Pages

Ads 468x60px

Wednesday, November 20, 2013

TUZUNGUMZE....

Wandugu  nimeguswa kidogo naona nilitendee haki kwa kuzungumza na watu wawili watatu walioandaliwa kulipokea hili................

Ndugu zangu tujifunze kutumia nafasi tulizopewa, ninavyoamini mimi kama utashindwa kufanya nafsi yako kwa ufasaha ndoto zako bado zitakuwa ni muujiza usiotendeka, na hili nimelikuta hata kwetu wapendwa  kuna vitu tumekaa huku tukijitetea bado Mungu hajapenda au tunasema tunasubiri wakati wa Bwana............. nakubaliana na wewe lakini wakati wakusubiri Mungu nae anaangalia jitihada zako je umefanya nafasi yako????????

Neno linatuambia tutakuwa kichwa na wala sio mkia,na pia fedha na dhahabu ni mali yetu kwa akili zangu hizi ndogo ni kweli naamini MIMI NI KICHWA WALA SIO MKIA, MIMI NI MRITHI WA MALI ZA BABA, lakini haya hayaji kirahisi ,kuna garama ambayo unatakiwa uilipie  kimaombi,kiutendaji,kiimani na wakati mwingine ukubali maumivu ya muda...............

Leo nimekaa ofisini  kwangu baada ya kikao kidogo na team yangu, nimejikuta nimemtafakari mno Mungu kwa ajili ya nafasi alizonipa katika safari yangu.Nimekumbuka vile alivyoniruhusu nakunipa wepesi wakufagia vyoo vya wazungu  masaa sita mpaka tisa kwa siku, nimekumbuka jinsi nilivyokuwa nazifanya na jinsi nilivyozimudu, nimekumbuka jinsi nilivyofanya mapokezi kwenye hotel fulani na vitu havikwenda sawa ikabidi niache,nimekumbuka jinsi nilivyowaogesha wazee mweee, wengine ndo hivyo hawakupendi, wengine ndo kichaa cha uzeeni, yaani nimekumba hata nilivyoenda kubembeleza hiyo kazi niipate, maana  mwee nilivyoenda mwenyewe nilipeleka kacheti kangu kadegree eti kwa kazi ya wazee walininyimaje sasa?????? 

Libarikiwe jina la Bwana aliyemwinua mtu kutumika kwa ajili yangu, yaani we bidada ukinisoma hapa nakupenda mimi wewe hujielewi tu, kweli ulitumika mnoo na Mungu alinichagulia the right person, Mungu wangu akukumbuke na kukutetea my dear. huyu Dada aliingia kwa Boss wake nakumtolea chozi kuniombea kazi .........Boss akasema aje ajitolee siku tatu nimuone kwanza, huyu na hichi cheti chake atatukimbia soon. Nilipiga mzigo huo boss mwisho wa siku aliniambia mwenyewe nimepata kazi, hakuna haja ya kujitolea tena (chezea mtoto wa mkulima wewe) ,kiukweli natafakari ule mzigo hata mimi sijielewi ukizingatia sina experience yoyote  mwisho wasiku walinisomesha wenyewe  na cheti walinipa. (so watu wangu wa USA & UK nakuja holiday huko  ntakuwa navikamata vishift kiaina kwi! kwi! kwi!) najiuliza kwa nini Mungu aliruhusu hayo yote????? kwa nini alitaka nipite huko na hali angeweza kunifanya nipate kazi fulani @ list hata bank teller inayolingana na cheti changu kidogo? nakumbuka kuna kipindi nilikuwa naenda Bank naaanza kujisemesha na bank teller ili nijue viwango vya vya elimu narudi kwenye gari nalia huku na muuliza Mungu hivi mi ni mburura kiasi hiki hata hii kazi umeshindwa kunipa???? nakumbuka nilifanyiwa interview kadhaa mwisho wa siku NO!!!!

BILA SHAKA NAONGEA NA MTU NA UNANIELEWA. ninachotaka kusema Mungu aliruhusu niingie huko ili nikatumie nafasi  na aliweza kunipa neema yakuitumia vizuri. ningeweza kusema kisa chakuhangaika baba watoto anaweza kuniwezesha nikakaa nyumbani na kulea kama wengine,au ningeweza kusema sifanyi chochote kisicho hadhi yangu huku nikikaangalia kaelimu kangu na kubaki kusugua goti mpaka Mungu anipe cha hadhi yangu, au ningechagua kazi kwa kuhofia bongo wakisikia nalea wazee kutoka officer fulani bongo mbona aibu!!! hayo yote yalikuwa na sababu kamili. Mungu wetu aijuaye kesho yetu na yeye atuwaziaye aliyo mema alijua mimi ni nani na kipi kinanistahili nikifanye.........................na kuna nafasi zingine nimekaa najiuliza hivi leo nikirudishwa nitazifanya kwa umakini ule??? kumbe Mungu alitaka nijue maumivu na utamu wa kazi za dizaini hizi, alikuwa ananiaanda jinsi yakukabiliana na vijana wangu wakazi, alikuwa ananianda kujua utu hasa ukiwa kwenye sehemu fulani ya mamlaka, alikuwa ananiaanda kuwajibika na kutofautisha baadhi ya mambo kama kuweka undugu na kazi na mengineyo meeeengi..........

