Pages

Ads 468x60px

Monday, August 31, 2015

Ila na nyie wadau wengine  mbona mnahasira hivyo kha!!! utafikiri team naniliu??? Jamani siusiingie tuu humu???? mnanitesa mjue maana nawaoneaga huruma mpaka nalia............ kisema na wengine napenda kujiliza liza ila kiukweli nina huruma sana yaani........Halafu ninaugonjwa mmoja ambao hauna dawa mara nyingi huwa naiangalia hiyo comment kwa jicho la tofauti sio km lilivyokuja ..... mwisho wa siku nazidi kutambua ni jinsi gani hii neema niliyonayo ni garama mnooo .............. na pia nisiichukulie poa, maana the struggle is real out there........na pia huwa najisikia vibaya sana kwa sababu Muhusika sina nafasi yakuonana nae face to face  tukazungumza labda kwa namna moja ama nyingine tukasaidiana kurejesha matumaini....... chezea safari ya matumaini bila hata dawa ya maumivu???!!! ngumu sana kuyasubiri wengi wanafia njiani................

Haya minawapenda basi...... Na huruma zangu zote ila mapicha ya ze look kuyaacha nashindwa  sa sinitafunga Blog????ha!ha!ha! Sasa wale wadau wangu wa ukweli watanionaje???najitahidi mnoo kuzuia mashauzi mengine ila ze look mmh!! nilishawambia hii stage pekee naona ndo niliyoiruka utotoni  ha!ha!ha! blame my Mama hakuninunulia Camera ha!ha!ha!
ila kupendeza ndo napendeza nyela??? napemulonge!!! ndilimchepenge ha!ha!ha! only hehe land wataelewa.


userious wa mabox huwa nauleta mpaka mbele ya Camera.......





Wasumbufu hawakosekani..........






Thursday, August 27, 2015

Hii siku mwenzenu nilitoka nitokako nimefika home naambiwa  Baba watoto  yuko kwenye shed yake ndo nikaingia humo........  Basi sasa nawazo la mapicha likaja nikaanza kumvuruga tuu  kijana ha!ha!ha! 



Black haimkatai mtu eti eeh???


kununa sasa.....!

Wakuvuruga utawajua tuu hicho kifaa kinavyoshikwa sasaha!ha!ha!

hamna kitu hapo..........

huo userious hapo kushoto kwangu vepe wadau?? mmmh!! sio kwakuwekewa mapozi hayo na mkewe ha!ha!ha!

Baba kamwage huo uchafu tuje tumalize siku (happy ending) wakubwa tuu ndo wataelewa hapa!!!(mission completed)

Nawapenda

Monday, August 24, 2015


Hatujambo wapendwa??? Nyie ndo makamanda wangu..... bila shaka mpo pouas...... Eti nyie wenzangu huu mwaka hamja ushtukia?? au mimi tuu mipango mingi kha!! hivi unajua mwaka ushaisha yaani ndo tunaumalizia........... lakini unajua nini kwa Mungu miezi  labda kwake masaa au labda siku so bado inawezekana, miezi kuyoyoma isitufanye tuamini Muda hautoshi yale tuliyoyasogeza mbele za Bwana  kwa ajili ya Mwaka huu no kukata tamaa mpaka kieleweke.............. Nakitaeleweka tuu Kwani Mungu akiwa upande wetu ni nani .................. malizia mwenyewe kulingana na Muujiza wako.

Mapicha sasa

mtanyooka tuu  kasura kalivyotulia ha!ha!ha!mengine ni uumbaji tuu wa Mungu ole wako ukosoe nakupiga maombi ya upofu ki!ki!ki!ndo nishatangaza  biashara hapo............haya muingiage www.youniqueproducts.com/beyourose mkaniungishe.



Mama wawili


Nawapenda

Thursday, August 20, 2015

KITAA.........



Mishe mishe za kitaa hiyo mifunguo utajua tuu mfungua mageti ha!ha!ha!

leo na mimi nimejifanya kucheza na picha ha!ha!ha!

Mama wawili


Anawapenda mnooo......

Tuesday, August 18, 2015

TODAY'S PRAISE..................

