Pages

Ads 468x60px

Sunday, May 10, 2015

HAPPY MOTHERS DAY WADAU.............

MITHALI 31

10Mke mwenye sifa nzuri, ni nani awezaye kumpata? Yeye ni wa thamani sana kuliko marijani. 11Mume wake anamwamini kikamilifu wala hakosi kitu cho chote cha thamani. 12Humtendea mumewe mema, wala si mabaya, siku zote za maisha yake. 13Huchagua sufu na kitani naye hufanya kazi kwa mikono yenye bidii. 14Yeye ni kama meli za biashara akileta chakula chake kutoka mbali. 15Yeye huamka kungali bado giza huwapa jamaa yake chakula na mafungu watumishi wake wa kike. 16Huangalia shamba na kulinunua, kutokana na mapato yake hupanda shamba la mizabibu. 17Hufanya kazi zake kwa nguvu, mikono yake ina nguvu kwa ajili ya kazi zake. 18Huona kwamba biashara yake ina faida, wala taa yake haizimiki usiku. 19Huweka mikono yake kwenye pia, navyo vidole vyake hushikilia kijiti chenye uzi. 20Huwanyoshea maskini mikono yake na kuwakunjulia wahitaji vitanga vyake. 21Theluji ishukapo, hana hofu kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake, kwa maana wote wamevikwa nguo za jotob. 22Hutengeneza mazulia ya kufunika kitanda chake, yeye huvaa kitani safi na urujuani. 23Mume wake anaheshimiwa kwenye lango la mji, aketipo miongoni mwa wazee wa nchi. 24Hutengeneza mavazi ya kitani na kuyauza, naye huwauzia wafanya biashara mishipi. 25Amevikwa nguvu na heshima, anaweza kucheka bila kuwa na hofu kwa siku zijazo. 26Huzungumza kwa hekima na mafundisho ya kuaminika yapo ulimini 

Na kwa wale single mothers wooote kumbuka Mungu anawapenda................


No comments:

Post a Comment