Pages

Ads 468x60px

Wednesday, July 3, 2013

JE WAJUA??????


FURAHI NA WANAO FURAHI, LIA NA WANAO LIA...............

 Huu ni wakati ambao binadamu yoyote  anapitia...... kuna kitu  nimejifunza na kutambua hili neno lina maana nyingi ambayo kwa namna fulani sikuwahi kufunuliwa km ninavyoliona sasa,...........

Mara nyingi unapobarikiwa au kuinuliwa ktika eneo fulani iwe ni ndoa,kimaisha na vitu km hivyo, Mungu huwa anakusogezea pia watu ambao wako kwenye nafasi yakusugua goti, kuomba,na wengine kufanya lolote  bora mradi tu na wao wapate hicho ulichobarikiwa (tahadhari,,,, hapa nazungumza na wale tu ambao hawafanyi kwa kuiga , wanakesha ,wanaomba kwa ajili ya hiyo ndoto ambayo ni moja ya vitu ambavyo vipo ndani ya mioyo yao, wako tayari kusubiri na wanaamini muda na saa ipo, wana wivu wa kiroho na sio wa roho mtaka vitu)

Huu ni wakati wakuomba hekima yakutambua nafasi ulionayo,je unatumia kama silaha yakujeruhi mioyo ya watu, au unatumia km  ushuhuda ili hata yule anayesubiri asimame kijasiri kuamini km inawezekana????unatumia kumtia moyo na kumuinua yule aliyejikwaa au umegeukwa kuwa kisiki na utelezi wakumfanya adondoke na asiinuke tena??????? unakumbuka wakati ukisugua goti kulikuwa kuna mtu wakukutia moyo na kukuinua????? nafasi yako iko wapi sasa????na kwa yule anayengojea, kweli ni wakati mgumu mnoo ulionao lakini ni wakati wakukua kiimani, kusonga mbele,kuamini km ina wezekana, kwa maana imewezekana kwa huyo unayemuona hapo,hakukusogezea ili ujenge wivu mtaka vitu..........wala hakukusogezea ili ugeuke adui  na kusahau ule mda wako uliopoteza kwa ajili yakuomba na kusubiri .......mwisho wa siku tunaanza kuomba maombi ya manun'guniko ( maombi ya manun'guniko tunapoteza muda ni bora tusiombe!!!!! na wakati mwingine sio kila chozi ni la haki mbele za Mungu)

imeandikwa tutainuliwa kutoka kiwango kimoja kwenda kingine ............tujichunguze wandugu tukiona tupo hapo hapo hatusogei ni kweli tupo kwenye kipindi kilichoruhusiwa chakusubiri au ndio tuliinuliwa kidooogo tukainua mabega na kushindwa kurudisha utukufu kwa yeye aliyetuwezesha au wakati wakusubiri ukageuka kuwa adui na kufunga baraka zako mpaka sasa huoni pakutokea..............

habari njema ni hii, inawezekana tujikubali na kutubu na kila mtu asimame kwa nafasi yake

NI MTAZAMO TUUU WA MAMA WAWILI

2 comments:

  1. word word Rose! be blessed and stay blessed

    ReplyDelete
  2. Huwa unanibariki na kunifundisha sana na maneno yako.. zidi kubarikiwa mpendwa.

    ReplyDelete