Pages

Ads 468x60px

Monday, September 8, 2014

SIVUMI LAKINI NIMO KWI! KWI! KWI!!!!

Haya wandugu  mwanamke kujiongeza kidogo eti  eeeh.........sawa tunapiga goti naamini kabisa bila goti Haiwezekani  we kama mbishi haya...........  haya mengine ni nyongeza tuuu.   Haya mwenzenu  ilikuwa Father's day huku kwetu kwa kweli sikuwaza kuwafanyia chochote wanangu kwa ajili ya Baba yao, walikuwa na vizawadi vyao wenyewe mashuleni huko nilikuwa nawasaidia tuu kuvificha Baba yao asivione mpaka siku ifike.......... Ukizingatia a night before tulikuwa na couple's day out mtu mzima nikajua ntampa maneno matamu huko,  basi inatosha, Na asubuhi mwanamke ntaenda kuwaamsha wanake waje wamsuprise Baba yao chumbani............ Duu!!!!  hapana chezea Mwanamke nimestuka saa kumi na mbili sio kawaida ujue???? akili hainipi, natamani kufanya zaidi na nilichopanga ( Chezea kupenda nyie!!!) na mara nyingi siku kama hizi yeye ndo huwa anatupa offer yakututengenezea Breakfast , Sikuhitaji kabisa hii offer kwa siku hii. Mwanamke nilinyata asinisikie jikoni tafuta kilichopo Mama mtu nikasababisha maandazi ya fasta, maini roast, chai tangawizi,.............. weeee!!! mtaniweza nyie??? (ha! ha! ha! ha!) kabla ya alarm yake kumuamsha Mama mtu mbio kwenda kuwamsha watoto na  zawadi zao  na mplate wangu wa haja........twendeni wanangu na wenyewe wanavyopenda masuprise  yaliyoendelea ndo hayo mjionee wenyewe...............

 meona eeh!!! bado mtu anashanga shanga usingizini....

 Haya na zawadi za shule hizo


 jamani mahanjumati yangu kama yameshasahaulika vile eti??? kweli mtu wanawe.......


Angalizo... dont try this kama  mnuno ulikuwepo ,ambao unatakiwa kumalizwa  yaani ushughulikiwe kwanza kabla ya mahanjumati yako .......aiseee usije mwagiwa chai yako ya tangawizi usoni ukajuuuutaaaa!!! Matatizo yanatatuliwa hayafunikwi,funikwi ukipenda kuyafunika mwisho wa siku lazima uwe fake kwa mwenzio.................


 Kumbuka hakuna mkamilifu ila Ahsante Mungu kwa neema yake kutulinda na kutuwezesha........

4 comments:

  1. Nice family. God bless you!

    ReplyDelete
  2. Heri ni yako mama wawili,
    Upewe hay na kuzidi

    ReplyDelete
  3. wow! ilikua furaha kweli hongera mama wawili

    ReplyDelete
  4. Shetani anatunyanyasa mno wanawake kupitia Ndoa! Ndoa nyingi mno za waaminio na wasio amini zinatikiswa na shetani tena huku kwetu afrika hali ndo mbaya zaidi coz ya mfumo dume waliokulia wanaume wetu. Kama wewe si miongoni mwao mshukuru Mungu kupita kiasi, just say Lord thank you.

    ReplyDelete