Pages

Ads 468x60px

Sunday, November 10, 2013

NGOJA NIKUTIE MOYO........

Ninachokumbuka ni hichi, japo si kwa kutonesha donda au kubeba yale maumivu niliyopata au kutaka kumjibu shetani kimwili, bali  ni kushuhudia na kuthibitisha ukuu na utendaji wa Mungu katika safari yangu.......................nikisema nibebe yale maumivu  au nitoneshe kidonda au kuenenda kimwili zaidi nitakuwa ni mpumbavu  kwani hayo yote kwangu imekuwa history..............ambayo inaweza kutumika kama muongozo wa kuokoa roho fulani zilizokata tamaa..............

Kwa miaka mitano na ushee nimekuwa nikijitafuta na kila nilichokuwa nakifanya nilikuwa nafanya lakini ndani ya nafsi yangu nilikuwa na msiba  nikisugua goti nakumuliza Mungu ni wapi nilipo, mbona najitafuta mnoo na huku nikijua uweza uliopo ndani yangu ni mkuu  kuliko............ kama mwanadamu nilijeruhiwa na wakati mwingine Mungu aliruhusu wanadam waunipe maumivu zaidi, kejeli na masimango ndizo nilizokuwa nikikutana nazo kila iitwapo leo, na kwa sababu kwa ajili ya upumbavu wangu kuna wakati niliruhusu akili zangu zakibinadam ambazo zilinihangaisha  huku Mungu akiwa pembeni akinisubiri niruhusu uweza wake ufanye kazi......( kuna wakati wandugu kama jambo haliendi fanya juhudi Mungu akusaidie ujue km ni mpango wake ulio halali au ni ubinadamu umekuzidi kiasi kwamba umezuia utendaji wa Mungu juu ya hilo jambo) hili litakusaidia hata kujua muda na wasahaa uliofaa kujibiwa ombi lako.

Wakati niliojeruhiwa zaidi ni pale ambapo  baada ya Miaka minne  ya maombi yangu niliona kabisa dalili za ushindi wandugu nilikuwa nashauku sikuweza kujizuia  na shuhuda zilianza,shukrani kila nilipoguswa kufanya kitu kwa ajili yakumshukuru Mungu kupitia hilo nilifanya, nilitia watu moyo hasa wale nilijua wanapitia kipindi nilichopitia,nakumbuka hata humu ndani nilisema BWANA AMETENDA, kwa mnaonifuatilia mnaweza kukumbuka hili .................... kumbuka hizi zilikuwa ni dalili ombi lilikuwa halijajibiwa japo nilikuwa namatumaini asilimia 100% ......... siku iliyoandaliwa kupewa jibu nikiwa nimekunja nne nikisubiri file kusign jibu lililokuja  SAMAHANI KAMPUNI YETU IKO KWENYE UHATARISHI WA KUFIRISIKA HIVYO UONGOZI UMEONELEA KUTOKUKUSIINISHA.....................

aiseee huwezi ukaelewa hili jeraha mpaka uwe umelipitia mpendwa, kumbe Mungu alikuwa ananifundisha kitu, ( hekima ya kila jambo) kipindi nikiwa na shuhudia ushuhuda ulifika kwa wahusika ambao kwa namna moja ma nyingine hawakuwa tayari mimi kuingia katika hiyo ofisi wakiwa wana siri zao humo  walifanya walivyoweza  nakunithibitishia wao ni washindi kwa jinsi ilivyokuwa nilijikuta ni kimwambia Mungu sijawahi kukuona umeshindwa ila kwa hili umenifanya niwe namashaka,nijuavyo mimi ukitoa hakuna atakae chukua lakini kwa hili umenitatanisha,umesema wewe si mwanadamu hata ukasema uwongo lakini kwa hili naona dalili zakunifundisha uongo, nitaiambia nini ile jamii niliyoishuhudia,( mbaya zaidi nilikuwa napokea ujumbe wa all the best katika hili kwani kila mtu alijua leo ndo napokea rasmi muujiza wangu) nitawajibu nini????? Mungu hawezi au ???????Nilimuuliza mengi kuna wakati nilihisi nimemshika na kumtikisa kwa ajili ya majozi na maumivu niliyonayo...........( piga picha yule mtu uliempenda akiwa mbele yako amekudisapoint halafu unamuliza hakujibu)  hapo nilikuwa sijapata hilo jibu hapo juu la wanadamu waliofanya mbinu zakuharibu ......................

ninachotaka kusema Mungu ni mzazi, Baba wa kweli anajua kukuadhibu na kukurudie kuliko unavyodhani........... cha ajabu alinipa amani sikupokea maswali yoyote na kama nilipokea nilikuwa na ujasiri wakujibu nhaukuwa mpango wa Mungu nausubiri mpango ulio halali bila kureuhusu maelezo mengi............. ila nilizidi kujifunza kutokujishughulikia nakuachia uweza wa Mungu ..............  baada ya miezi kama saba leo Mama wawili nasema Bwana amenilipa zaidi ya matarajio,ameniinua, amenitetea  nimefikia hatua kujiona nilichokuwa nakiomba kilikuwa sio kiwango changu nilijiweka low level mnooo kumbe mimi ni mkuu mnooooo...........

www.stevosdetailing.com.au
 leo Mama wawili naongea lugha za accounts kama mwendawazimu ukisema Cr,Dr,invoice,purchase order sijui myob sijui ma nini na nini hayo yote ndo niliyokuwa namuomba Mungu nikawafanyie watu leo nafanya kwenye kampuni yangu mwenyewe.................... MWACHENI  MUNGU AITWE MUNGU
na kupitia hili naomba mnielewe ninaposema EDUCATION IS ACCESSORY naomba mnielewe huwa sinia kumjibu mtu ila ni kile kitu nilichokipitia na ninavyokicgukulia............

MBARIKIWE
msisahau kutulike kwenye facebook page
stevo's detailing

1 comments:

  1. umeniamsha kiimani mpz..nlikua nayo but ilikua imelala tnx much be blessed always

    ReplyDelete