Jamani nyiee  nyimbo za hivi msiwemnachelewa kunijuza  wa madongo kuinama mie......!!!! Huyu Dada jamani nyieeee, mwacheni Mungu aendelee kumtumia aisee duu!!! nyimbo zake huwa zinanipa radha zooote ..........ukiisha kama nimaombi nimeshafanya,nimeabudu, nimesifu yaani wimbo mmoja tuu kata kiu..................... yaani dah!!Naona nalia tuu huku nyuma ya komputa......................

Jina la Bwana libarikiwe

Yes for the rest of my life.................



Monday, August 17, 2015

MAMA WAWILI...........


Na ubora wake........ ha!ha!ha! hii misemo mnanifundisha nyie wenyewe.........

 juzi kidogo nimwambie Baba wawili ingekuwa kipindi kile anatoa mahari ndo nilikuwa mcharo hivi weee ningekomaaje na wanduguzi maana duu!! walimkomaliaje na mimi niliwakomalia live yaani niliwaambia mkiendelea kumkomalia najimuvuzisha yaani ha!ha!ha! maana ningeringa tuu ingekula kwangu.............. khaa!! maana kasura kalijaa mkorogo wa hatari, full stress, yaani  nyie acheni Bwana......ha!ha!ha! ila unajua nini na yeye alijua anachokomalia ha!ha!ha! wanasema deal deal aliona mbeleeee................ kama unafikiri mwanamke sura au urembo ndio ndoa wee endelea kusubiri ha!ha!ha! nyie nawatania bwana  your better half anatoka kwa Mungu haijalishi muonekano wako wa nje.... hii mionekano ya nje inatudanganya sana... Mama yangu kaozesha mahouse girl wake huwezi kuamini kwanza hata kutegemea lakini sasa ni wake tena wake bora...........  all in all mwamini Mungu.

kununa sasa......... +++ domo kudondoka hatariiiiiiii

Mama wawili

Wednesday, August 12, 2015

NYIE ENDELEENI KUNIPENDA TUUU...........

Jamani eeh mwenzenu nimechoka kujitetea yaani..... siku zinavyozidi  najikuta na maliza project hii naingia nyingine. Ambazo zote nahisi zinahitaji Muda wangu halafu unajua nini??? Mama wawili karibu kila kitu kinamuangalia yeye inaweza kuwa full au half.....

Nina ndoto zangu km mwanamke, nina wajibu wangu km mwanamke,Mama na rafiki....Katika vyote hivi namshukuru Mungu amenipa moyo wa Marry sio wa Martha, wasomaji biblia mnanielewa hapa au labda niseme unapofanya kitu fanya km unafanya kwa Bwana..... ha!ha!ha! watasema najifagilia haya basi, wenyewe wanasema fanya kitu yenye roho inapenda..................

Mara nyingine huwa najioni ni mtu tofauti kidogo, nimejikuta na penda vile ambavyo labda wanawake wenzangu wengi hawavipendi nawaza tuu jamani sina uhakika lakini mwee ha!ha!ha!

Leo kuna kitu fulani kimetokea na uzuri nimepata kamda kakuja kuongea humu nimeona labda tutiane moyo.ngoja nijifagilie kidogo lakini ha!ha!ha!

 Wanawake wenzangu ni hivi Mama wawili huyu anauwezo wakukaa nyumbani na kulea watoto na maisha yakaenda yaani...... Jamani eeh Baba wawili anafanya kazi mgodini....... halafu mjuege aliitwa kuja kufanya kazi  na alikotoka alikuwa si pabaya.........
Leo nimisifa tuu humu ndani ili mnielewe........... Nikimaanisha japo kuwa nimekuwa nikitumia lugha ya mabox ni namna tuu yakutaka kuelewana na wale walengwa ninaotaka kusema nao, lakini kiukweli kweli  uwezo wa kuishi nakulipa bills na haya mapicha yote mkayaona labda ninachoweza kusema sina uhakika kwenye nafasi ya maamuzi km ingekuwa hivi na haya maficho ficho ya mara kwa mara labda yangekuwa under bajeti sana.................. ninavyosema maamuzi sio yakununua soseji, nepi za watoto sijui uji wa mtoto nazungumzia maamuzi makubwa ambayo  yaani ni makubaliano tuu kulingana na unachokiona.(kuna mtu atanielewa)

Na pia pamoja na hayo masifa yote hapo, km we mgeni humu ndani  kwa miaka 6-7 niliyoishi huku ka cv kangu  kana uzoefu wa kulea wazee,na kusafisha vyoo mpaka kufika HAPA  ........ labda nitumie hayo maneno ambayo kwa wengine huwa mnaona hayasemeki mbele za watu, achilia mbali kale kadegree kangu niliko kuja nako, japo kaliwahi nifanya niingie kwa ofisi ifananayo kwa mda wa less than week ha!ha!ha! chezea wazungu weye ..........no!no!no! ulikuwa ni mpango kamili wa Mungu aisee ...japo sikuuelewa ndani ya ile week ha!ha!ha! nilijionaje sifai sasa duu!!! 

