Pages

Ads 468x60px

Saturday, September 27, 2014

MREJESHO............

Wapendwa nilisema  ntawaambia kwa nini huu mwezi nimewachomesha mahindi sana japo, ni kawaida yangu kutokana na hali halisi ya kimaisha,  lakini kwa mwezi huu naona imekuwa too much.... Wengine mmeni inbox kutaka kujua kulikoni Mbarikiwe mnoo. 

Haya ngoja niwape mrejesho............

 Kama baadhi yenu mjuavyo maisha yangu ya siku za kazi ndo haya (pichani) ............Kwa mwezi huu ubusy umeongezeka  sana kwa sababu nimeona nifunge kaofisi kidogo kwa ajili ya Binti yenu Careen si mnajua ndo tunasherekea miaka sita???? basi kama familia tumeona tupate sababu  yakusahau mambo mengine yoooote ili tuwe na muda wa kubond zaidi kama familia.

Ninachomshukuru Mungu Biashara yangu kwa sasa haiangaiki kupata wateja......... yaani ninawateja ambao kila siku ya Mungu lazima wanipe kazi ,Ni nguvu zangu tuu mwenyewe( JINA LA BWANA LIBARIKIWE)........ Kiukweli ni mwendo wa toa gari ,Ingiza gari na  mara nyingine inanibidi nikatae kazi za wateja wa kawaida, maana nakuwa nimezidiwa mnooo ......Hasa ukizingatia huku kwetu kupata nguvu kazi ya haraka haraka ni kazi mnooo na hata ukipata sometimes unaona bora ukomae mwenyewe..........(Hapa ndo nawakumbukaga mateja wa Bongo duu!!!! ningewapaje ajira nakuwapiga neno huku nikiji Ray C foundation humo humo Kwi! kwi! kwi! Tatizo visa duuu!!!!) 

Anyway,

 ili kuiweka biashara kwenye mazingira mazuri  ya kipesa na kuwafanya wateja wangu  wasihangaike sana kwa kipindi ambacho sitakuwepo, aiseee!!! imebidi tupige double mzigo( Thanks to the team)....... yaani ni mzigo haswa leo nimekamilisha mahesabu ndo nasikia mwili hauna kazi ni choka mbaya............

Naamini kwa kipindi ambacho sipo kuna $$$ nyingi nimeziacha ziende lakini  nahitaji haka kabreak mwee!!! halafu ni vile tuu hatujui jamani....... break ni njia nyingine yakurudisha shukrani kwa Mungu kwa jinsi alivyokuwezesha .................

Nimetamani sana, hii break ningekuja Bongo mweee!!! kwa kweli nimewamiss mnoooo.......... miaka miwili na kitu sasa  mguu haujatua Bongo!!!!! tatizo moja tu....... Mungu anisaidie nipate mtu wakumwamini kumwachia Biashara yangu mweee!!!  Hii kazi inahitaji mtu mwenye moyo wa kazi sio tu kwa sababu anataka pesa yakujikimu, inahitaji mtu atakae ifanya kama biashara yake,mwaminifu, anayemthamini mteja na kujishusha ikibidi, anayeamini huduma anayoitoa leo itajitangaza yenyewe kwa kipindi kirefu, asikwambie mtu kwa wale wafanya biashara wooote kama utashindwa kumuhudumia mteja pale anapoondoka akaridhika na huduma yako, Ndugu utajaza matangazo kwenye ma Instagram, Blogs,maredio na tv mwisho wasiku utapoteza $$ na nguvu zako bure........... tena hasa huku tulipo utajutaaa!!!............ Acha mteja akutangaze mwenyewe yes, utapata ambao kwa namna moja ama nyingine hawakuridhika  huwa hawakosekani lakini, mwisho wa siku asilimia kubwa ya kile unachokitoa ndo kinajitangaza.........( Bila kusahau kuachilia upako kwi! kwi! kwi!)

Kwa kusema hivyo basi Wapendwa wangu Bongo bado ngumu mnooo!!!Lakini namwamini Mungu hili litafanikiwa tuuu.......yaani nahitaji @list mwezi.........si mnajua tena lazima twende mashambani  kina Mbeyela, kina Mwinuka, kina Sanga, Wapendwa,Mashoger,Zenji,Mwanza,Arusha is a must go, mpaka ni kwa Be you Fans duu!!! hata mwezi hautoshi..........





Haya ndo Maisha ya Mama wawili...........

NAWAPENDAAAAA!!!

1 comments:

  1. pole na kazi muke ya slay!
    ila ukija mwanza he he he he am booking for a selfie kwi kwi kwi!

    ReplyDelete