Pages

Ads 468x60px

Wednesday, February 12, 2014

KWA PAMOJA TUNAWEZA

Haya ndugu zangu yule mwana beyou wetu tulieamua kumuwezesha hapa ndipo alipofikia, nilifanikiwa kutuma kidogo kama maelezo yake hapo chini kiukweli hata mimi nilitaka kujua kile kidogo ambacho hakijakamilika bado kitakuwa msaada kwake??? Amina  hata nyie mtakubaliana na mimi. wito wangu kwenu wote mlioniahidi mwezi huu kwa ajili yakupanda mbegu kwa mwenzetu  kwa jinsi Mungu atakavyokujalia please tuunge mkono  ili lengo la kumuwezesha litimie.Tukimuwezesha huyu tumewezesha kizazi chake pia.Na hata kama hukuahidi lakini umeguswa kwa hili tafadhali tuunge mkono.

LENGO LETU TUPATE MILLION NNE TUU. 
MBARIKIWE .
(Kuna sehemu nimeweka .......... kwa sababu maalumu kulinda hisia za muhusika)
Habari yako dada natumaini umzima pamoja na familia yako.
Baada ya kupokea ile pesa nilipeleka benk ila kila nikilala nawaza nitafanya kitu gani mana bado sijatosheleza lengo lile la kufungua ofisi hivyo nilimwomba Mungu kwamba hii mbegu nimepewa inatakiwa nioteshe ikue na yapatikane mazao hivyo siyo hela ya kuhifadhi benki inatakiwa ifanye kazi.
 
Dada nimefikiria nikaamua na kwa kupitia neno mana nimekuwa muoga kuanza kitu naona kama sitaweza basi nikaweka neno NAYAWEZA YOTE KATIKA YEYE ANITIAYE NGUVU unajua dada haya mafundisho nilifundishwa kanisani....................................kichwani na wakati mwingine huwa nasoma biblia na kusikiliza redio za injili. Kupitia hilo neno nikaamua kwenda kuulizia bei za jumla za vitenge na nikafanikiwa na kushauriwa jinsi nitafanya. Sababu sijaacha kazi basi niliona vyema kuzungusha katika maofisi na marafiki ambao nina uhakika nitalipwa. Nimeanza na biashara toka juzi na nimeona mkono wa Bwana hata sijaamini. Nilitoa ile hela benk nikanunua pea 23 za vitenge vya bei tofauti tofauti kuanzia 15,000 mpaka 30,000 kwa bei ya jumla nimepiga faida nitakayopata  inaweza kununua Computer moja ikiongezewa kidogo hivyo dada mbegu nimeiotesha na kwa uweza wa Mungu kila kitu kitakuwa sawa mpaka hivi naandika nimebakiwa na pea 5 tu.
Nitafanya hivi mpaka hapo nitakapokua tayari kifedha kufungua ofisi ya stationary & secretarial service.
 
Naomba nizidi kukushukuru sana kwa wema wako na Mungu akuzidishie.
Picha nitatuma kwa whatsapp mana simu yangu haina sehemu ya kukonect na computer.
Asante sana salimia familia yako


No comments:

Post a Comment