Pages

Ads 468x60px

Friday, May 16, 2014

IT'S FRIDAY.........YEAH!!!!!!!!!


Sikia nikwambie,Jaribu lolote linalotokea kwenye  maisha yako, chunguza  kwa nini limetokea... ukijua  sababu ni wewe mwenyewe  hebu chukua hatua yakutubu, na kurekebisha... unajua nini mimi naamini sana ule msemo wa majibu hapa hapa dunia nikiingia kaburini huko ndo kuna hukumu ya wapi nastahili kwenda. so kuna vitu kwenye maisha yangu jamani huwa vinanitokea and i feel the pain mwisho wa siku nakumbushwa ,unakumbuka ulimsababishia someone pain kama hii???sasa ni wakati wako............unajua nini nimejifunza kukubali wakati kama huu maana ndio wakati pekee ambao huwa naamini  ni wakati wakujitathimini  kwamba mimi ni mtu wa aina gani, wapi maneno na matendo yangu huwa hayana kibari japo huwa najiona niko sawa,huu ni wakati ambao kiwango changu chakupondeka kinakuwa maana nimetambua na niko tayari kurekebishwa,na pia ni mda ambao huwa unanipandisha kiwango cha kiroho maana huwa najitahidi sana kuutafuta uso wa Bwana ili nijue natokaje sasa maana kuharibu ndo nisha haribu(KUBAKI NJIA KUU NO MCHEPUKO).................mwisho wa siku najua MUNGU ni mzazi wangu anayeniadhibu na kunirudia( wasomaji wa neno mnanielewa hapa)

 lakini,

unapojichunguza ukaona kabisa hilo jaribu limekuja kwa mlango ambao hauonekani ( bila kulazimisha haki).Akili yako imefika mwisho huelewi  Mungu akupe hekima hapa jinsi yakusogea mbele zake kwa habari ya hilo maana,( Angalia usije kuwa kama mfarisayo aliyejigamba.........Luka 18 soma yote tuu kuna mengi yakujifunza hapo)  Vinginevyo mpendwa chill out....... Bwana yuko kazini...... kupaniki kwako,huzuni zako, lawama zako,manung'uniko yako,stress zako HAZIBADILISHI MPANGO WA MUNGU .......  ni kweli imeandikwa Bwana atafuta chozi lako (jiulize chozi la manung'uniko, chozi lisilo na imani hata kidogo?.........) Bwana anataka uelewe ameruhusu kwa sababu, na yeye ndie akupae neema yakulishinda kwa  maana, Bwana ameandaa MKATE MBELE yako.

 NIKIKWAMBIA UJUE NIMEPITIA NA NINASHUHUDA JUU YA HILI yaani ni  NO LONGO LONGO wapendwa. kama hapa nina liushuda hilooooooooo ila kulisema nasubiri Mungu aniruhusu nikushirikishe.

Otherwise mimi nawapenda mnoooo aiseee dont forget IT FRIDAY YEAH!!!!!!!!!!!................
Jamani fashion ya kucha nimeona inipite mpaka vacation or long weekend, nature ya kazi yangu imegoma kabisa...... nimejikuta siku za jumatatu  nateseka sana kubandua na mara nyingine najifanya Boss lady ofisini uzalendo unanishinda (najikuta na act kwa sababu ya kucha lol) nikitoka nje nikaona mzigo unaotakiwa upigwe duu!!!! gafla uzalendo unanishinda hahahaaaaa!! yaani hapo hata nikikosa kiwembe ntang'ata kucha mpaka nishike jembe.................(mtoto wa mkulima ni mkulima tuu hata  aingie mjini atalima bustani).
be you
sijui napenda rangi gani za nguo ila nikiwa nimetupia black huwa najipenda zaidi.
mapozi mengine hata sijui nayatoga wapi????

mubarikiweeeeeeeeeee mpaka mchanganyikiweeeeeeeee

4 comments: