Pages

Ads 468x60px

Saturday, March 29, 2014

THE LOOK


BELIEVE,BE YOURSELF, BE STRONG, PRESS OOOOOOOOON!!!!!!!!!!!!!YES WE CAN DO EVERYTHING THROUGH .......................................AM THE KING, AM THE PRIEST. THE AUTHORITY AND MINISTRY IS IN ME.



Mapozi na mama wawili

ngoja niwachekeshe ushamba mzigo aiseee au ze lugha mgongano???
nilifikiri nimenunua red colour ya nywele...... sikutaka iwe nyekundu sana  so nikaenda na deep red, ile kuja kuweka sasa!!!!!ngozi nyekunduuuu, nywele nyeusi kwi! kwi! kwi!
 karibu miaka miwili sasa hichi kiatu hakija valiwa nakipenda ila huwa sijui nikivalie nini!!!
nimeamua kukomaa nayo hivyo hivyo.............

 love you

Thursday, March 27, 2014

PART 2........



 Nimepokea maoni yenu wadau, kilichonifurahisha kuna kitu tumejifunza na kukumbushwa....... na hilo ndo lengo letu BEYOU. tunata uhalisia,tumechoka na maigizo, kile ambacho mimi na wewe tumekipitia na kututesa tusingependa na mwingine apitie, na lile lililo jema tunatiana moyo na kuliombea. zaidi ni kuamini hakuna kinachoshindikana!!!! nakinawezekana kwa njia halali ni muda tuu, huku ukiendelea kufanya nini likupasalo kufanya kwa nafasi yako.................TUNAYAWEZA YOTE KATIKA YEYE ATUTIAYE NGUVU. wafilipi 4:13

 tukirudi nyuma kidogo niliwahi kusema, MAISHA YAKO YA NYUMA YANAWEZA KUWA ADUI YAKO WA MAISHA YA SASA NA YAJAYO.  Hili nimeliona katika maisha yetu, Majeraha tulioumizwa utotoni,miaka ya nyuma yamekuwa kikwazo kikubwa chakukamilisha ndoto zetu.

 Hatuhitaji kujua zaidi habari ya upande wa pili unasemaje, ninachoweza kusema yawezekana mwezetu ana majeraha makubwa mpaka akaamua kuwa hivyo alivyo ila kilichoshindikana hapo ni namna yakutibu lile jeraha ambalo ni ugonjwa wetu tulio wengi (Mungu atusaidie)

Najiuliza??? Wanawake wengi kilio chetu ni kuwa na amani..... sasa inakuwaje wakati nyumba inawaka moto ( kukosa amani ndani ya nyumba,marumbano yasiyo ya lazima) tunaweza kuvumilia kwa namna yoyote ile tena mda  mwingine tunasema nitavulimia for the sake of my kids. Uliomba  yawezekana hata kufunga kurudisha amani. kama tujuavyo Mungu wetu ana namna zake za kujibu, ameona ili amani ilirudi ndani ya nyumba ni kuchukua kile kinacholeta jeuri na majigambo (miungu vitu,) nakuwarudisha kwenye mazingira ambayo wote mtakaa chini kusikilizana na kujadili.Mfano( aliposema wasio na elimu ndo wanamtafuta Mungu mimi kwa nafasi yangu hii simuhitaji) miungu vitu. hapo hakuna nafasi ya maelewano zaidi ya kiburi na jeuri...........Mungu kajibu maombi sasa, kwa macho yakibinadamu utahisi ni jeraha zaidi lakini, ukiingia kiroho kulikuwa kuna sababu na yawezekana goti  na chozi ulilomlilia Mungu ndo majibu. Baada ya hapo unaachiwa uendelee kutumika kwa nafasi yako, kuita amani  na kuruhusu utendaji  Mungu uendelea badala yake,  roho za miungu vitu amekuingia wewe sasa ( rejea " ninaishi kwa hela ya mke wangu anayolipwa na serikali lakini hiyo hela imegeuka kuwa masimango,nakukumbushwa yale yote mabaya niliyomtendea na mara nyingine ananifukuza ndani ya nyumba")   hapa ndipo story ina badilika  JE NI KWELI TUNAVUMILA KWA SABABU YA UPENDO NA WATOTO  NAKUAMINI IPO SIKU  IMANI ITARUDI ????AU KWA SABABU YA MIUNGU VITU AMBAYO HUKUWA NAYO HAPO MWANZO SASA MMEBADILISHANA JAPO NI KIDOGO ambavyo hapo mwanzo uliviabudu kwa mateso na manyanyaso na mwenzio aliviabudu kama silaha ya kukunyanyasia na kukunyima amani???( Ukiangalia hapa hii roho inahusika pande zote)

