Pages

Ads 468x60px

Tuesday, November 11, 2014

USHUHUDA........

Haya ndugu zangu mi ni mmoja kati wale ambao inapofikia kwenye neno la Mungu,  huwa sijishughulishi sana na vitabu zaidi ya Biblia yangu , ukiniona nimenunua ujue labda tu nilitaka  kuchangia tu nakumtia moyo muhusika, mi mwenzenu Biblia  huwa naona imejitosheleza.................. Kwa kusema hivyo sijasema tusisome vitabu vinavyoambatana lakini inabidi tuwe makini sana maana duuu!!!! wandishi siku hizi tuko wengi mjue??? Ki  ukweli unahitaji Roho wa Mungu akuongoze, ujue muandishi aliandika kwa kuongozwa au kwa hisia  na mara jingine huwa no kuongozwa wala hisia wanatumika ........mpaka ukaje kujua  umechelewa  na umeshajifunga kwenye maagano  ( nilimsikia Teddy Kalonga juzi kati yalimkuta sijui picha imeendeleaje best yangu, simuoni Instagram lakini namuelewa sana........ ni kazi sana kujua siri ya mtu anayetumika na yeye anajua kabisa yuko kikazi aiseee)

Ilishawahi kunikuta kipindi fulani kuna mtu akanishawishi kuingia kwenye maombi kwakuongozwa na kitabu cha nabii fulani hata simjui nilielekezwa ninunue online.... Duu nikaenda kununua hiyo kununua tuu masharti kitabu hakitakiwi kushare na mtu ye yoyote zaidi ya mnununuzi, na pia kuna stage ukimaliza hiki unatakiwa ununue kile mmmh!!! haya nikanunua   kilipofika nyumbani huo mwanzo tuu masharti ya Muda wakuomba ni lazima yazingatiwe,unapotakiwa kusema hiyo sara unatakiwa kutamka kwa sauti..........  mmmh!!! Biblia yangu inasema unapoomba uingie kwenye chumba chako cha ndani na Mungu wetu anasikia (kwa uelewa wangu Maombi yangu yasiwe kwanzo kwa wengine) sasa wanangu, Mume wamelala  mimi napiga kelele saa sita za usiku kisa ndo masharti ya sara,chakuchekesha zaidi ukimaliza hiyo sara hadi kizunguzungu unakipata......!!!! mpendwa huchelewi kujipa moyo duuu!! leo nimemponda shetani hadi nimesikia kizunguzungu kha!! wapendwa na sio sa nyingine!!!!!

mwenzenu mwisho wa siku nilichoma moto !!!maana siongozwi na masharti bali kwa roho mtakatifu. 


Anyway,
 Wiki mbili tatu zilizopita nilibahatika kumsikiliza huyu mtumishi wa Mungu JANINE KUBALA. usiku kabla ya siku kuna vitu fulani nilikuwa navitafakari kwa namna fulani fulani...Nilichomshangaa Mungu ile asubuhi nimeenda kumsikiliza huyu mtumishi, ni kama alitumwa aje anipe yale majibu ambayo nilikuwa nayatafakari usiku uliyopita,  na baada ya hapa alianza kutoa ushuhuda jinsi na namna ambayo Mungu alimuokoa mpaka hapa alipo.

Wapendwa wangu, huyu Dada niliona kama niliwahi kumsimulia ni jinsi gani hii Neema ya Bwana ilivyonitoa kwenye shimo la takataka yaani sijui nisemaje??? kilichonifanya nitofautishe ni yale mazingira  aliyofanya nakupitia hayo, Vinginevyo ningemdai $$$$ zakutumia ushuhuda wangu wakati sijamruhusu ha!ha!ha!  Kitu ambacho sijawahi kujionea aibu inaponibidi huwa nashare bila kumugopa wala kumuonea aibu mtu........ ila mara jingi ninapo share hasa nawapendwa wenzangu  najionaga kama mimi ndo nilikuwa mtoto mbayaaaaa....... Unajua kwa nini??? ngoja nimsome huyu Dada nijue kama niwazacho mimi na yeye ndicho alichokuwa nacho. 

ntakuja kushare hapa......

Kiukweli amenifanya nikinunue hiki kitabu chake nijue zaidi hasa pale kwenye ushuhuda. 

 Nanikikimaliza hichi ndo kitabu changu cha kwanza kukisoma nakukimaliza.

3 comments:

  1. Umesema kweli kabisa mama wawili mi mwenyewe kuna wakati mpaka nikasinzia kisa maombi yaliyokua yakiongozwa kwa kusomwa kwenye kitabu. Mjomba (mchungaji) alisoma kwa nguvu nasi kurudia alichokisoma kwa sauti maombi yalianza baada ya chakula cha usiku duh nikikumbuka najichekea mwenyewe mana mtu unaongea huku unasinzia alafu maombi marefu kweli.

    ReplyDelete
  2. yaani umenikumbusha mbali ! enzi za A-level mweeeeh kuna mdada alikua anasalikwa nabii....... akaona aitishe kikundi cha Maombi halo shuleni kwetu bila matatizo wapendwa tukajumuika shughuli ilianza kwenye Maombi hayo maana kulikua na hivyo vitabu vya Maombi kutoka kwenye kusanyiko lao hayo masharti take sawa mweeeh! kifu nikwamba sikumaliza siku tatu nkajiondoa .... Mwenyezi Mungu anisamehe kama nilikosea aiseee!!

    ReplyDelete
  3. Dada rose unanibariki jaman na maneno yako Mungu azidi kukutumia dada.

    ReplyDelete