Baada yakuwaza haya nimejikuta nikijisemea moyoni, kuna wakati hatufikii malengo kwa sababu tunaweka vizuizi sisi wenyewe na pia tumekua tukitii sana sauti za wanadamu kuliko kusikiliza nini kusudi la Mungu katika maisha yetu.........na mwisho nikajisemea mimi ni mimi ntabaki kuwa mimi nachotakiwa ni kujitambua  na kuruhusu yale yaliyoandaliwa kuwa yangu bila kujifananisha na mtu yeyote........

BEYOU
Wewe ambaye hujaelewa ujue huu ujumbe haukuwa wako please pita kimya kimya bila kuchafua hali ya hewa
 otherwise nakupenda endelea kututembelea na Mungu wetu akubariki


13 comments:

  1. Ubarikiwe Sana da'Rose.. na MUNGU azidi kukufunulia.
    Yaani Umetumwa!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Wow luv, bonge la ujumbe aisee, umenipa moyo Na nimejifunza kitu. Ubarikiwe sana. Hongera kwa kijitambua na kushare nasi ulikopitia, waliopo huko kwa sasa watakuwa wamepata nguvu zaidi. Barikiwa zaidi mama.

    ReplyDelete
  3. Love u mingi mingi..

    ReplyDelete
  4. Hilo halina ubishi ahsante ingawaje ni mgeni humu nimejifunza kitu msg delivered nimeipenda ghafla bloy yako!

    ReplyDelete
  5. Maneno yako huwa hayana ushirikiano hata kidogo....ngoja nikuulize ndugu degree uliyosoma ni ya nini...na mwakagani..na chuo gani..au ile biashara yako ya kuzengea hostel ndo unajipa moyo ulikuwa miongoni mwa watahiniwa? unajua ukiwa muongo usiwe msahaulifu.......huruma sana....

    ReplyDelete
  6. ma mdogo nimekuachilia ili uendelee kufunguka kidogo maana sijielewi japo mimi ndo muhusika......nakupenda bureeee

    ReplyDelete
  7. Kweli huyo umemweza, napenda unavyomjibu atasema mwisho wake atachoka. Kuna msemo usemao kuwa "usibishane na mwendawazimu" mwache abwabwajike wewe life inasonga mbele. Watanzania inabidi tupendane wivu hautatufikisha popote! Hiyo degree yake akwambie ili iweje? Hayakuhusu dada!

    ReplyDelete
  8. Hongera Rose kwa kukubali kutumika kama chombo cha Mungu kwa ajili ya watu wake. Kwa hilo Mungu ameendelea kukuinua sambamba na ahadi zake. Mimi nimejiunga rasmi kwenye boti yako na ninabarikiwa sana na huduma yako. To God be all the Glory.

    ReplyDelete
  9. Huwa nakupenda sana Rose. unaniinspire sana..na ninabarikiwa mno kila napokuta umeweka maneno ya kutufundisha na kututia moyo. Mungu azidi kukuinua.

    ReplyDelete
  10. Jamani, hadi nimetoa machozi. Ubarikiwe ulichokisema ni kweli kweli tupu, tujadi.mwacheni Mungu aitwe Mungu, unaomba unasubiri na pengine unakata tamaa, HAPANA USIKATE TAMAA MUNGU HUTENDA KWA WAKATI WAKE. USICHOKE, ANASEMA 'NIKUMBUSHE, TUJADILIANE" kiukweli nasema rasmi...SHETANI NI MWONGO SANA. thanks for inspiring, be blessed.

    ReplyDelete
  11. watu wengine kwa kweli sijui huwa ni wagumu kuelewa au ndo vipi maana sidhani kama hapo degree yake inakuhusu rose ma dear kila nikiingia humu huwa najifunza kitu kutoka kwako na huwa nakumbuka kumuabudu mungu wangu aliyenitoa mbali, japo mafanikio yangu si makubwa lakini nasema asante mungu wa Israel aliyenitoa mbali , Rose ubarikiwe na bwana Mungu aendelee kukupa nguvu na afya iliyo njema uendelee kututia moyo sisi tunaoelewa nini unamaanisha katika maandiko yako. cheers

    ReplyDelete
  12. DADA ROSE NAOITIA ULIPOPITA! NA SIJUI KWANINI NIMEFUNGUA BLOG YAKO! NMEJIKUTA NALIA! IMAGINE HAPO PEPAZ SINA! NNADEGREE YANGU ILA BADO UNABEMBELEZA KAZI ZA AJABU! EEH YESU! YOTE HAYA NAFANYA ILI FAMILIA YANGU IPATE KTOKA KULE UCHOCHORONI! ILA BADO NAONA SIFIKI! ILA NAAMINI LEO NI SIKU MPYA KWANGU ! YA KUMTAZAMA MUNGU KWA JICHO LA TOFAUTI AISEE

    ReplyDelete