 Ni hivi wapendwa kama kile kinachotendeka ndani ya maisha yako ni mpango kamili wa Mungu nakuhakikishia MUNGU hawezi kukuacha.  usishtuke kwa kudhani maisha yako yalikuwa yanategemea  sh. 5000 leo umerudishwa kwenye sh.1000 ukadhani Mungu amekuacha!!!! mpendwa kaa kwenye mstari hiyo sh. 1000 utaishi nayo na kukupa amani kuliko ile sh.5000 ambayo ilikunyima usingizi na kukunyima amani. YEYE NI MUNGU ATUWAZIAYE YALIYO MEMA

najiuliza tena  nina sababu gani???? ile dhambi aliyoifanya mwenzangu miaka hiyo ambayo tayari mwenyewe ameshamalizana na Mungu wake na tena yawezekana pia hata kwangu aliikiri  labda kwa namna fulani nilionyesha kusamehe inakuwaje tena baada ya muda kadhaa lile donda  linachomoza??? nazungumzia kwa yule mtu aliyetenda na kuacha haendelei( yule anayeendelea hii topic haimuhusu)

 kwa mfano  miaka fulani ilyopita jamaa alifanya mchepuko fulani ( ALIGOMA KUBAKI NJIA KUU KABISA)  kwi! kwi! kwi! lakini uligundua na kutambua yawezekana kwa namna fulani na wewe ulikuwa sababu au la ( Wapendwa shetani halali aisee) na umekuja kugundua tayari mwenzio anataka kutengeneza maana amegundua mchepuko sio. KWA NINI TUNAKUWA WAGUMU WAKUSAMEHE??? KWA NINI TUNATAKA KUTENGENEZA MALIPIZO AMBAYO YANATUVURUGA NAKUTUNYIMA AMANI????? lipi bora  kwetu????? HIVI KAMA SI NEEMA YA UKOMBOZI MIMI NA WEWE TUNGEKUWA WAPI?????

Angalizo 

Mazungumzo haya ni kwa lile kosa lililopita ila linaendelea kukumbushwa na kututolea amani zaidi  kushindwa kutimiza ndoto zetu. kwa ile inayoendelea ( mfano mchepuko daily)hako kanahitaji kajitopic kengine. ..............na pia mazungumzo haya yamenia mahusiano ya mke na Mume ili kwa pamoja tukalitimize lile kusudi lililowekwa mbele yetu kwa ajili ya utukufu wa BWANA.

wakolosai 1:21
21 Hapo kwanza ninyi pia mlikuwa mbali na Mungu na mlikuwa adui zake kwa sababu ya fikira zenu na matendo yenu maovu. 22 Lakini sasa, kwa kifo cha Mwanae aliyeishi hapa duniani, Mungu amewapatanisha naye, kusudi awalete mbele yake mkiwa watakatifu, safi na bila lawama. 23 Mnapaswa, lakini kuendelea kuwa imara na thabiti katika imani hiyo, na msikubali kusukumwa mbali na tumaini lile mlilopata wakati mlipoisikia Habari Njema. Mimi Paulo nimekuwa mtumishi wa hiyo Habari Njema ambayo imekwisha hubiriwa kila kiumbe duniani.

Wednesday, March 26, 2014

THE LOOK


Nipo nipo wandugu kapart 2 ketu kanakuja...... .... Kwa leo pata muonekano wangu, nimefanya kurudia dress na vikolombwezo tofauti kwenye kajimtoko tofauti.

aiseeeeeee!!!!!!!!

