Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 29, 2013

TUZUNGUMZE


Wandugu mnalazimika kumsamehe Mama wawili yaani hii miezi miwili yuko busy mno ...........anahitaji maombi yenu pia, chochote atakacho post au akipitisha siku bila kupost tafadhali mnielewe................. sijafulia lakini (ha! ha! ha!) niko jikoni napika chakula kizuri ambacho sitaki kuwanukisha harufu bali nikiweke mezani tule wote natushukuru kwa pamoja na kumwinua Mungu wetu zaidi na zaidi na zaiiiiidi...............( angalizo linaweza kawaida kwako lakini kwangu ni ushuda!!!)na hata hivyo BADO YEYE NI EBENEZA ALIYEKUWEPO,ALIYEPO NA HATATOKEA MWINGINE ZAIDI YAKE.


Turudi kwenye topic yetu

Mwanadamu anakosea na hakuna aliyemkamilifu bali ni neema ya Mungu inayotuwezesha na kutufanya tuwe watu wa toba kila siku.... na kwa sababu hiyo wengi wetu tumeshindwa kujitambua  nakutupelekea kufanya ndivyo sivyo..................

kuna upepo ambao unapita kwa kipindi fulani ambao unaweza kupewa majina meeengi mabaya mfano,(mchonganishi,muongo,mchawi,malaya, na mambo km hayo) na  ukijichunguza mwenyewe unajijua kweli iliyopo ndani yako......... nazungumza na wale sasa ambao wakijichunguza kwao ni kinyume na lile jina walilopewa na mara nyingine unachogundua kwamba hili jina nimepewa kwa sababu ya kitu fulani ambacho wahusika walilipokea vibaya , au ulishindwa kulifikisha vizuri kwa wahusika au wahusika wenyewe wameamua kuliweka hivyo lilivyo kwani  ni njama halisi iliyopangwa na wanajua wanachokifanya.............mbaya zaidi neno lolote la uongo huwa linavuma mnooo, ndani ya saa moja Tanzania nzima imeshajua. niliwahi kumsoma kaka yangu mmoja facebook alisema hivi ( mara nyingi uongo unavuma km upepo ila ukweli unapanda ngazi taratibu ipo siku utafika kileleni)

ninachotaka kusema ni hichi tumekuwa tunapoteza sana mda ili kuufanya ukweli ueleweke, tumeumiza akili zetu na mara nyingine hata kuwa watumwa wa jambo fulani ili tuu yule aliyekuelewa tofauti ajue kweli, ni kweli katika kila livumalo kuna nafasi yako unayotakiwa utumike, labda kwa kusema kitu kitakachofanya watu waelewe au kuomba msamaha,lakini uwe nakiasi usilazimishe sana  mara nyingine hivyo ndivyo ilivyotakiwa iwe kwa muda fulani kwa ajili ya ushuhuda fulani, kumbuka kuna watu wako kazini na hawako tayari kupoteza ajira zao kwa kuruhusu kweli yako........

nijuavyo mimi nikikukosea nikakuomba msamaha kwa kumaanisha baada ya muda tena lile kosa bado linaendelea kutumika km silaha yakukujeruhi ,nikimaanisha aliyetakiwa kukusamehe alikusamehe kwa sababu alitaka kuonesha watu amekusamehe au kwa sababu ya mazingira fulani iliyompasa kukubali lakini ndani ya nafsi yake bado lipo nalinazidi kuota mizizi......... wanasema chapa lapa au funga vilago vyako na usonge mbele ukajitafutie amani ya roho na kufanya yako...............huo sio muda wako wakuitwa majina mazuri ........ by they way hayo ni majina tuu hayawezi kuondoa ule uhalisi wako kama ukijitambua na kusonga mbele...................LAKINI kama hujajitambua mbona unaweza kuitwa chizi unavyojiongelesha peke yako!!!!!!!!!!

BEYOU!!!!

2 comments:

  1. Ahsante mama wawili kwa ujumbe wako nami nimeonja joto ya jiwe baada ya kusingiziwa issue fulani na mtu ambaye sikuwahi kujua kumbe ananichukia kwa kiasi kikubwa sana.
    Aisee sikuamini masikio yangu ila nacho mshukuru Mungu kila mtu amejua kuwa bidada anatunga tu uongo ili kuniharibia na najua atashindwa kwa jina la YESU!!!
    Message yako imenitia moyo sana!!!!
    Ubarikiwe sana Rose.

    Mdau wa Musoma

    ReplyDelete
  2. hata mimi hii mada imenigusa sana kuna ndugu yangu fulani aliwahi kuambia uongo na mtu ambaye ni ndugu yetu pia sasa badala ya kuchunguza ajue ni kweli au la!yeye ameweka rohoni chuki kwangu hakiishi ktu kidogo tu ugomvi ukijaribu kuchunguza huu ugomvi hauna mbele wala nyuma alimradi tu maudhi sasa nakaa najiuliz nini nijishusha chini tuelewane tunaelewa siku mbili inarudi palepale tu sasa kitu nimegundua hanipendi kabisa sasa simwombei mabaya wala mimi simchukii kama yeye anavyonichukia bure maana hilo jambo analozani mimi nimemfanyia nikuja kugundua ni ya uongo kabisa na sasa haniamini hata kidogo lakini sijali maana huyu aliyeniumba anajua ukweli wangu sas nakaa naye mbali nilikuwa nimemuami kama mdogo wangu na kumpenda nijua shida yake ni yangu kumbe mwenzangu yuko mali sana mimi nataka nikaae naye kama jirani tu sio ndugu sitaki kuwa karibu naye sana sitaki kuwa mbali naye sana kwa ujumla mazoeya sana nimepunguza dunia ya sasa imeharibika hakuna cha ndugu wala nini kwekifupi hii mada imenigusa sana asante sana dada rose ubarikiwe sana

    ReplyDelete