Pages

Ads 468x60px

Thursday, September 25, 2014

NIKUSHIRIKISHE...........


Wandugu mwenzenu pamoja na uchovu, huwa lazima nipitie NENO........ niko tayari kuwasahau humu ndani lakini japo dakika tano tuuu nijiongeze kwa Neno.Wapendwa wangu hebu jengeni haka kautaratibu,HUTAJUTAA............ Halafu unajua nini huhitaji kusoma kama gazeti mpango nikuelewa sio kukariri au kumaliza ukurasa. 

Tafadhali usifanye kwa sababu Mama wawili amesema..... Weka nia Muombe Mungu akupe Masikio ya rohoni yaani kuna siku unaweza ukasoma mstari mmoja tuuu na roho yako ikapona.


Leo nilikuwa na 1Wakorintho1 nilipofika hapa nimeshindwa kuvumilia nimeona niingie tuu kukushirikisha


26. Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za binadamu; wengi hawakuwa wenye nguvu au watu wa tabaka ya juu. 27 Ndiyo kusema, Mungu aliyachagua yale ambayo ulimwengu huyaona ni upumbavu, ili awaaibishe wenye hekima; na aliyachagua yale ambayo ulimwengu huyaona ni dhaifu, ili awaaibishe wenye nguvu. 28 Mungu ameyachagua yale ambayo kwa fikira za dunia ni mambo yaliyo duni na yanayodharauliwa, mambo ambayo hata hayakuwako, ili kwa hayo ayafutilie mbali yale ambayo kwa fikira za binadamu ni mambo ya maana. 29 Basi, hakuna mtu awezaye kujivunia chochote mbele ya Mungu. 30 Mungu mwenyewe ndiye aliyewaunganisha ninyi na Kristo Yesu. Mungu amemfanya Kristo awe hekima yetu; kwa njia yake sisi tunapatanishwa na Mungu, tunakuwa watu wake Mungu na kukombolewa. 31 Basi, kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Mwenye kutaka kujivuna, basi, na ajivunie kazi ya Bwana."


nawapendaaaaa!!!!

1 comments: