Pages

Ads 468x60px

Tuesday, February 25, 2014

NI KWELI NA AMINA

Nimekutana na huu ushuhuda  umenigusa, Nimeona niulete wandugu, Huyu ndo Mungu wa haki, hawezi akakuacha ukaangamia ........Sio kwamba tunafurahia lililomkuta adui ila tunashuhudia ukuuu wa Bwana unavyofanya kazi kwa mwenye haki, Shuhuda kama hizi zinatujenga nakututhibitishia yanayotendeka nyuma ya pazia sio kama tunavyoyafikiria bali kuna jeshi linalotusumbukia na kutuepusha na vita vya sirini...............MIMI NI NANI HATA NIKAJIVUNA ????WANDUGU TUPONDEKE KWANI TUNAISHI KWA NEEMA TUU......... siku hizi nimejifunza kuomba maombi yakutokuonyeshwa maadui zangu kwa macho aisee, Dunia ya sasa haileweki ila nipo busy kumsihi MUNGU wangu kama wapo ashughulike nao huko huko maana nimechoka  kuishi kwa hofu na kusumbua akili yangu wakati nimepewa mamlaka ya kuliamuru jeshi la mbinguni kwa ajili yangu mwenyewe............HATA IWEJE MWANADAM HAWEZI ,CHAMSINGI NI KUKAA KWENYE MSTARI..... najua kwa akili zetu hatuwezi maana ni ngumu kuwa kwenye mstari, ila kwa kumsihi yeye anayetuwezesha inawezekana!!!!!Niaminivyo mimi Mungu wetu haihitaji kitakatifu(1 yohana 1:8( Tukisema kwamba hatuna dhambi , twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu)) anachohitaji ni moyo uliopondeka na kumruhusu yeye awe muongozo wa maisha yetu basi.......,

Naitwa SAKA niko na miaka 32 na nafanya kazi
katika kampuni moja ya oil hapa mjini.
Juzi nilipewa milioni.32 mida ya jioni wakati benk
zimefungwa kwa ajili ya mkataba niliyotakiwa
kupeleka benk kwahiyo ilinibidi nichukue pesa hiyo
na kwenda nayo nyumbani bila kujua kuwa ilikuwa
ni mpango wa mkurugenzi wangu Kazini kwani
alitaka aniue na kisha kuchukua pesa hizo na
kusema nimevamiwa na majambazi na wameiba
pesa.
Usiku nikwa nimelala na mke wangu kuna kitu
kiliingia kichwani mwangu na kuamua kwenda choo.
Nilipokuwa huko nilisikia mke wangu akipiga kelele
kisha kusema jamani mume wangu.hajarudi
nyumbani siku ya leo na sijui kaenda wapi... Jamaa
wale 4 walionivamia waliendelea kumbana mke
wangu, mke wangu aliwaonyesha pesa zilipo ila
hakuthubutu kusema mimi nipo nyumbani,
kipindi hayo yote yanaendelea niliwapigia simu
polisi wakawahi kufika nyumbani kwangu na
kuizunguka nyumba yangu.
Basi jamaa wale walivyochukua pesa hizo walianza
kutoka nje na kukutana na polisi kisha zilisikia risasi
na majambazi watatu walikufa na mmoja alikamatwa
ambaye alisema ukweli ni nani aliwatuma kufanya
ivyo.
Mkurugenzi wangu alikamatwa na kuhukumia miaka
21 jela na mie nilipewa nafasi ya kuwa mkurugenzi
pale ofisini.
Fahamu aliyenilinda siku hiyo ni Mungu na ndiye
aliyenifanya na mie kuwa hapa nilipo. Amini kwa jina
lake yeye mabaya yote uliyopangiwa na wanadamu
wa dunia hii yawarudie wenyewe na ww uzidi kuwa
juu na wao wazidi kuumbuka 


AMINA

1 comments:

  1. kumbe ulikuwa hujaiona hii mtumishi ningejua ningekutumia ni ya mwezi jana

    ReplyDelete