Pages

Ads 468x60px

Monday, December 16, 2013

NAFUNGUKA!!!!

Wandugu nimepita pita huko vijiweni naona kama tunajazana ujinga kiaina sina uhakika lakini ni maono yangu tuuu................Wanasema mwanamke  kujiamini mwanaume asikubabaishe hata kidogo tena kama unakazi yako na unajeuri yakulea mwanako/wanao  MBONA watatukoma!!!! Binafsi naona huu ni umaskini wa kufikiri uliojawa na ubinafsi............ UPENDO kwetu umeondoka kwa kiburi na jeuri  tumesahau nini maana kamili ya ubavu wa mwenzio ,Tumesahau kiapo tulichoapa  akili zetu zimekaa kuwaza baya litokee all the time na zaidi tunafikiri tunawapenda hawa viumbe wa viuno vyetu asikwambie mtu nenda kamuulize yoyote aliye lelewa na single parent, au muulize mzazi anayelea mtoto bila mzazi mwenzie kama mkweli atakwambia........ wachache sana wanayomudu hayo maisha na mwisho wa siku wanaishia kuwa  wazinzi( nini kwani hao ni wanadam aisee......... na mbaya zaidi walishawahi kuonja asali)  nenda kasome  na kuelewe neno linalotuambia tuwahurumie wajane.......... ndo utaelewa ni maana ya Baba na Mama........ asikudanganye mtu.HOFU YA MUNGU INAPOTEA watu tunafikiri tunaweza kubadilisha uhalisia TUNAJIDANGANYA



Naongea na kina sie ambao mpaka sasa hivi Tunamshukuru Mungu tunazimudu ndoa zetu.....na badala yakuendelea kumuomba Mungu atupe Hekima zaidi kwenye ndoa zetu, tumekaa mkao wakuwaza hayo.... kinachonikasirisha zaidi tunawashauri wenzetu wafanye hayo....... ni kweli wanapitia lakini kuna namna fulani ya hekima inayotupasa kuifanya na sio kumpa jeuri na kiburi kuharibu zaidi............................Pamoja na kuwa ndoa zetu zina amani na upendo lakini bado kuna vi ups and down vingi tuu  ambavyo hatuvileti kwenye mitandao   na unavimudu....... yawezekana huyu mtu alivyolileta kwako ameshindwa kulifikisha sawa sawa na wewe ukalichukulia kubwa kumbe ni zaidi ya lile ulilolizoea......... ni jinsi tu yakulichulia na unavyofikishiwa.

kwa kuongea hivi naelewa kuna watu wanapitia....... ni bora kunyamaza nakumuombea huyo mtu kuliko kushinikiza afanye uhalifu zaidi ya hilo analopitia...... na katu usifananishe ndoa yako na mwenzio. Huyo ni mtu na ubavu wake kama tungekuwa wamoja  basi kusingekuwa  na tofauti kwetu.

MSINIPIGE MAWE HAYO NI MAWAZO YA MAMA WAWILI  NA YALE YALIKUWA YENU  HIVYO NIJUKUMU LA MLENGWA KUELEWA NINI AFANYE.

MUHUBIRI 7

5Afadhali kusikia karipio la mtu mwenye
hekima,
kuliko kusikiliza wimbo wa wapumbavu.
6Kama ilivyo kuvunjika kwa miiba chini ya
sufuria,
ndivyo kilivyo kicheko cha wapumbavu.
Hili nalo pia ni ubatili.
7Dhuluma humfanya mtu mwenye hekima
mpumbavu,
rushwa huuharibu moyo.
8Mwisho wa jambo ni bora kuliko mwanzo
wake,
uvumilivu ni bora kuliko kiburi.
9Usiwe mwepesi kukasirika rohoni mwako,
kwa kuwa hasira hukaa kifuani mwa
wapumbavu.
10Usisema, ‘‘Kwa nini siku za kale zilikuwa bora
kuliko siku hizi?’’
Kwa maana si hekima kuuliza maswali kama
hayo.

