Pages

Ads 468x60px

Tuesday, July 16, 2013

MWANADAMU MWANADAMU MWANADAMU!!!!!!


Mwanadamu yeyote anayeweza kuongea na wewe gizani, anayekupa ujumbe fulani kwakutumia jina la kivuli,mwanadamu aliyekosa ujasiri wakujidhihirisha kwenye mwanga, nazungumza na yule mwanadamu anayekufahamu,mwanadam ambaye kama ana neno na wewe anauwezo mkubwa wakukutafuta nakukwambia, mwanadamu ambaye anakuona kwenye mwanga yawezekana kila iitwapo leo lakini hakwambii, hana uhuru na mwanga, mwanadamu ambaye hawezi kutumia silaha zake  wakati akuonapo ila ukimpa nafasi ya giza kidogo anaitumia vizuri,mwanadamu asiyekuwa na ujasiri wakukutishia ila atakutishia gizani na ngurumo nyingi zenye vishindo.......mwanadam ambaye anakuthibitishia gizani kuwa yuko kazini na anaamini utaanguka na amekaa mkao wakusubiri uanguke duuuuu!!!!!(sina jina la kumpa ila mara jingine sidhani km anastahili kuitwa mwanadam) kwa maana nyingine ni ASKARI WA GIZANI....... 

walio wagizani hawaoni yaliyomwangani,na waliomwangani hawaoni yalio gizani....... wa gizani hata ukimwashia taa kwa jinsi yakibinadamu ataona, lakini kwa sababu yeye ni wagizani atatumia nguvu kujibadilisha ndani yake aendelee kuona giza, japo kuwa neema ya mwanga imemfikia (kwa mana nyingine hana neema yakutambua yaliyo  kwenye nuru)....na alie kwenye mwanga hata giza limpitie bado ataona mwanga tuu japokuwa kuna misukosuko,milima,mabondo, na mikasa ya kila namna bado ataona hicho ni kipindi tu.........JARIBU NI KAWAIDA YA MWANADAMU..............)

ninachoweza kusema ni hivi...... acha vita vya rohoni viwe vya rohoni, kuna wakati huyu mwanadamu (PEPO) anaweza kukupush ubinadamu ukuingie kwa namna fulani  USIJARIBU!!!!! Huo ni mlango mkubwa wa yeye kuingia kwa sababu utafanya uwanadamu usaidie kazi za rohoni  NI MWIKO MKUBWA KUSAIDIA KAZI ZA ROHONI............. ACHA KAZI ZA ROHONI ZIFANYIKE KIROHONI(VITA TULIVYONAVYO SI VYA DAMU NA NYAMA BALI..........................),( VAENI SILAHA ZOTE ZA VITA ILI.............) 

 ninamengi yakuandika ila naogopa kuenenda kimwili kwenye kipengele hichi  wandugu......... JICHUNGUZE, JITAMBUE,JITATHIMINI, JE WEWE NI WA PANDE HII .......... basi kula nondo hii, mwanadamu alie umbwa kwa damu na nyama asikuumize kichwa cha msingi uwe na hekima na neema ya kujua unadeal naye vipi............. MOJA YA NONDO YETU NI HII

Zaburi 109

1  Ee Mungu wa sifa zangu, usinyamaze,
2  Kwa maana wamenifumbulia kinywa; Kinywa cha mtu asiye haki, cha hila, Wamesema nami kwa ulimi wa uongo.
3  Naam, kwa maneno ya chuki wamenizunguka, Wamepigana nami bure.
4  Badala ya upendo wangu wao hunishitaki, Ijapokuwa naliwaombea.
5  Wamenichukuza mabaya badala ya mema, Na chuki badala ya upendo wangu.
6  Uweke mtu mkorofi juu yake, Mshitaki asimame mkono wake wa kuume.
7  Katika kuhukumiwa ataonekana hana haki, Na sala yake itadhaniwa kuwa ni dhambi.
8  Siku zake na ziwe chache, Usimamizi wake na atwae mtu mwingine.
9  Wanawe na wawe yatima, Na mkewe na awe mjane.
10  Kutanga na watange wanawe na kuomba, Watafute chakula mbali na mahame yao.
11  Mdai na anase vitu vyote alivyo navyo, Wageni na wateke mapato ya kazi yake.
12  Asiwe na mtu wa kumfanyia fadhili, Wala mtu wa kuwahurumia yatima wake.
13  Wazao wake waangamizwe, Jina lao likafutwe katika kizazi cha pili.
14  Uovu wa baba zake ukumbukwe mbele za Bwana, Na dhambi ya mamaye isifutwe.
15  Ziwe mbele za Bwana daima, Aliondoe kumbukumbu lao duniani.
16  Kwa kuwa hakukumbuka kutenda fadhili, Bali alimfukuza mnyonge na mhitaji, Hata akamfisha mtu aliyevunjika moyo,
17  Naye alipenda kulaani, nako kukampata. Hakupendezwa na kubariki, kukawa mbali naye,
18  Alijivika laana kana kwamba ni vazi lake. Ikamwingilia moyoni kama maji, Na kama mafuta mifupani mwake.
19  Na iwe kwake kama vazi ajivikalo, Na kama mshipi ajifungao daima.
20  Ndiyo malipo ya washitaki wangu toka kwa Bwana, Na ya hao wanaoisingizia nafsi yangu mabaya.
21  Na Wewe, MUNGU, Bwana, unitendee kwa ajili ya jina lako, Kwa kuwa fadhili zako ni njema uniokoe.
22  Kwa maana mimi ni mnyonge na mhitaji, Na moyo wangu umejeruhi ndani yangu.
23  Ninapita kama kivuli kianzacho kutoweka, Ninapeperushwa kama nzige.
24  Magoti yangu yamedhoofu kwa kufunga, Na mwili wangu umekonda kwa kukosa mafuta.
25  Nami nalikuwa laumu kwao, Wanionapo hutikisa vichwa vyao.
26  Ee Bwana, Mungu wangu, unisaidie, Uniokoe sawasawa na fadhili zako.
27  Nao wakajue ya kuwa ndio mkono wako; Wewe, Bwana, umeyafanya hayo.
28  Wao walaani, bali Wewe utabariki, Wameondoka wao wakaaibishwa, Bali mtumishi wako atafurahi.
29  Washitaki wangu watavikwa fedheha, Watajivika aibu yao kama joho.
30  Nitamshukuru Bwana kwa kinywa changu, Naam, nitamsifu katikati ya mkutano.