Nawapenda wandugu

Monday, March 24, 2014

MAMA WAWILI

kama mjuavyo mwenzenu unyayo ukiwa mpya nakomaa nao mpaka unatubu wenyewe................. wiki tatu hizi tangu uingie  ndani mwangu kila kivazi ninachotaka kuvaa nakifikiria kivazi gani kitaenda na unyayo huu, hata kama hakuna ntalazimisha mpaka kieleweke!!!! kipya kinyemi eti???????

 naona kula zimepita kwenye mishikaki kuanzi kwa Baba wawili mpaka kwa wadau kwi! kwi! kwi!
Red & black huwa haikatai wandugu......... ni mtazamo tuuu

Muwe na week njema wandugu........

Friday, March 21, 2014

KUTOKA KWA MDAU........................



Dah,yan mama double ile story ya yule kaka inasikitisha sana,ila Mungu ana mpango nae amelileta lile kwa makusudi yake.Ila na sisi wanawake wengine tunapenda kulipiza kisasi sana,halafu mama unaposimama kwenye zamu yako kila kitu kinaenda sawa,mwanamke mwezetu alikuwa hajasimama ndio mana hata mume wake alikuwa hamuelewi,alikuwa anatumikiwa watu wawili either kwa kujua au kotokujua.Huwezi ukawa unakunywa pombe na kwena kanisani kwa wakati mmoja,hata biblia inasema mwisho wa siku tutatapikwa kwa sababu Mungu wetu ni wa utaratibu,kama ni wa moto ni moto kama wabaidi ni baridi,hapendi watu wa vuguvugu.Ndio mama amekosa ushuhuda kwa mwanaume,halafu mama wawil amini nakwambia wamama ni jeshi kubwa na mda mwingine sisi wenyewe ndio tunachangia na mwanamke ukisimama kuna uwezekano wa asilimia tisin kumbadilisha mwanaume,Mimi mume wangu alikuwa ni mlevi wa kupindukia amini nilivyosimama kwenye zamu yangu sasa si mnywaji tena ikifika j"pil wote kanisani lakini hii yote imekuja badala ya mm kujielewa,coz nilikuwa kama huyo mama ambaye mme wake amekosa ushuhuda kwake,na mwisho wa siku sisi ambaye ndio tunaosababishia wenzetu maovu tuashida Yesu akirudi mana hataangalia kama ulikuwa mtoaji,mfagia kanisa,mwimba kwaya,mhudhuriaji ibada yani ni kilio cha kusaga meno,ila ashukuriwe Mungu wetu mana anatupa nafasi ya kutubu,huyo kaka inaelekea ana majeraha sana na mke imekuwa ni tatizo,asimwangalie mke wake anafanya nini anachotakiwa kufanya ni kusimama na yeye ndo ambadilishe mke wake,samahani nimeandika maneno mengi sana kwa sababu nimeumia sana,mama wawil umenibarki sana na uvaaji wako wa tarehe 17/03/2014 kuwa hivyo hivyo tuwe na ushuhuda kwa wenzetu tuache mawazo ya kusema Mungu haangalii mavazi anaangalia moyo wa mtu,si unaona mwenzetu alivyokosa ushuhuda kwa mumewe kwa kitu kidogo tu bia,atamani uipost kule ili tupone wengi na watu nao wachangie.ila email yangu kapuni.siku njema

Thursday, March 20, 2014

MAWAZO.........


Haya wandugu miezi mitatu ndo hiyo.......... nywele zetu zimekuwa msitu, sijielewi kote nataka....... kubaki hapa nilipo zinatakiwa zipunguzwe kidogo ili zikae vizuri, kama natakurudi kwenye kamchicha basi ndo niendelee miezi mingine mitatu naamini kamchicha katakuwepo....... Ki ukweli mwezenu mafuta yakupikia yamenikubali sana tuu,siumizi kichwa kabisa sijui wenzangu tulioanza pamoja umefikia wapi??? nimepitia baadhi ya picha nashawishika kurudi enzi hizo....... mpango ni no fake nikucheza nazo tuu nywele zangu na kubadilisha rangi.

 haya sasa mchicha 

v/s







mishikaki





wapi nigande???? sijielewi



Wednesday, March 19, 2014

Tuesday, March 18, 2014

KAJISTORY..........

