Pages

Ads 468x60px

Sunday, May 31, 2015

BADO NI MBINU ZA MUOVU..................

 Unajua nini?? iko hivi, kila kitu huwa kina sababu, ni vizuri kukipa nafasi japo hata kwa sekunde kukitafakari.......... Waamini tunaamini Mungu anaweza kutumia kitu au mtu kusema na wewe...... 
Mara nyingi huwa na tofauti ya mapokeo labda kwa sababu aliyetumika ameshindwa kufikisha ujumbe au mpokeaji ameshindwa kuupokea km ulivyokusudiwa................. 
Kushindwa/kuweza kwa hawa wawili kupokea au kutoa ujumbe huwa kunatokana na mazingira au mahusiano yao.........
Ninaposema mazingira ninamaana hii, labda ujumbe ulivyokuja umekuja katika muda ambao kiakili za kibinadamu unaona kabisa sio sahihi yaani hutaki kuamini kama huo ujumbe umekusudiwa kwako.... unachotaka kuamini kwamba ni haters tuu ............. 

Sikia ni kwambie adui huwa anatumika vizuri sana kukupa ujumbe, kwa kauzoefu kangu haka kadogo niliko nako,nimegundua hana huruma yaani ,hajali maumivu ya muhusika,mara nyingi huwa anajua uhalisia uliopo ila huwa anatafuta namna yakuitosheleza akili yake ijue kile cha uhalisia sio cha ukweli maana hakifurahi kukiona, akiwa kwenye harakati za kuvuruga na kutafuta mbinu za kuvuruga hapo ndipo pia anapoanza kutumika ha!ha!ha! Mungu atamtumia kukupa ujumbe how bad adui anawish kukuvuruga...... ni namna tuu yakukumbusha endelea kuishika hiyo neema uliyonayo...............wakati huo huo adui hawezi jua km anatumika for a good reason yeye ataamini amekupata sasa ha!ha!ha!ha! si tayari amejipatia kaushahidi kakuiridhisha akili yake!!!!atahakikisha anavyokufikishia ujumbe hilo jambo limejeruhi hisia,akili,............... maana hizo ndio ndoto zake bila kujijua anatumika............  ki!ki!ki! kwani???? hujasikia, Mwizi huja ili kuharibu,kubomoa na kuiba????? unategemea nini hapo sasa???? Mpendwa SILAHA ZA KIROHO.

 ninachotaka kukutia moyo hizo bado ni mbinu na pia ni ujumbe unaokwambia usijisahau sana, pamoja na yote endelea kujivika silaha....... kuna mambo yanayoendelea nyuma ya pazia ambayo Mungu hajataka kukufunulia, Adui halali huko aliko anatafuta kila mbinu kuyavuruga hayo mazingira uliyo nayo sasa..... Mungu ameruhusu tuu usikie labda km uvumi ili usijisahau...........
1Petro 5:8 (Mwe na kiasi na kukesha,kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi,kama simba angurumaye,huzunguka zunguka akitafuta mtu ammeze)

mapicha time eti eeeh???? haya twende sasa
nani hawa eti???

wamejificha eti...........
  Mungu ndie ajuaye........... Sitasahau fadhili zake maana amekuwa mwaminifu.... wala si kwamba sisi tu hodari, au tumetenda zaidi ni Neema tuu. 

duu!! ndo utaelewa why i love high heels ha!ha!ha!



NAWAPENDA MNOOOOO

8 comments:

  1. mama wawili sisi wapendwa hatushindani kwa damu na nyama yani kuambiwa umeachwa juzi leo umekuja kuprove mpo pamoja it shows una kitabia cha kishindani kikemee dear am not a hater picha za leo ni nzuri mmependeza na chemistry ipo

    ReplyDelete
  2. Barikiwa mpendwa lakini kabla hujanisaidia maombi ya hako karoho ngoja tujipe tafakari kidogo, kwa mfano nilikuwa na kahome away ka siku chache kalikoanza siku ya tuhuma. na nikawaida sana kuwarushia mapicha wewe ni shahidi most of my family picha huwa niko nje ya home. Sasa ningeharisha kwa sababu ya kumpa ushindi huyo binadamu??? nahisi hiyo ni roho ya unyonge ......lakini nakuelewa maana siku ya tuhuma nilikuwa nakajievent ambako kila mtu alikuwa anaisubiri Camera ya mama wawili ha!ha!ha! kuna watu wananielewa hapa haya ndo mjue why sikuileta hiyo camera niliwadanganya sikusahau wala nini ki!ki!ki! haka roho ndo kalikuwa kamoto moto kakanishawishi next day nikagundua haitamsaidia muhusika.................. ngoja niendele kufanya yangu mwisho wa siku mdau simaanishi umekosea ila nilitaka utafakari yawezekana ni kweli but not kwa hili yaani km kameambatana basi ni kidogo sana maombi yake huhitaji kuyafanya special ila ni muhimu ili kasije kakakomaa.... kiroho safi nimekuelewa mno

    ReplyDelete
  3. sawa mpendwa ni ktk kujengana kama umeudhika unisamehe

    ReplyDelete
  4. Nawapenda sana Mungu awabariki

    ReplyDelete
  5. We na baba wawili mzidi kubarikiwa!!

    ReplyDelete
  6. Ha ha ha....wewe ni mfupi au shem mrefu? Najuaga wewe mrefu ujue...embu nambie urefu wako if you don't mind....mimi hapa ni cm 162 na najiona mrefu (najipaga moyo kwi kwi kwi)...

    Ila siyo siri you are the best couple...mnapendeza sana dear...

    Mama wawili mwenzio

    ReplyDelete
    Replies
    1. Niko hapo hapo kwako ila nikisimama nae bila heels najionaga kashortie fulani hahahaaa

      Delete
    2. nimesahau kusema ahsante kikikikiii

      Delete