Pages

Ads 468x60px

Thursday, December 12, 2013

LABDA HATUKUELEWANA...............


 Wandugu niliposema TUJIFUNZE KUCHUKULIANA nahisi labda sikueleweka vizuri kwa baadhi yetu na mbarikiwe wote tulioenda sawa, baada yakupokea inbox nyingi kuhusiana na topic yetu ya tuzungumze iliyopita kuna kitu nimeona nikazie..........

 Dunia yetu ya sasa  hatujui tunaishi na nani, tunakula na nani, Tunamshukuru huyu Mungu aliyetuachia huyu ROHO MTAKATIFU anayetupa mafunuo ya yanayoendelea na kutupigania tusivyoweza kutambua, japo kuwa, kama tujuavyo  hakuna aliye mkamilifu na kwa sababu hiyo kuna wakati tunamzimisha huyu Roho mtakatifu  na kuwa kimwili zaidi na hapo ndipo adui anapopata nafasi yakuingia................ 

TUNAPOSEMA  TUCHUKULIANE kuna hekima ya ziada inatakiwa itumike usije ukajikuta unachukuliana na pepo.... na kazi ya pepo nikutumika (mawazo yangu). Pepo anaweza kutumika kupitia mpendwa mwenzio, ndugu, rafiki,jirani kama wasemavyo kikulacho ki nguoni mwako............ ukitaka kunielewa zaidi kamsome Abel na Kaini, nenda kakazie kidogo kwenye habari ya Yusufu iliyompelekea kuuzwa, Ili upate nyamanyama zaidi kasome habari ya Daudi na mwanae utanielewa.....................

 Naongea  kwa kutumia kajiuzoefu kadogo, ambako Mungu aliwahi kuniruhusu nipitie, ilinitesa sana, nilijikuta nakosa ujasiri  wa kila japo, naweza kusema sikuwa mimi Muda mwingi nilikuwa fake bora mradi nilihifadhi hili neno TUCHUKULIANE.  hili neno lilinifanya niwe mjinga naweza sema, nilikosa ufahamu na kuna wakati nakumbuka nilifanya maombi special  na kwa sababu ya kutokufahamu nilimpa Mungu mipaka  anijibu vile  nilivyotaka mimi.......... (mtageuka kuume au kushoto, masikio yenu yatasikia sauti nyuma yenu, ikisema, “Hii ndiyo njia, ifuateni.’’) hii sauti niliisikia lakini sikuipa nafasi... nilijisumbukia mno.

nilikumbatia watu ambao naamini  hawakutakiwa kuwa wangu kwa kipindi hicho, nililazimisha mahusiano chakushangasha kila niliposhughulikia hilo ndo niliharibu kabisa....... kuna watu mnanielewa hapa kuna kipindi unakwenda kukutana na watu unajianda hadi maneno utakayozungumza maana unaogopa usije ukajeruhi mioyo ya watu,  na kuharibu mahusiano,lakini bado baada ya siku hiyo kupita utakutana na wale watu ulio thubutu kugandisha akili yako ili kuwafurahisha,we unajichekesha mwenzio  amekununia  amelivuta hilo domo  mbona utajuata!!!!  unajiuliza kulikoni  badae  utaambiwa ulimjeruhi mtu,  utajitahidi kutafuta suluhu wapi itajirudia rudia mwisho yanakuwa km mazoea, Na hivyo wakina sie tunamalizwa na kauli zao zile YULE ANAJIFANYA MLOKOLE MNAFIKI, ANA MAMBO YAKE ANATUMIA KIVULI ( kwi! kwi! kwi!)  leo nacheka lakini kiukweli nilikuwa nalia mnoo  mbaya zaidi unaambiwa na anavyojifanya analia lia atatukoma nyie we acha tuu sehemu zingine ambazo Mungu alikupitisha ukizikumbuka unaweza kujicheka aiseee.........nilipoteza muda mwingi kwa ajili ya hili na hata muda ambao nilikuwa natakiwa kutumia na familia yangu  nilijikuta naingiza hayo ilinipata wakati mgumu mnoo, asikwambie mtu hata amani na familia yangu ilikuwa inakosekana Baba wawili nae alishachoka kunifuta machozi duuu!!!! kweli kale kapepo kalitumika aisee mpaka nilikuwa naona Mungu hana msaada kwa hili...........

Kumbe nilitakiwa niruhusu uweza wa Mungu na mamlaka  zaidi  kuomba bila kumpa mipaka Mungu.  Hadi hapo nilipojikuta nimefanya hilo. ........TUCHUKULIANE kwangu kwa sasa lazima liambatane na amani, furaha, nakutokuwa fake( uhalisia wangu)  naweza kusema hapa ndipo nilipotoka na 
BEYOU.Na hapo ndipo nilipofunguliwa kuna mambo huwa yanafanyika katika ulimwengu fulani ambao wewe hujui na vita vyake si vya kitoto ukikuta watu wamekununia bila sababu ya Msingi  ambayo hata ukijikagua utafute wapi hapakuenda sawa hupaoni ujuwe MOTO unawaka somewhere....... na wala usiulize ulize kwa nini na chanzo chake nini we mshukuru Mungu kwa ushindi maana naamini hajataka kukuonyesha maana huwezi kustahimili ( VITA TULIVYONAVYO NI VYA MUNGU) ila ukitaka kumsaidia mwisho wa siku utapitia niliyopitia mwenzio na usiombe aisee...........

