Pages

Ads 468x60px

Thursday, December 26, 2013

THE LOOK

Wandugu kwa wale mlio bahati kumuona yule mrembo aliyebebeshwa ( wanasema punda) mimi mwenzenu nimejikuta nalia aisee mpaka nashindwa kulileta humu ndani kama topic. sasa??? hivi  urembo wote ule amekubali kuwa punda!!!!! anavyojua kujitupia sasa  hata mama wawili huwa ananifanya kumchungulia mara kwa mara ......kinachonisikitisha ni watu wangapi kwa kumuangalia wamelazimika kuwa kama yeye  na kutafuta mteremko na mwisho wa siku ndio huyo tumemuona halafu alivyopendeza sasa  na pingu yake plus gwanda la yellow duuu!!!

huwa nafikiri kwa mtu kama yeye (mrembo) $100,000 kwake ni hela ndogo, tuu sasa kumbe hapo  ni mtaji wa boss  ye atapata mshahara baada ya boss kujua faida yake aiseee!!!  naelewa kwa nini lugha zake zote zilikuwa ni mabrand karibu kila week... jamani anauchungu gani  na hiyo pesa wakati yeye anachojua kunyweshwa, kupandishwa ndege na kuingia chooni kuzitoa??? na mwisho kuteketeza maisha ya watu???? inauma aisee sana.....ukiona mtu anamfurahia mtu wa dizaini hii mmmh!!!   acha niendelee kupigika juani na hii summer inanipigaje maana kazi yangu ni 10hrs napigika hapo hapo ntakachokipa kilipe tax, super,insurence,wages yaani we acha tu mpaka nikaje kuongea lugha za brand mpaka kiwe kimeeleweka mno tena kwa mawazo, sema tuu unakuwa umekipenda unataka kujipongeza na wewe lakini ukiifikiria hiyo hela unapata na mawazo maana huko nyumbani bongo sasa!!!! lakini bado najivunia aisee ni changu,na hakimuathiri mtu zaidi yakumfaidisha, hakuna kitu ninachojivunia kama kuokoa ajira za watu wakiwemo wazawa na wasio hasa kuokoa ajira ya watanzania washio huku yaani kwa hili huwa najiona mwepesi mnoooo kwanza naringa.

leo nimekubaliana na mdau wangu kweli usililie.................... atamalizia mwenyewe
nimeanza kuyachukia mapicha gafla 

Muwe na weekend njema

1 comments:

  1. Maisha bila hekima na uvumilivu, utasahau kama dunian kuna mungu kulingana na uzur na starehe zakupta zilizo chini ya jua.tufanye kaz kwa bidii na juhudi tuwe watu wa kiasi na kulizka itasaidia sana.

    ReplyDelete