Pages

Ads 468x60px

Friday, July 26, 2013

TUZUNGUMZE


Ninacho amini kila mwanadamu aliwahi/anayo/ amesha kuwa na maono juu ya jambo fulani linalomuhusu, nalo hili mara nyingi huwa linabeba uhalisia wa mtu husika .....lakini kwa sababu ya msongamaono wa maisha yaliyotuzunguka na kushindwa kujitambua, wengi wetu tumepoteza uhalisia nakubaki kuwa chombo kisicho namuelekeo..............

ni vigumu sana kutimiza malengo kama tutauzika uhalisia na kuwa vile mwanadam anataka uwe,kuiga au kutamani kusiko na kiasi hadi kupelekea kupoteza muelekeo wa uhalisia wako,mwanadam ni mwanadam lakini tumeletwa kwa uhalisia tofauti. kwa mfano:

  (Mwanzo 37 nakuendelea) nimejifunza mengi. namuangalia Yusufu alikuwa ni kipenzi cha Baba lakini ndugu zake walimchukia kwa kile ninachoamini uhalisia wake nanukuu ("Yusufu akamletea Baba yao habari zao mbaya basi Israeli akampenda Yusufu kuliko wanawe wote") pamoja na kwamba hakupendwa bado Yusufu mazingira hayakumbadilisha alibaki kuwa Yusufu,ukiendelea  tena tunamsoma Yusufu alivyoota ndota Yeye km Yusufu hakujua km alichoota kina uhalisia alivyosimulia ndugu zake walitambua uhalisia uliopo katika ndoto, chuki iliongezeka na kuzidi kujipalia kaa la moto........kwa wale watu wamaono hapa tutaelewana vizuri, kuna wakati unaweza ona kitu usikipe uzito,au ukaona hakiwezekani na kukipuuzia na tena iwe imetukuta hata tumekosa hekima yakulisimlia kwa jamii, mara nyingi  imetupelekea kuwa adui nakuitwa majina fulani fulani.........na mara nyingi unapoona huwa huoni njia mbadala zitakazotumika...... hivi ndivyo nnavyomtazama Yusufu kwa maana nyingine ni hii.........Aliota? ndiyo, akasimlia? ndio, cha msingi kakaa kwenye mstari (uhalisia)

naendelea zaidi kumsoma, ameota ndoto nyingine ambayo hata kipenzi chake Baba yake ilimuumiza masikio nakumkanya..... hii inaniambia uhalisia wa mtu uko ndani ya mtu, na mtu mwenyewe ndio anaweza kujibadilisha....... nnachokuja kuona ni mbinu za kutaka kumuua ambapo pia ilishindikana mmoja wa adui akageuka kuwa daraja lakumpitisha Yusufu katika safari yake(wow! nzuri hiyo) na badala yake mwingine akashauri tena auzwe wakijua wanamkomesha kumbe wanamsindikiza Yusufu kwenda kujitwalia utukufu wake...............kajisomee mwenyewe utanielewa mpendwa

NAJIULIZA??????
 hivi Yusufu asinge simulia ndoto zake kwa hofu ya wanadamu ndoto zake zingetimia (Yes! inawezekana Mungu hakosi njia,lakini ninachokiona  uhalisia wake uligeuka kuwa chuki na chuki ndio iliyotumika kuwa daraja la yeye kupitia) na hili ndilo lililopo katika dunia ya leo mara nyingi chuki inajengeka kwa sababu ya uhalisia wa mtu( kile kituu cha kipekee ulichonacho ambacho waliojenga chuki hawana na km muhusika ukisimama kwenye mstari na hekima chuki ya huwa ndio mlango wako wakutokea  wengi tunaushahidi wa hili.........na habari njema ni kwamba HAKUNA MWANADAMU AWAYE YOYOTE MWENYE UWEZO WAKUKUTOA KWENYE MSTARI zaidi ya fujo fujo tu zakukuchelewesha na kukutengenezea mazingira mazuri zaidi........

na mwisho naiona aibu ya ndugu zake walipoenda kumuinamia km ndoto ilivyosimliwa aiseeeeee!!!!!!

KAA KWENYE MSTARI,TUNZA UHALISIA WAKO,BE YOURSELF)

ANGALIZO

hekima na uhalisia viende pamoja, uhalisia pekee muda mwingine unaweza ukafanya usumbufu mwingi kwenye safari yako ambao unaweza ukajikuta unakata tamaa na mambo yafananayo........

weekend njema

No comments:

Post a Comment