Sijamaliza misifa nasema hivi kabla sijaja mwenzenu nilikuwa ka afisa masoko kwenye ofisi fulani ya serikali na kumiliki ka  mkoko kangu mwenyewe bila kusahau boutique Sinza kwa lemi, oh no! nimesahau nilipanga nyumba nzima sinza ha!ha!ha! rafiki yangu mmoja alikuwa ananiambia Bwana we si useme unakaa kwa mtogole??? Sinza gani vituo viwili mbele kwa mtogole ha!ha!ha! Lakini unajua nini maisha yale yakuwa tosha kuitwa toto la mji ha!ha!ha! cha ajabu maisha yangu mengi yalikuwa kanisani duuu!!! nahisi bado Mungu na akiba ya yale maombi duuu!!! hamna kitu najidanganya yale maombi yalikuwa yakusafisha uchafu wooote wa kabla ya neema ya wokovu maana duu!!!Mpaka leo huwa najitia tuu moyo na andiko linalosema sitaukumbuka uovu wako wooooteee..............Haya hivi unafikiri kazi kuleta heshima mjini?? ila sema nini nilitakiwa kufanya kazi ya ziada mitandaoni kujiweka karibu na mablogger,na wale wote watakaonifanya nionekane bila kusahau mapicha kuachia kila siku ha!ha!ha

Nimesema ni masifa day right???Mmezoea kunisikia nasema ni kwa Neema ha!ha!ha! Yes ni kwa neema lakini neema haiji km hujafungua mlango ndugu zangu.Nilikuwa namsikiliza T.D J jana anasema ("Do you want it bad enough to do what it takes to get it done???" )  


Hichi kilio cha wanawake cha mitandaoni mi kuna wakati natamani kusema ila nashindwa ndo maana mkiniweka huko kwenye magroup najuaga lengo kubwa wanaoniweka labda wanataka nifunguke au niwe msaada eneo fulani, maana wengi wenu huwa mnakuwa wadau wangu humu ninaowajua lakini ,huwa inaniwia vigumu kwa maana sijui kusudi la yule muhusika kuanzisha hilo group ni nini?? limebeba watu gani?? na je ni kweli ntakachokisema kitamsaidia mtu au ndo kuharibu mpunga wa mwenye shamba??? so mtanikuta napita tuu kimya kimya japo kuwa huwa nawashwa haswa...................

 Nimekutana na mada eti watu wanabishana jukumu la nyumba ni la nani? wengine wameweza kwenda mbali nakujisifia eti Mume wangu anafanya kazi ambayo inaweza kumfanya aishi nakulea watoto wake, kwa hiyo yeye haoni sababu afanye kazi ya nini..... Kha hii akili matope??? aisee mi nilianza kuhisi ametufanya wote mamburura wenzake, nilikasirikaje??? huko nikaogopa kutia neno kwa sababu hizo niliziweka hapo juu.Kilichonimaliza ni vile comments zilizoendelea zikawa km za kusapoti fulani, nakujazana ujinga (Mawazo yangu) na pale ndipo nilipojiona labda niko tofauti km nilivyosema hapo juu sehemu km hizi ukiona nimesema kitu ujue nimeharibu maana huwa siwezi kumridhisha mtu...............

 Mi labda nifunguke kidogo namuelewa yule mwanamke mwenye watoto garama za kulipa mara nyingi huwa zinakuwa kubwa kuliko za kile utakachokipata.... au km ni tofauti basi ni ndogo mwisho wa siku wanafamilia inabidi kile kitakacholetwa ndo hicho hicho kitumike kwa bajeti. 

