Pages

Ads 468x60px

Friday, June 14, 2013

TUZUNGUMZE



Ni kweli Mungu  haliachi chozi la mwenye haki likamwagika bure, na ushindi wake huwa niwakishindo mnooo .... siongee kwa sababu  tu imeandikwa bali, nimeona kwa macho yangu, nimeshuhudia  na nimethibitisha...... lakini  pia chozi linaweza kumpa shetani ushindi na hatimaye   Kumkosea Mungu wako.

Hii ni kwa wale wenzangu na mimi  (emotional people)...... ni kweli hiyo hali haitokei kwa kujipanga ni kitu ambacho kipo ndani.........Hapo kale nilikuwa mtu wa kulia nakunung'unika sana hasa katika mahusiano na jamiii, nilipotaka wanadamu wanielewe nakujitahidi kuwaeleza kile wanachokifikiria juu yangu sio ndicho, na hata km kweli nimepitiwa km mwanadamu nakujigundua  nimekosea ilinipelekea kulia nikimaanisha kutubu kwa lile nililopitiwa bora mradi tu kutetea yale mahusiano tuliyonayo katika jamii na hata wao nilipoona wamenikosea niliumia sana na hata kulia bila kudhani kuwa wao walifanya kwa makusudi  na km haikuwa makusudi bado hawakujali  wala kulichukulia mzigo zaidi chozi langu lilifanyika km silaha yakunijeruhi. Hii hali ilinisumbua sana na hata nilipokuwa nikiingia kuomba kwa hilo tatizo niliishia kulia na kulalamika mbele za Mungu na kusahau  Mungu wetu   hapendi manung'uniko anataka tuitetee imani tuliyonayo na kusahau kuwa amelaaniwa mwanadamu amtegemeae mwanadam mwenzie......... kwangu mimi ile ilikuwa ni upungufu nilitaka huruma za wanadamu, nililazimisha kubadilisha watu nakusahau  MUNGU  ndie anaebadilisha, nilijitafutia hukumu  huku nikisahau vidole vitatu vinaniangalia mwenyewe, kwa kweli ilinibidi nichukue hatua ya kiroho na kimwili naashukuriwe huyu MUNGU kwakuniwezesha hili. nimejua kujitetea nakujipigania,nimejua kuishi na  yeyote na kujua mipaka ya hisia zangu, nimekuwa na furaha na amani karibu Muda wote, nimejifunza kuna wakati kuna watu  wanakuwapo kwenye safari yako kwa muda fulani lakini muda wakufika kuondoka lazima waondoke.........zaidi ya yote nimejifunza maombi ya vita nakuvaa silaha yaani ukifika muda wa kung'oa, kuharibu na kuvunja  Aisee  kashetani lazima katubu kwi! kwi! kwi! sasa ndo itokee kuna baraka fulani zimefanyika ndani yako wale walizoea kukuona unalia watageuza usemi tangu amepata hiki na kile anajisikia kweli........... ngoja nikutie moyo hao ni wanadamu hawatakosa lakuongea kikaoni  hata iweje songa mbele...........nakumbuka siku moja nilikuwa katika maongezi yakawaida nikaambiwa   nilijua na leo utalia aiseee  hakuelewa ni jinsi gani kwanza niliona ushindi mkubwa ndani yangu pili ilinithibitishia chozi langu lilikuwa ni bure hakuna aliyelijari zaidi yakufanyika burudani kwa watu fulani.

SASA BASI...........
 ndani ya wiki hiki nikiwa katika hali yakawaida tuu nikiwa pembeni ya Baba wawili wangu  akiangalia  wrestling ( mieleka) nilimwona John Cena kwa jicho la tofauti akiwa katika  nafasi nzuri ya ushindi huku akiwa amembana ipasavyo adui yake gafla mpambe akamvuruga nilimuona akilia kiume sura imeiva akaamua kuachia ushindi bora mradi amdhibiti huyu mpambe  bila kujua ile ni mbinu tuu na hatimae adui akapata ushindi japo kuwa nae mpambe cha moto alikipata.... sijui kwanini hii kitu ilinikaa sana ninachoamini kuna kitu nilikuwa nafundishwa mara kidogo kuna taarifa fulani nilikuwa naitegemea ile nimefungua email ikawa 1+1+1=3 wakati mimi nilitaka iwe 1+2=3 ukiangalia hapo maana haijabadilika ila kwa sababu yakupenda short cut au haraka nilipondeka gafla nikajikuta nadondosha chozi ambalo siku nyingi nimekuwa nikifanya  niwezalo nilizuie kwa namna fulani nilishindwa namshukuru MUNGU nilianza kujikumbusha mistari na kuona hivyo nivitisho tu vya adui cha ajabu nilipoingia chumbani kwa ajili ya maombi nilale ile hali ilinijia nilishindwa kujizuia hili chozi lilikuwa tofauti mno nilijikuta nasoma haya maandiko ( marko 15:33-47,zab 143) ndani nilikuwa naona jinsi ambavyo YESU alipolia pale msalabani akisema Mungu wangu mbona umeniacha sikwamba hakujua uweza na mamlaka aliyonayo na alijua kwamba lile ni andiko lazima litimie ila kwa sababu alikuja km mwanadam na aliuvaa ubinadamu ndio maana alisema hivyo hii ilinidhibitishia pamoja na yote km mwanadamu chozi ni sehemu ya mwili na huku nilipoendelea kusoma zaburi HUKU  machozi yakiendelea kunimwagika ndani nilikuwa naangalia ile milango ambayo Bwana aliifanya nakunipa ushindi  mkubwa mnoo na huku nikiuona ushindi unakuja kwa habari ya lile linalonitoa machozi. 

NILICHOJIFUNZA
Chozi linamaanisha unyenyekevu mbele za Mungu,ubinadamu  halisi na pia chozi linaweza kukuweka mbali na Mungu kwani unaweza kujikuta unanung'unika nakutokutafakari ukuu na uweza wa Mungu na zaidi kufanyika kuwa silaha ya maisha yako itakayokupelekea kutokuwa na amani na furaha. kwa hiyo inategemea hilo chozi unalitoaje...........

MUWE NA WEEKEND NJEMA WAPENDWA


2 comments:

  1. asante dada maneno yako yananigusa sana napitia hali ya majari sana lakini kwakuwa namwamini Mungu na kumtegemea hili jaribu ninahakika litapita na njia yangu itafunguka hakika ingekuwa sina Mungu majaribu haya ninayopitia ningekuwa kichaa lakini saa nyingine nasema Mungu amesema vita hivi sio yetu ni vyakwake basi nikikumbuka hayo nafarijika sana ubarikiwe sana dada kwa hili somo

    ReplyDelete
  2. Mmmmhhh mwanakwetu UMEZUNGUMZA..Yaani MUNGU azidi kukutumia..umenibariki sana sana...

    Nanukuu;nimejifunza kuna wakati kuna watu wanakuwapo kwenye safari yako kwa muda fulani lakini muda wakufika kuondoka lazima waondoke.

    ReplyDelete