Pages

Ads 468x60px

Wednesday, March 5, 2014

KUTOKA KWA MDAU............


Tafadhari rejea post  ya tarehe 18/02/2014 (SEMA NENO) ili kuelewa huu ujumbe..... 
MBARIKIWE
Asanteni kwa ushauri wenu mmenifanya niishi tena

Nachukua nafasi hii kukushukuru wewe dada Rose na wasomaji wako wote kwa ushauri wenu aisee nimefarijika kwa kiasi na kujiona nathaminiwa na kuna watu wana matatizo makubwa ila bado wanaishi kwanini mimi nikate tamaa mapema hii. Asanteni sana niko vizuri kiasi naanza kupata nafuu na machungu moyoni yanapungua pungua na imani yangu pia inazidi kuongezeka. Unajua wapendwa unaweza kumshangaa mtu na maamuzi yake n.k ila usiombe upate tatizo maishani mwako kanisani utaenda utaongea na watu, utashauriwa ila mwisho wa siku utabaki mwenyewe mwanzoni nilikuwa vizuri sana tena nikawa najifariji. Siku zikawa zinaenda ikiwa mwaka hadi mwaka wa sita umevumilia tu pekeyako unawaza unajaribu mpaka mwisho wa siku unatafuta solutions mwenyewe kichwani ndio maana nikafika hatua ya kutafuta msaada wa zaidi ninaoupata kwa watu wangu wa karibu. Wengine mlinishangaa eti najiua ni uamuzi mgumu sana hata binafsi yaani unakuwa umepitia mengi mpaka kufikia huko umeshachoka kichwa kabisa. Binafsi nilianza taratibu kukata tamaa bila kujijua taratibu nikawa sio smart tena kama zamani kichwa kinauma sana, stress ndio usiseme, nikanenepeana hadi sitamani kujiona yaan ni mambo kibao nimepitia lakini najipa moyo kwamba na hili litapita. Imani yangu ikaanza kupungua nikawa nasikia sauti inaniambia kwanini usife tu kila mara uwezi amini nimenusurika kugongwa na gari mara nyingi nimeshanusurika kupata ajali mara nyingi. Nakumbuka siku moja nikiwa naendesha gari naenda ofisini na mawazo yangu tele ile kustuka niko darajani nimenusuka ile sauti ikanirudia tena kwanini usikanyage mafuta tu kwa spidi uingie darajani kwa spidi? nikajipa moyo nikatoka eneo hilo mpaka ofisini, Ilifika wakati nikaacha hadi kuendesha gari jamani nasimulia haya yote ili watu nimepitia wapi mpaka kufika nilipokurupuka nakusema trh 28/2 najiua. Ni stori ndefu na ya kusikitisha ila nawashukuru sana mmenifanya niishi tena na naendelea vizuri na pia naombeni maombi yenu zaidi niweze kupata hao watoto jamani 

4 comments:

  1. please mama wawili usiweke jina katika hiyo comment coz nimetuma kwa kutumia my account bila kujua plssssssss

    ReplyDelete
  2. Asante mama wawili God bless you.

    ReplyDelete
  3. God is good all the time; nimefurahi kwa ajiri yako mpendwa na Mungu azidi kukupigania its seems kuna roho ya mauti hapo inakunyemelea inakuandama thats why unakuwa hivyo so u have to kemea hiyo roho kila mara na ukiwa unapata hayo mawazo kemea usijiulize mara mbili mbili kemea mpka uone hiyo hali inaondoka na uvunje hiyo roho kuanzia kizazi chako cha kwanza mpka cha nne ikianzia na babu wa mababu zako inawezekana ikawa ktk ukoo wen u kuna mtu alijiua so ile roho bado inafatilia .otherwise mshukuru Mungu kwa kila jambo. na mama wawili Mungu akubariki kwa kutumika kwa kazi yake

    ReplyDelete
  4. Mungu atukuzwe na sifa apewe. Mungu ni mwaminifu dada zidi kumuomba kwani anajibu maombi. Mbarikiwe washauri wote na pia wewe mama wawili. Mungu ni pendo

    ReplyDelete