Ni marufuku kuchukuliana na mtu ambaye anataka kuzima ndoto zako, mtu anakwambia haiwezekani  wakati tumeambiwa TUNAYAWEZA YOTE KATIKA YEYE ATUTIAYE NGUVU,mtu aisyeweza hata kukutia moyo,mtu anaependa kukuona huna furaha, mtu anayetaka kila siku ukalie njaa kwake asikupe mbinu yakujisaidia mwenyewe ( hakuna mteremko), mtu ambaye ukiinuliwa kidogo ye kanuna, mtu ambaye  haoni zuri kwako. yaani ye ni hasi mwanzo mwisho kwa ajili ya maisha yako no chanya hata kidogo mmmh! mpendwa hapo stuka  CHUNGUZA SAWASAWA maana na uelewa wako wa neno TUCHUKULIANE...................

Angalizo
nimeongea kama mwanadamu ......Nikikubali japo kuwa na hayo yote bado hata mimi kuna wakati nilikuwa na mapungufu ambayo yawezekana nilizidi kumpa nafasi adui akae sawasawa...... na kwa kuandika hivi sijania kukumbusha au kutibua vidonda vilivyopo au kwa namna moja ama nyingine yawezekana unaenisoma haka kapepo kalikuwa kanashughulika ndani yangu na wewe  Mpendwa take it easy. Tukubali tulitumika ili tuzisaidia roho fulani fulani zilizoandaliwa kupitia mfano wetu...........
nimekutana nayo nimeipenda nimeona niwachafulie ka hali ya hewa kidogo 

MBARIKIWE

7 comments:

  1. nakupenda bure mama wawili ubarikiwe. Yaani hivo vya kutumika acha tu wengine tumepitia tangu shule ya msingi na ma sekondari unajigonga kwa kundi la wat wanakuona hufai ukiwashinda class wanakununia .Mwacheni mungu jamani ukija inuliwa baadae wanakuogopa na kukukwepa kabisa......acha tu.

    mi nimeropoka jambo leo uko ofisini limenikosesha amani I wish ningekuwa na blogu.ivi lazima kuweka picha ?hana blogu ya maneno tu?.tuombeane.Uwiii amani ni kila kitu.

    Mama watatu

    ReplyDelete
  2. kwa mdau hapo, co lazima blogu unaweza andika hata kwenye email yako ukasave kama draft! mimi hufanya hivyo mara nyingi sana nikiwa kwenye situation kama yako!
    kwa dada rose umenikuna maana hilo jambo limenikuna hasa maisha yangu yote ya shule kama mpendwa hapo juu alivyo sema, unakaa na watu kiurafiki ila joto la jiwe unaliona, ila nilicho jifunza hasa mara nyingi unakua ni wivu tu unawasumbua au kutokujiamini ndo maana kila unachoongea lazima kibadilishwe in a negative manner,imenichukua muda sana kujifunza somo hili ila namshukuru mungu nimejitambua!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wadau mkijisikia kushare humu just inbox ntatupia kwa manufaa ya wale waliokusudia katika hilo

      Delete
    2. Wadau mkijisikia kushare humu just inbox ntatupia kwa manufaa ya wale waliokusudia katika hilo

      Delete
  3. Yani Rose umenigusa! Me blog yako nimekuwa addicted sana.
    Topic ya leo aisee actually its what im going through.
    Yani ndugu yangu kabisa ambae nategemea kuwa nae karibu kuliko yyte kwa kuwa wote tupo mbali na wazazi wetu!
    Yeye ni kukusesha raha maana we mgeni ye ana kamuda kidogo,basi anakuona ndio basi tena,useless,hufai! Wivu,majungu,habari za huku kupeleka home!
    Yani ni shida! Anajua wewe utalea watoto milele...!hana msaada! Kwake manyanyaso matupu! Unajitahidi basi uwe karibu maana hujui mtu bado,unajitahidi yani kutenda kitu hata kabla hajarudi unaangalia,wapi pasafi ama pachafu,nini kimekaa sawa nini hakipo sawa! Basi tabu tupu!
    Ukisikia kengele ya mlango roho inaruka paah! Yani kama ametoka bdo unaamani,only hapo au usiku kitandani usingizi hupati unawaza tuu! Mungu amekuacha ama anasubiri nini!
    Basi unajitahidi kujichekesha,story za kinyumbani za kuchekesha,fashion n style za hapa na pale,shows n stuff,wapi!!!! Mtu ndo kwanza kama kuna kitu umemboa yani akikuangalia hadi anapumua kwa nguvu ile ya hasira!
    Mungu huyu,ameweka mafumbo sana! Kuchukuliana bila msaada wake jamani inaelemea Rose,af msaada wake ndo ivo upo ila naona kama haufiki jamani mimi

    ReplyDelete
  4. Kwangu mimi nimejifunza kitu kikubwa sana leo kwa kweli , nimeyaona hayo , nimepitia hayo na na nashukuru mungu leo kuliona hili neno hapa litaniongezea ujasiri wa kufanya yale yanipasayo. thx Rose God bless you

    ReplyDelete
  5. Binafsi nimeguswa na hili neno,mfano ninao wa familia ya mume isiyochukulika,nilichoamua ni kuwa mimi means BE ME,

    ReplyDelete