Haya wandugu hili nimeona nililete tujifunze kitu, binafsi huwa kuna maandiko huwa ninayasoma lakini huwa sijakutana nayo kwenye uhalisia ingawa huwa naamini yapo........... kupitia hili kuna neno nimefunguka nakuliona katika uhalisia , mtanisamehe siwezi kuliweka wazi hilo neno kwa maana, naweza kuwa natoka hukumu wakati sistahili kuhukumu au naweza kudhani nimeelewa kumbe nimejidanganya............... Kikubwa nikujifunza kitu........  kama ulitakiwa kuwa kwenye huu ujumbe utanielewa na unaweza kufunguka ni neno gani au unaweza ukawa hujaelewa kama nilivyoelewa mimi lakini na uhakika utajifunza kitu.


Angalizo
 Muhusika yuko radhi kutumika kama shuhuda ili mimi na wewe tupone. kikubwa ni mimi mwandishi kuwa na hekima yakulileta ambalo halitania kumdhalilisha.(MUNGU ANISAIDIE)

Ni hivi, nilipata maombi ya kazi kwa mtu ambaye kwa kweli nilistuka , nilitaka kujua kwa nini? maana akili yangu haikutaka kukubali kama muhusika anataka kazi yangu hasa kulingana na sifa alizonazo. nilitaka urafiki wa karibu sijui kwa nini nilikuwa nahisi kabisa kuna kitu natakiwa nijifunze kupitia yeye siku iliyoruhusiwa ikawadia na hivi ndivyo alivyoniambia....

 Nina umri wa miaka arobaini, nina watoto  wanne na mke, ni msomi ( GEOLOGIST) nina experience ya kazi ya miaka kama kumi na miwili, nimefanya kazi na kampuni nyingi na kubwa. tangu nilipomaliza shule kila nilipoweka barua yangu ya maombi sikuwahi kukataliwa ,tena nilikuwa nachagua ipi niende ipi nisiende.Nimeishi maisha yakujivunia sana na Elimu yangu sikuwahi kuwaza kama kuna siku Elimu inaweza kuwa pambo naisinipeleke popote. Sikuwahi kuwaza kama kuna kitu zaidi ya Elimu kikakufanya kuwa mtu. 

Mke wangu ni mtu ambaye huwa anajishughulisha sana na mambo yakanisa, Nisikudanganye kuna mengi yalichangia kuweka chuki ila zaidi lilikuwa ni hili sikuwahi kuamini kama Huyu Mungu ni zaidi ya Elimu yangu, nakumbuka ni mara nyingi nimewahi kumwambia Mke wangu kama huna Elimu ndio uhangaike na huyo Mungu, maisha yangu kwa sasa simuhitaji huyo maana hawezi kunipa mahitaji yangu, na maneno mengi yakejeli niliwahi kuongea, lakini siku isiyo najina,

Nakumbuka nilimtuma mke wangu akanunue bia pub ( japokuwa alikuwa kanisani lakini tulikuwa tuna kunywa wote,tunagombana kiukweli sikuwa naona ushuhuda anaoubeba wa mimi kunitoa kuamini tofauti na nilivyokuwa naamini zaidi yakuhudhulia ibada). 
Alichelewa kidogo mimi nilihisi tofauti na kwa sababu nilikuwa nimelewa kidogo niliamua kumfuata. Nilimkuta  pub na kumnasa kibao mbele za watu,  nakurushiana maneno ambayo waliona hawakupendezewa. kama ujuavyo sheria za nchi hii, mwanamke hapigwi hata kama amekosea hiyo kesi itakugeukia.