11Hekima, kama ulivyo urithi, ni kitu chema
na huwafaidia wale walionao jua................


kwa pamoja na umoja Mungu anatupa neema yakuwafanya na furaha zaidi kuwafundisha nini maana ya upendo


maombi yangu kwa all single parents MUNGU AWAPE FARAJA YA ROHONI
na huyu ndo Christabell
Anaitwa Careen




8 comments:

  1. Rose ni kweli kabisa ulichokiandika maisha ya u single mother ni kazi kubwa ,lakini kuna wanawake wanaosuffer sana siku hizi kwenye ndoa na wengine mpaka wameletewa magonjwa na kuhuliwa kabisa ndani ya hizi ndoa kwa sababu ya kuogopa usingle mother.

    ReplyDelete
  2. Wanasema "" kitanda usichokilalia huwezi kujua kunguni wake""
    wewe mshukuru Mungu kwa mume aliekupa. Mambo ya ndoa ni MAGUMU mno, mimi sasa hivi nimeachana na mume wangu, mambo niliyopitia ni mengi mno..nikikumbuka kila nikikumbuka nalia tu, nakua mpweke ila ni bora nilitoka kwenye hiyo ndoa.
    Mlio na wanaume mnaoelewana na kupendana mshukuruni sana Mungu.

    ReplyDelete
  3. we nawekwenda zako yani umeona kuolewa ndo umemaliza maisha na ulivo libaya bas umepata zari mda wote stori hizo hizo unaboa we kama umeolewa shukuru mambo ya kusema sjui single parents wewe mwenyewe ni single parent umelelewa sasa kuutwa kujisemesha ndoa wakat mume mwenyewe Serengeti boy na hakupendi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani tatizo nini mpendwa? Hata kama amelelewa na single parent inahusu nini? Hata kama mume "" serengeti boy"" inahusu nini? Umejuaje kua hapendwi? Au ni fikra zako fupi tu? Jamani tumjue Mungu na kutambua uwepo wake. Hapa duniani si mahali pa kumnenea mwenzio mabaya..Mungu yupo na anatusikia. Wengine hapa tumefiwa na wazazi wote wawili na kuachana na mume. Bora hata huyo unaemuita "" single parent "" angekuepo. Kuna wakati unajihisi dunia yote imekuacha. Ila Mungu wetu ni mwema na hafungi jicho. Kama wewe umebarikiwa yote basi usimsemee mwenzio ubaya. " likutokalo mdomoni ndio litakutia najisi sio liingialo moyoni"".

      Delete
  4. ni kweli mdau siwezi kujua kunguni wake hivyo yanipasa kukuombea MUNGU aingilie kati maana yeye ndie ajuaye kweli iliyo ndani yako kuliko kufungua mdomo wangu kukushauri kitu ambacho kinaweza kukupa nafuu kwa Muda mbeleni kikakusumbua zaidi. naamini ukifanya maamuzi mwenyewe na neema ya Mungu ikikuongoza haijalishi mimi ntayaonaje au kuyachukuliaje hilo ndo litakuwa kusudi la Mungu ndani yako.Sauti ya Mungu ni ya upole na busara hailazimishi ila inakuangalia wewe umefanya nini kwa nafasi yako, sauti za wanadamu zinamakelele mno na ni rahisi sana kuzifuata mara nyingi huwa zinajimarket mnoo kiasi kwangu hupati nafasi yakujua ubora wake ila ni kujump nakuifuata, by the time unakuja kushtuka umeshachelewa.... hilo ndilo ninalolipiga vita........... POLE NA YALIYOKUKUTA MDAU MUNGU AKUPIGANIE NA KUKUTETEA

    ReplyDelete
  5. Anonymous at 10:04pm ukiona hivyo humu ndani hakukufai nenda pande nyingine utakufa na pressure bureee maana hilo joto, kumbe unajua nimelelewa na single parent na utam wake naujua...... .... haya basi sawa serengeti wangu anakupenda wewe mwenye sura nzuri usie na hata ujasiri wakuonyesha si sura wala jina uko uvunguni. maana hujielewi nimepata zari halafu tena hanipendi mwee!!! nakupenda lakini

    ReplyDelete
  6. yaani nashangaa hata mimi, mbaya mwenzangu amependwa na a hunky of a man, kupendwa nipendwe mie, kuolewa niolewe mie, chuki ikupate weyeeee kha !!! ingekuwa watu wanaoa kwa sura hakyanani warembo na mamiss wote wangekuwa washakuwa mamrs, mke mwema mtu hupewa na BWANA

    ReplyDelete