Nilitamani kuuliza swali lakini kwa maelezo yake niligundua huyo mwanaume mwenyewe ameajiliwa yaani.... nilitamani kuuliza miaka mingapi amefanya hiyo kazi yakuajiliwa na ni kazi gani??? ha!ha!ha!ha! umbea tuu wakati kusutwa naogopa........ Nyie sikilizeni kwa nchi zetu hizi za ulaya ukiona mtu mpaka kwenye miaka ya hamsini bado yuko chini ya bosi na kwa sifa hizo za mitandaoni kujinadi eti anamaisha mazuri mmmh!!!mkimbie huna utakachojifunza hapo zaidi ya mashauzi ya mapicha  ya kutry kuweka jina mitandaoni ha!ha!ha!ha!......am telling you (In Diamond platnum sauti ha!ha!ha!) kimbia aisee Beba jembe nenda shamba asikupotezee muda. 

Tunataka kujua leo kesho huyo anayekulea akiondoka utasimamaje, basi haya unamsaidiaje huyu anayekulea km unampenda kweli kwa nini usimsaidie mwenzio in his 40's hayuko chini ya boss..... we bwana wee kwenye 50' watu wanataka kula bata  sio kukurupushana mamaboss na basi uwe boss mwenyewe kwa sifa hizo............ nani hapendi????   eeeh nyie bwana mi ntaongea sana ila akili mukichwa na hii mitandao.............

 haya nawapenda





mbeba mabox in a serious mood......

Mpiga picha tulia watu tujipange
Kwa heri  wenzangu tulio nchi za watu mnisamehe nimeona tuwasaidie kidogo wenzetu tunawadanganya sana  hadi huruma....

Monday, August 3, 2015

ONJA (MEMORY'S BABY SHOWER)

Haya mwenzenu hii shughuli nilifanya tuu kupigiwa simu na best friend wa muhusika, alikuwa anataka kuandaa just simple dinner bby shower ila hana idea aanzaje ha!ha!ha!ha! Mama yenu sasa ninavyopenda shughuli nilitoa maelezo mpaka Bimkubwa akaona anikabidhi chungu nipike mwenyewe chezea kimbelembele weye!!! Kikubwa kilikuwa rangi maana Mama kijacho mwenyewe Diva.....yaani sikutaka kumuangusha halafu sikupenda kuweka Blue wala Pink niliona ntavuruga privacy za watukwanz aunaweza kusutwa nani kakwambia???  na ukilizwa ulizwa yanakuhusu!!! Ninavyoogopa kusutwa siku hizi na uzee huu ha!ha!ha! Kumbuka nikimbelembele tuu.........Nilivyopewa jibu Mama kijacho yupo tayari kiyellow yellow weee faster niliendeleza majeshi na haya ndo yaliyoendelea........

 Msiangaike mnaye party planner wa bureeeeee kabisa ha!ha!ha!



Ndo mtajiuliza tangu lini Soksi zikawa mapambo ki!ki!ki! yaani humo kuna games nilikuwa nimeziandaa sasa ilitakiwa zisionekane...... niliangaika kufunga na gift paper mweee nikachemka nikaona isiwe shida kwani soksi si brand new??????? Basi ndo iwe na Deco na kifichio mumo kwa mumo ha!ha!ha! Niulize na huyo niliemuomba anitengenezee keki nahisi alijua am the best baker yaani........ha!ha!ha! kumbe hata kukoroga uji wake sijui......

 She is Gorgeous aiseee 



Divas with selfie ha!ha!ha! Hang on! so who is Prego there??? Ha!ha!ha! she is blessed eti eh??? yaani, eti anytime soon baby is out kwa tumbo lipi sasa??? na belt juu ha!ha!ha! huu utani aisee i think i can i have my no.3 soon ki!ki!ki! Iga ufe wanasema!!!

The table was set........



Colours!!!!
who is better in heel????????

Happy people

 Show them how we do in Africa Sis.!!!! Yes she did in Zambian Style ha!ha!ha! Next time i will bring my Tanzanian team to beat Zim & Zambia ha!ha!ha!ha! (joke)...................


So that was my full look.......  Well as far as i know am  brown not black ha!ha!ha! blame on whoever snap this ki!ki!ki!ki!


The woman behind the Camera

kama rafiki yangu facebook na bado unahamu yakuona matukio ya hii event haya nenda kachungulie siwezi kupost zote hapa nimefanya kuwaonjesha tuu