Pages

Ads 468x60px

Thursday, April 10, 2014

WAKATI WA MAPITO............


Kumekucha wapendwa wangu, Napita mwenzenu leo hii nimepokeaje habari mbaya??????? ( si huwa nawambia na habari nzuri eeh??? hii ya leo kama bado naota vile ni mbayaaaaaaaaa kibinadamu lakini  naamini kuna mlango waakutokea) ni habari ambayo ukiweka  mezani Mtu lazima uchanganyikiwe aiseee na hata nikiwaambia  halafu nisiwape upande mwingine wa karatasi  Mnaonipenda mtaliaje sasa, mtanihurumiaje sasa  na shetani atafurahiaje sasa?????  of course nahitaji maombi yenu wandugu. Nahitaji mtu wakupiga magoti na mimi. nahitaji ule uweza upitao akili za binadamu wote.  nisingependa kuhurumiwa juu ya hili maana ninaamini kuna ushuhuda mkubwa  mbele yangu.............. unajua nini?????? maisha yangu yote sijawahi kupita kwenye mteremko kila unaloliona ndani yetu  lilichakachuliwa, kunolewa, na kupitishwa kwenye moto. nanilipo toka kwenye hilo jaribu nilisema,KAMA SI BWANA NI NANI????????? 

 Tunamshukuru Mungu sana kwa hili alituandaa bila kujielewa, hatukujua, na bado hatuelewi. Yawezekana tuwahi kuwaza kwa namna ya tofauti lakini Mungu alijua zaidi.(YEYE NI MUNGU ATUWAZIAYE YALIYO MEMA). kwa kweli alituandaaa..........

 Wapendwa wangu, ni maombi yangu kwenu,unapopiga magoti kuniombea hili kwa uaminifu naomba Mungu akafungue milango yako. milango ambayo siku kama hizi zikitokea uwe na backup aiseee,yaani awe amekuandaa fulani,(KWA KWELI JINA LA BWANA LIBARIKIWE) hata kama itakustua fulani, kwa namna ambayo mipango yako itavurugika kwa muda( simnajua Shetani anachelewesha ila hawezi kuzuia moja kwa moja)  lakini isibadilishe sura kamili.Wapendwa wangu naomba Mungu wangu aliye Hai akawawezeshe  kila mmoja wenu, akawape Hekima juu ya hili aiseee. naamini Yeye ni Mungu asiyetuacha tukaabika, lakini hizi backup ninazozisema mimi nimeona wengi wetu tumefungwa juu ya hili, tunaridhika........... na kama tumeridhika maana yake huna muda wala jitihada za kuliombea............Hivi unajua kuna vitu Mungu hawezi fanya kama hujamruhusu aingilie kati?????  OMBA KWA UAMINIFU

 Ninavyoamini mimi NITAPANDISHWA KUTOKA KIWANGO KIMOJA  KWENDA KINGINE . Hili halina mjadala hata shetani analijua, Sasa hutu tumajaribu jaribu  tunapojitokeza katikati ya mbio tunatupumzisha tuu, maana mbio zake  na vita vyake si mchezo shetani hatazamiki huko aliko........Kwani tulipataje ule ushindi msalabani???? haikuwa rahisi aiseee. najua YOTE YALIKWISHA  lakini je tunaukamilifu wakutosha kiasi kwamba tusijaribiwe???? Tunawakina Samweli  ambao tangu watoto walianza kupata misuko suko lakini wapi uliposoma ukaambiwa NDOTO ZAO HAZIKUKAMILIKA na wapi uliposoma ukaambiwa WALIOZUIA NDOTO WALIFANIKIWA MPAKA MWISHO?????? na vipi DAUDI, Sauli alifanya afanyalo, alitumia mamlaka, na hata alimwaga Damu ili kupoteza lengo kamili lililoandaliwa juu ya Daudi, vipi kwani alifanikwa???? au mbio tu za sakafuni??? sasa mimi ni nani hata niishi kimteremko?????? WAPENDWA NILAZIMA TUTAMBUE KUNA WAKATI WA KUPIKWA   sasa ni juu yako wewe umelipokeaje?????? na umejiandaje kukabiliana nalo???

 ukiniuliza nimelipokeaje??? ofcourse nimelia, mimi si mwanadamu Mbona hata Yesu alilia pale msalabani alisema kama nilivyojisemea mimi  leo mara baada ya taarifa MUNGU WANGU, MUNGU WANGU,MBONA UMENIACHA !!!!!!! ni ubinadamu tuu................



 Nina meeengi hayaishi ila  nimekaa hapa jamani najiuliza hiyo mipango tuliyokuwa  nayo kichwani in the next few months duuu!!!  naomba nikubali kwamba huu ni mpango kamili ulioruhusiwa yaani!!!!! nasikia sauti kabisa ndani yangu ikiniambia TULIA TULIA TULIA ( punguza kasi, Punguza kasi)  niaminivyo mimi hii sauti ningeisikia kabla ya hili pito ningeipotezea aiseee nakuikemea bila kujua unamkemea roho mtakatifu( imewahi kukupa hiyo????) kwi! kwi! kwi! all  we need ni hekima na jinsi yakukabiliana nalo baaaasiiii.

OTHERWISE TUPO POUA SANA. TUNAHESHIMU MAAMUZI YA MUNGU tunayaheshimu. maana YEYE NDIE ALIYETUTOA NAKUTUFIKISHA. ATUPAYE FARAJA NA KUTUSIMAMISHA TENA. YEYE ATAKAYEFANYA HILI KUWA HISTORIA NA USHUHUDA WAKUMUINUA YULE ALIYEKUSUDIWA. 

Angalizo, labda nisingetakiwa kufunguka hili, lakini nimejikuta najiuliza kama huwa nawashirikisha baraka kinamna fulani kwa nini na hili nisiliseme ili tujifunze??????. na wakati nimekaa mkao wakupokea zaidi maana naamini ni lazima kuna mlango wakutokea sasa nikija na ushuhuda ntaanzaje ili muelewe??????

 MBARIKIWE

4 comments:

  1. Pole mama wawili, Mungu yupo. Ni nini mbaya jamani?

    ReplyDelete
  2. AMINA DADA ROSE POLE SANA DADA AN GU NA AMINI UTAYASHINDA YOOTE KATIKA YEYE ATUTIAYE NGUVU NININI JAMANI MBONA UMENISTUA MDOGO WAKO

    ReplyDelete
  3. Nyamahemba wankuruApril 11, 2014 at 9:02 AM

    Pole jamani tupo pamoja sana. Mimi ni mmoja wa wanaokupenda mno. Mungu akakupiganie nawe utanyamaza kimya, Kutoka 14:14.

    ReplyDelete
  4. Lolote liwalo kwa kua Mungu ametangulia mbele yako litafanyika okuwa dogo sana.

    Ni nani aliamini kua Goliat ataangushwa na bwana mdogo mwenye siraha hafifu

    kwa Mungu yoote yanawezekana
    utashinda hili pia.

    Pole Rose

    ReplyDelete