Pages

Ads 468x60px

Tuesday, November 5, 2013

NA IWE HIVYO KWA NEEMA YA MUNGU...................

Wapendwa wote ambao huwa mnani inbox ujumbe wa dizaini hii......... kwa kweli Mungu awabariki sana mnanifanya nitambue nafasi yangu nje na familia yangu na wakati mwingine wengi wenu huwa siwajibu  ni kwa sababu  kuna wakati huwa naogopa kulewa sifa za dizaini hii, zisije kunitia kiburi na kupoteza kusudi na mpango halisi ulioandaliwa kupitia mimi.................. na hata hivyo huwa najiona natakiwa kufanya zaidi ya hiki kwa ajili ya utukufu wa Mungu........................ nazipata inbox zenu wote na wengine huwa mnanifanya nibubujike na machozi kila ninaposoma......... mbarikiwe mnoo....... tuendeleze safari makamanda.

Hi,
Mimi naitwa ..................... ni mtanzania, ambaye kwa neema ya aliyetushindia msalabani, neema hiyo nami imenipitia kwa maneno mengine ni mpendwa.
Ukweli ninaguswa sana na ulichoandika na jinsi ambavyo unavyojieleza kwa sehemu umefanyika ni njia ya kunitoa katika eneo fulani kwenda eneo jingine, wewe ni mwanamke jasiri mwenye maamuzi na ni mwanamke mwenye maono ya kufika mbali ili umuinue Mungu na wengi wamuone kupitia wewe, unajua Mungu ni wa ajabu sana yeye hutafuta mtu ili awe sababisho la mwingine kutoka aliko na kuingia eneo ambalo Mungu anataka aingie na ni kwa kusudi lake au sababu alizonazo Mungu mwenyewe.
Kitu kingine ninachokiona kwako ni kuwa ndani yako una hofu ya Mungu na unapenda sana kufuata muongozo wa Mungu anaokuongoza, imani, na msimamo wako kwa kupitia tu kusoma kwenye blog yako ukweli unanipa kujifunza na kupenda kusoma kila siku kwa kila unapoandika kitu kipya mimi hujifunza na kupata kitu cha kunisaidia.  Sikujui wala hunijui lakini ninachokiona kwako kuna kitu cha thamani sana ambacho Mungu amekiweka ndani yako ili yeye Mungu ajitwalie utukufu - Mama wawili kaza buti ili KRISTO ainuliwe hata katika mipaka ya mbali, na huko uliko ni kusudi haswa la Mungu wewe kuweko huko.
Kwa leo naishia hapa, Mungu Muumba wa Mbingu na Nchi na ianulie juu sana.
Nakupenda.

No comments:

Post a Comment