31  Maana atasimama mkono wa kuume wa mhitaji Amwokoe na wanaoihukumu nafsi yake

ANGALIZO

tafadhali usiseme sala hii km hujajikagua nakuona uko kwenye nafasi yakusema sala hii japo kuwa ni kwa neema ila kwa namna fulani  km wewe ni wa pande hii neema ya Bwana itakujilia kujitambua umesimama wapi na pia huyu mwandamu yawezekana kuna namna fulani ya uanadamu uliopo ndani yako ameutumia kugeuka kuwa adui yako JITAMBUE NATENGENEZA, otherwise itatumika kuwa silaha kwetu wenyewe...........

Mbarikiwe mnooo

15 comments:

  1. Hili neno limekuja kwa wakati muafaka kwangu!! Jana baba yangu aliniambia ninyamaze niuuone ukuu wa Mungu, leo nakutana na hii Zaburi!! Ubarikiwe....

    ReplyDelete
  2. Naiogopaga hii zaburi vibaya mno da Rose, imenibidi niiruke nikimbie, hii zaburi hainaga mchezo inakata kama panga lililotoka kunolewa. Ole wake aliyeombewa hii. Mungu akubariki mama na azidi kukupigania. Nakupenda

    ReplyDelete
  3. Nadhani umesahau angalizo kuliweka mwanzo, isijewageukia watu ikawakata wao. Yes labla ya kuitumia sala hii unapaswa ujikague ukikuta upo sawa huna kosa na mtu unakaa tayari kupambana nao, Yesu wetu ni mwaminifu anatenda kwa wakati wake, alishasema hatotupa nyoka tukimuomba samaki. Nakupenda mama wawili mwenzangu

    ReplyDelete
  4. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  5. mmmh...ubarikiwe sana..Mwanadamu anatisha wakati mwingine zaidi ya shetani.. maana shetani ukitaja jina la YESU anaogopa sana. lakini baadhi ya wanadamu wanatumia jina la YESU Kujifichia dhambi zao...
    MUNgu azidi kukubariki kila iitwapo leo.

    ReplyDelete
  6. Ujumbe mzuri mnoooo mwenye masikio na asikie na mwenye macho na aone mana binadamu mmmhhhhh

    ReplyDelete
  7. Mbona comments nyingine huweki?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yawezekana nilifuta bahati mbaya Au haikuwa na upako jaribu tena ukiona sijaiachilia tena ujue wewe ni mmoja wa wale mburula wangu na sina jinsi yakukusaidia wala wadau wangu hawana msaada wa kukupa zaidi yakukupotezea

      Delete
    2. Asante kwa kuniita mburula..ila mimi binafsi sikuandika comments mbaya ila nilikua nawapa ujumbe hao wanaosemea vibaya. Mungu pekee ndo shahidi wa nilichoandika kwa nia njema.
      Again, asante kwa kuniita mburula.

      Delete
    3. Samahani kwa kukukwaza ila nisome tena utanielewa

      Delete
    4. Hamna neno mamie..usijali.

      Delete
  8. hajakuita mburula usome vizuri coment yake, amesema labda alifuta kwa bahati mbaya, na akasema ujaribu tena km hataiachia ndo ujue kuwa wewe ni mmoja wao. Watu tuwe na roho nzuri, wanawake tupendane, wivu hauna faida kama siyo wa maelendeo.

    ReplyDelete
  9. Dada Rose hii Zaburi nliisoma mara moja lakini niliiogopa sana lakini asante kwa maelezo yako nimeielewa.

    ReplyDelete
  10. its too strong for me Rose... I don't wish it to anyone unless someone has intentionally KILLED one of family members....

    ReplyDelete
  11. Hua unanifariji sana ma dia....

    ReplyDelete