Taarifa zilifika ofisini kwangu kwa namna ambayo hata mimi sikuilewa na bila kumlaumu mtu, nilijikuta nimefukuzwa kazi kwa kosa hilo, niliondoka kwa majigambo japokuwa nipo kwenye record yakumdalilisha mwanamke nilijipa moyo kwa sababu nahitajika sana na baadhi ya makampuni bado hawata fuatilia hiyo record .niliondoka kwa kiburi nikidhani haitachuka hata mwezi ntarudi kazini.

kwa mara ya kwanza niligundua Mwanadam anahitaji zaidi  ya Elimu. kila nilipo peleka maombi nimekataliwa,hata wale waliokuwa wananihitaji nakunitoa kwenye kampuni niliyokuwa mwanzo kwa dau kubwa leo hawanitaki hata kwa dau dogo. Nimejikuta nimeuza hata magari leo natembea kwa miguu umbali ambao sikuwahi kuwaza kuna siku ntatembea, miezi kumi ya mateso najiona kama nimeishi maisha haya kwa miaka mingi sana. nakataliwa na kupewa kejeli kila ninapoingia nakutoka.  najikuta ninaishi kwa ajili ya hela ambayo mke wangu anapata serikalini  lakini hiyo hela imejaa masimango, chuki, sioni nafasi yangu kama Mume. na wakati mwingine ananiambia niondoke. kila ninapojaribu kuleta amani ndani ya nyumba nakuonyesha   upendo ninachopata ni majeraha na zaidi kukumbushwa ule uovu nilioufanya miaka mingi ya nyuma.

 Sijajua kwa nini umenikubali nikajihifadhi hapa, Kila siku nnavyoondoka hapa huwa nakutafakari sana.....najipa moyo nakuona kweli Mungu  anakupa adhabu,nakukusamehe. nahisi huu unaweza kuwa mwanzo wa milango yangu kufunguka!!!!!! ( ahsante sana Dada, umenisitiri mnooo) unajua, Huyu Mungu anachotaka ni mwanadamu kujitambua  kwamba pamoja na yote bila  neema yake wewe si kitu. kinachonishangaza ni kwamba huyu Mungu ni wa wote  uwe udhambi au sio  ila isifike mahali ukamtukana kama nilivyofanya mimi. najishangaa baada yakugundua kwamba hii yote ni kazi ya Mungu nimefikia mahali nimekubali  kuitumikia hii adhabu maana, inanistahili ila siachi kumsihi Mungu anipunguzie maumivu ya adhabu hii maana kuna wakati nashindwa kabisa nasioni mwisho wake................akifuta machozi

Pamoja na kwamba nimetambua uweza wa Mungu my sister, Bado sijapata shuhuda  ni wapi naweza nikakaa nikamwabudu huyu Mungu , maana kila ninachokiona mbele yangu kuanzia Mke wangu na wengine ni maigizo tuu!!!!!! na tena kama leo nikipewa nafasi kushauri pamoja na haya yote, siwezi kumruhusu kijana wangu au yeyote KUOA. ninachokwambia my sister,Hii adhabu ninayoitumikia   na hii ya ndoa nahisi nikifa leo ntaenda mbinguni moja kwa moja sidhani kama ntapata adhabu nyingine( Wanawake wenzangu mpo hapo?????)

TUTAENDELEA............

Angalizo yawezekana nimeongeza au nimepunguza nimejitahidi kujiweka kwenye ile nafasi kama alivyokuwa ananielezea na kuileta kwa kiswahili,hapo ndipo nilipofikia naamini ungemsikiliza mwenyewe ni zaidi ya hii aisee.

