Pages

Ads 468x60px

Wednesday, December 25, 2013

NIMEMUELEWA MNOO


hebu tusikilize kwanza kwa wale ambao hamjabahatika  kuiona hii video halafu  nisome chini mpendwa...........






Wandugu bila shaka sikuu ziliende vizuri na kama sivyo amini kuna kusudi jema lililo mbele yako........Mungu hawezi akakuacha na wala hajakusahau hiyo ni safari unayotakiwa kuipitia ili muujiza wako ukamilike. Namuelewa mnoo Charles anaposema akili imefika mwisho aisee................ lakini ninavyoamini mimi kipindi kama hicho kama bado tutang'ang'ania  kweli mpaka ushindi upatikane wewe umepanda kiwango cha imani, na kwa uelewa wangu huu mdogo kiwango cha imani kinapimwa kutokana na lile jaribu unalopitia na ukiona wewe kila kitu mteremko mmmh!! labda inawezekana!!!! lakini, tunaomba maombi yako mwenzetu maana hichi kipindi cha kufika mwisho wa akili ni noumaa........... wala usikitamani kikupate kuna watu mnanielewa hapa ........kikubwa ni ule ushindi wake   ambao ni lazima upatikane no matter what!!!!!!

Naomba nikutie moyo tuu, binafsi nimejitambua asilimia 30% ya mimi is very tough, sijui niisemaje  kwa kiswahili fasaha na 70% yangu ni very very soft aisee mpaka kuna mda najichukia............... hii nafasi inaambatana na machozi ambayo wakati mwingine yanakosa mfutaji zaidi ya Mungu pekee, yale maneno ya huruma na kunitia moyo siyapati maana nimechoka na huruma za wanadamu hivyo mara nyingi chozi langu anayeliona ni Mungu tuu,  nimwepesi sana wakufuta chozi langu  hata wakuja kwa kunyata ntamsikia nakufuta chozi langu  haraka ili asibahatike kuliona wanasema nakufa kisabuni mwee!!!  yaani hichi kipindi maumivu yake niliyonayo sidhani hata kama dawa zakutuliza maumivu huwa sinafaa aisee, huwezi kunielewa ila usiombe mpendwa we endelea kusimuliwa kama tunavyosoma habari ya Tajiri na maskini  kama mwanadamu ukisoma mwili huwa unasisimka imagine jiweke mwenyewe kwenye hiyo nafasi..... .......nnachomshukuru Mungu baada yakujua  hiyo 70% ilibidi nifanye maamuzi ya lazima  kutumia hiyo 30% ipasavyo..... nahisi imenisaidia sana imepelekea 90%  ya jamii inajua am a very tough person, kitu ambacho kimesaidi shetani anavyokuja lazima aje amekamilika akija kijinga jinga hapewi hata round ya kwanza nimeshamzika....... lakini  ukweli unabaki pale pale asilimia hiyo 70 ni kubwa kuliko nyingine hivyo kunawakati  ni lazima huwa inashinda pamoja na jitihada zangu zoote.................................AKILI YANGU HUWA INAFIKA MWSHO wandugu........ lakini nichoipendea hii asilimia  huwa inanirudisha na kujua mimi ni mwanadam,inanifundisha kuwa mnyenyekevu,inanipa muda wakutafakari na kujua namna ya kuchukulia jambo, inanikumbusha kuwa hakuna aliye mkamilifu, inanifundisha kuishi maisha yakumtegemea Mungu zaidi na kusahau kabisa peke yangu sitoweza bila neema yake, inanifundisha wakati mwingine ni lazima upondeke na ukubali ili kuruhusu mpango ulio sahihi, hapa ndo huwa nakaa hata kwenye choo changu nakujifungia mlango na kumwambia Mungu sasa ushuke tuhojiane imekwaje??? maana sielewi akili yangu imefika mwisho.........(samehe lugha yangu cha msingi unielewe)

Angalizo:  Tafadhali  dont take advantage ya watu wa dizaini hii aiseee........ maana Mungu huwa anaruhusu lakini hawaachi  YUKO UPANDE WAO... ninaujasiri na hili maana nimeona nakushuhudia.

UBARIKIWE SANA H KWAKUNITUMIA HII LINK.... sijui unapitia nini au imekuwaje ukanitumia  MUNGU ajuaye kweli yako akakutetee na kukupigania

No comments:

Post a Comment