 Nawe usigeuke kando ya maneno yote ninayowaamuru ninyi leo, upande wa kuume au upande wa kushoto,+ kutembea kwa kuifuata miungu mingine ili kuitumikia.+
15 “Na itatukia kwamba ikiwa hutasikiliza sauti ya Yehova Mungu wako kwa kuwa mwangalifu kutenda amri yake yote na kanuni zake ninazokuamuru wewe leo, laana hizi 

11 comments:

  1. MUNGU AMEKUBARIKI MAMA HONGERA NA JINA LA BWANA LIBARIKIWE SIFA NA UTUKUFU NI JUU YKE MWWAAAAAAA

    ReplyDelete
  2. hongera sana mama wawili.inaonyesha australia sehemu mnayoishi ni posh area.jamani watu wanasema wa australia ni wabaguzi special kwa watu weusi sijui ni kweli.mimi nipo uk,ni fan mkubwa wa home and away na neighbours,vipindi hivyo huwa havinipiti.na nyumba yenu ya tz hongereni.ila jee hayo madirisha ya nondo ni yake ya kufunguka?siku hizi kujenga ni vizuri madirisha hayo ya nondo yawe yana funga na kufunguka for the health and safety,kama ajali ya moto.

    ReplyDelete
  3. dada maneno haya uliyoyanukuu ktk biblia imenifariji sana maana napita ktk kipindi kigumu sana nanimekuwa navunji moyo sana magonjwa majaribu ya maisha yaninikatisha tamaa sana nimekuwa very disappointed yaani nimefarijika sana baada ya kusoma hapa utafikiri unaelewa nanayopitia pasipo msaada wa mwanadamu ni mimi tu na Mungu wangu ubarikiwe sana na jina la aliyetuumba litukuzwe daima ndie jibu la mambo yote

    ReplyDelete
  4. hongereni sana. nipe kazi basi mama wawili

    ReplyDelete
  5. Umenitia moyo! Barikiwa zaidi!

    ReplyDelete
  6. barikiwa mnyalu mwenzangu

    ReplyDelete
  7. Hongera sana dada angu,mi nimekujulia lia humu humu kwenye mablog lakin seriously nakuadmire sana,umenipa moyo na kuni inspire,especially quote zako zimenigusa kumoyo.....endelea kubarikiwa mpendwa

    ReplyDelete
  8. Bwana Yesu asifiwe! Nimependa maelezo yako kuhusu kuangalia na kutembea katika ndoto bila kukatishwa tamaa. Naomba uniulizie ndugu yangu kama naweza pata soko la matunda na mbogamboga toka shamba moja kwa moja. ubarikiwe!

    ReplyDelete
  9. maneno yako yanatia faraja sana mpenzi.Baraka ziwe juu yako.

    ReplyDelete
  10. DAH KWELI UMEUONA MKONO WA BWANA UBARIKIWE SANA

    ReplyDelete
  11. SAFI SANA VAKUBOMA...HAYA NDO TUYATAKAYO

    ReplyDelete