Pages

Ads 468x60px

Tuesday, November 4, 2014

I AM INSPIRED........................

Wandugu mmenisikia mara nyingi nikisema natamani vi kilo viwili vitatu kwenye huu mwili.......  Na kama ni kuchagua kati ya kupungua au kubaki hapa nilipo aiseee  i can do anything kuhakikisha usinishushe kwenye hivi vikilo najionaga kama niko kwenye danger zone kwi!kwi!kwi!.......... na hiyo ndosababu pekee inayonifanya nitamani nipate vikilo vingine viwili vitatu....... lakini visizidi vitano khaa!!! Msinielewe vibaya huwa napenda sana kumuona mdada ana umbo lake balaa halafu yuko curved  (yaani mbele flat nyuma mzigo wa haja) Ila sijawahi wish kuwa mimi!!! nahisi kwa sababu hata huto  tukilo tuwili ni shughuli kutupata ha!ha!ha!ha!

 Anyway sasa kuna siku nilimsikia Flaviana anasema mwili wake ndo kama wa Mama wawili hata ulishe vipi  hauna majibu ila ukiunyima kidogo ni full kuonyesha mifupa........  duu nikajipa moyo kumbe tuko wengi eeh!! mwili wa Mama wawili nikitaka kupungua nipe wiki tuu utanihurumia!!!!ndo maana huwa najiona niko kwenye danger zone...... Sasa kama mwezi nikamwona Flaviana instagram anatupia vipicha vya namna hii....... Duu!!!! nilimuoneaje huruma???  nikajisemea hata kama kazi yake inamuhitaji awe mifupa mmmh!!! nikaendelea kumchungulia nione hatima yake ...........wakati huo huo juzi kati nilitakiwa kwenda mtaa wa pili mwendo kama wa dk 5-7 nikaamua kutembea yaani nilifika hoi  nahema utafikiri nimepanda mlima kitonga!!!wakati wakurudi nilitamani hata niite tax imagine!!!!

Basi bwana nikagundua kuna haja ya mazoezi otherwise nakaribisha vingine........ So Yes nimeendelea kumfatilia nikagundua kumbe unaweza kumaintain na bado ukafanya mazoezi, Jana nikafanya maamuzi nikaingia huko kwenye mijengo nimejiandikisha nna trainer wangu mwenyewe ila amesisitiza kama nilikuwa nakula milo mitatu  nahitaji kufanya mitano snacks between the meals ndo mpango( Guess what!!! Baba wawili ananisupport na yeye ameambiwa haitaji kuvuruga mlo wake zaidi yakuongeza) so kidizaini kama wote tutakuwa tunadeal na kubuild our bodies huku tukiwa fit and health(Subirini soon mtaona ma six pack na maNick Minaji shape ha!ha!ha! joke)

 Twende kazi sasa wale wa team health, sijui fit mnipokee mwenzenu mweeee na nyie wenzangu na mimi mnaovihurumia vinyama vyenu Wandugu mpango nikuwa na afya na kuwa fit ILA ningekushauri kuwaona watalaam wenyewe maana kama mimi nimeambiwa kukimbia ni Big no!! maana sina calories zaku burn nakuongeza kiwango cha mlo kitu ambacho kama nisingewaona watalaam nisingefanya.

 Ahsante kwa woote walionishawishi maana duu kila kona kwenye mablog,insta,facebook,tweet yaani habaree ni teamfitness,teamhealth,............ nilikuwa naskip tuu nahisi hainihusu... Kwi! kwi! kwi!


8 comments:

  1. Mama wawili yaani umenifurahisha sana wengine tunaomba kupungua wewe unataka kuongeza!!! Anyways..mie bwana nilikuwa na kg 56 baada ya kupata watoto nimeongezeka sana yaani nina kg 70!!!!! yaani nafanya mazoezi vibaya mno ndo kwanza napata misuli mikubwa mapaja yanakuwa kama ya Serena Williams..nadhani nakosea somewhere....nakimbia, na kutembea 45 minutes...nakula diets ya mboga mboga na no RED meat....

    ReplyDelete
  2. Mazoezi yanahitaji moyo kweli nilijaribu pia nikashindwa! Anonymous umenichekesha kweli misuli inakaza kama Serena inabidi uwaone wataalam

    ReplyDelete
  3. WOW WOW WOW HAPO SASA UMENIGUSA MAMA WAWILI TUKO WENGI TUNAHITAJI VIKILO VYA ZIADA NAOMBA TUSHEE WOTE MPANGILIO WA CHAKULA MAMA KILA UTAKACHOKULA

    ReplyDelete
  4. Best ni kukamua kwa kwenda mbele vitumbua ,mayai, mchemsho,maandazi,sambusa,wali,ugali,ndizi,pilau,........ milo mikuu mitatu ya uhakika na between mlo uwe na snack kama cheese & biscute,nuts,fruits. hiyo ndio adhabu yetu ambayo utajikuta unakula mara 5-6 kwa siku. Usipende kula take away zitakufanya vikilo vijae tumbo na kukufanya hata kale kajishepu ulikokuwa nako kapotee Ha!ha!ha!ha! Haya twende kazi

    ReplyDelete
  5. Mama R ushindweeeeeeee!!! ndo nini kutukatisha tamaa wenzio lakini????? Ulishindwa wewe mi mpaka kieleweke TUNAYAWEZA YOTE KATIKA YEYE ATUTIAYE NGUVU........... Ila ndo jana tuu nimeenda leo mwili wooote hauna nguvu nalalamika hadi kuvaa kiatu ha!ha!ha!ha!

    ReplyDelete
  6. Mdau hapo juu mbavu zangu bwana eti mapaja kama ya Serena Ha!ha!ha! duu nilimuuliza jana trainer wangu sitaki kuwa hivyo aisee akasema watu kama hao they go harder na mara nyingi watu wanene wakianza mazoezi huwa wanaanza na mazoezi yakutengeneza mwili kabla yakufanya mazoezi kama yakukimbia na kutembea huku wakifanya helth diet. then wakishafika mwili wanaoutaka ndo wanaanza kuumaintain kwakufanya hayo mazoezi yakutengeneza mwili that way haitakufanya uwe kiserena...........................am not sure though nimeambiwa.

    ReplyDelete
  7. Mdau hapo mbavu zangu bwana duu...... nimeambiwa watu km hao they go harder yaani anataka kupungua nakutengeza body @the same time. wanasema ukiwa mnene fanya mazoezi yakukimbia na kutembea huku ukifanya Diet then ukishafika kwenye kilo unazotaka ndo unaanza kumaitain kwa kufanya hayo mazoezi yakutengeneza mwili.............NIMEAMBIWA JAMANI SINA UHAKIKA!!!!

    ReplyDelete
  8. UPDATE: wadauzi i'm so happy in three weeks KG 6 down!!!! Mapaja ya Serena ninayafanyia kazi....

    ReplyDelete