Pages

Ads 468x60px

Monday, November 24, 2014

MDAU..................


 Leo nimefurahishwaje sasa na mdau wangu???? Duu!!! Mnamkumbuka yule mshindi wetu tuliamua tujichange change tupate stationary??? Nguvu haikuwa sana Shukrani  kwa wale mliojitokeza lakini baadae mambo yakawa sio nakushindwa kutimiza ahadi zenu....... Sio nyinyi tuu Hata mimi mahesabu yangu hayakupangika sana kuelekea hiyo project. lakini kikubwa wengi wetu tulionyesha nia,Ninachoweza sema ile nia ulionyesha ilitengeneza kitu katika ulimwengu wa roho. Kile kidogo nilichomtumia kwa kweli amenifanya nitoe machozi kwa jinsi alivyojiongeza kiakili  na hizo breakdown alizozifanya. Amenitia moyo mnooo!!! Ndugu zangu hatuhitaji mamilion ili tufikishe ndoto zetu  amini usiamini senti tano inaweza kuileta ndoto yako kwenye uhalisia ni vile wewe unavyoichukulia hiyo senti tano...........

Mpaka sasa anachohitaji ni kodi tuu....... Ila kanimalizaje sasa kajipanga weeeee huku akiliweka moyoni mama wawili kati ya ahadi yake alipa nusu  kwa hiyo ile nusu yake ndo italipa rent duu!!! mi sinilijua nimesha samehewa??? Ha!ha!ha!ha! Nimeanzaje sasa kujieleza??/ Ndugu yangu nivumilie kidogo hutu tumiezi tugumu mwenzio ukigeuka huku siku kuu, huku ada,huku mgonjwa ,huku.........chezea kudaiwa wewe??? 

Hii pia nikuwakumbusha na wale mlio ahidi mkasajisahaulisha kama mimi hapa leo ndio nimekumbuka heee kumbe na deni??? lakini km mambo bado hayajakaa vizuri usijari............ Mungu akakukumbuke kwa ajili ya nia uliyoweka.Ubarikiwe

 Haya mimi hapa mnionage........
Sura ya kikazi simmeona na vazi lenyewe la leo simmeliona????
Mama yao

Nawapenda......

2 comments:

  1. kikazi lakini umetokelezea! ulisema unataka kubadili mwonekano wa nywele kidogo kama ndivyo badili kama kwenye post yako ya AFRICAN ATTIRE ulipendeza sana.

    ReplyDelete
  2. Funguka zaidi mama wawili kuhusu huyo ndugu yetu. Mpaka sasa kipi kafanya na kile kidogo alichopata?

    Umesema ulitamani kulia jinsi alivyo jiongeza, nasi twatamani kujia kivipi?

    Inaweza kua somo kwa baadhi lakini pia inaweza kua chachu ya kumalizia ahadi zetu.

    ReplyDelete