Monday, March 17, 2014

MAMA WAWILI


Wapendwa wangu kama kuna tatizo nitawajulisha  tuu, mkiona kimya ni purukushani tuu za maisha, Ahsante kwa mlio inbox kutaka kujua kulikoni.............kama mjuavyo mwaka ndo huo mikakati mingi ili kukamilisha ndoto............... sipendi kuwa sababu kwa nini ndoto haikutimia ila, naruhusu nafasi ya yeye muweza wa yote kuruhusu kama ilikuwa wakati wake. tumeshachezea nafasi sana huko ujanani hizi za uzeeni ngoja tuzitumie vizuri eti?????  
kama nilivyowahidi last week natakiwa kuandika maelezo mengi kama kawaida yangu leo tena nimebanwa mno ila kesho no longolongo...................

 halafu poleni nasikia comments zinakataa sijui tatizo nini!!! huwa linaisha then linarudi tena . mara ya mwisho nilitakiwa kubadili design ya blog na jina libadilike kidogo kitu ambacho nahisi nalipenda hilo jina wandugu lilivyosima pekee yake bila kuongeza wala kupunguza tutangalia kama kutakuwa na ulazima basi itatubidi.

hivi na nyie mkipita maduka mnyama huwa anavuruga budget kama mimi???? nahisi na tatizo na hili yaani siwezi kuondoka sijambeba iwe kiatu,au nguo labda itokee ninaye



nawapenda



Thursday, March 13, 2014

LA FAMILY


Wandugu mnisamehe bure nimetingwaje sasa!!!!  haka  ka week????Nina kastory nataka kuwapa ila katakuwa kana part 1&2 labda tunaweza jifunza kitu, ila ndo kanahitaji nitulie na hii week haijakaa sawa. Ntajaribu kesho ili iwe tafakari ya weekend ikishindikana msinipige mawe tutairusha next week.............

 leo si alhamisi ndo kunakuwaga nakujiflash back??? haya na yetu hiyo ilikuwa mafichoni.


 IN GOD WE TRUST

Tuesday, March 11, 2014

SEMA NENO..........


 Haya wapendwa tafadhali sema neno tupone. Kama tujuavyo matokeo  ya kidato cha nne  yameshatoka. na matokeo ndiyo hivyo yalivyo kuna wale walifanikiwa na wale ambao kwa kweli hawakufanya vizuri. Sijui ni mimi au wote huwa naamini kabisa mtu huwa anahitaji second chance, huwasipendi kuuliza uliza sana ilikuwaje ,  najikumbuka mwenyewe kama nisingelipewa second chance sijui ingekuwaje???  hasa kwenye haya mambo ya shule na katika level hii. Utakubaliana na mimi asilimia kubwa kwenye hii level tulivuruga mnoooo. na wengi sio kwamba  walikuwa hawana uwezo wakufanya vizuri ila huwa kunakajipepo fulani kanadanganya  wengi kwenye umri huu nakusahau nini likupasalo kufanya, tena wengi ni ule umri unakuwa hutaki kuambiwa  unataka ujifundishe mwenyewe, ni neema sana kwa kipindi hiki kupata mtu wakutokata tamaa na kukubeba kwa namna yoyote ili uwe kwenye mstari..... nimejikuta nimetokwa hadi chozi  nilivyoandika NI NEEMA..... wapendwa naongea kwa uzoefu maana nimepitia hichi kipindi.

Nakumbuka mara baada ya matokeo nilijikuta nimerudi kwenye akili zangu nakujiona kabisa nimecheza pata potea. mbaya zaidi watu walishakata tamaa hawana mahesabu na wewe sasa nikipindi cha wewe kuwabembeleza ( dont take me wrong walikuwa wana timiza wajibu wao) na mbaya zaidi kipindi wewe unabembelezwa uwezekano wakufanyiwa chochote unachotaka upo ila hutaki kufanyiwa. kipindi kinapokuja  wewe ndo unabembeleza hata uwezo hao watu hawana  ila watajitahidi watakapo ishia......... piga picha  unapambana kurudi kwenye mstari kwa mazingira kama hayo na bado hakuna anaye amini you can make it!!!

 Naibarikiwe ile siku niliyopewa hiyo second chance aisee, ama kwa hakika ilibadilisha historia ya maisha yangu!!!!!( wengi huwa hawachezei second chance labda awe hajajitambua na hata kama haikuja kama alivyotegemea bado itatia matumaini fulani) . Mimi hapa ndo huwa najiuliza  maswali  kwa yeyote ambaye kwa namna moja ama nyingine natakiwa kumpa chance ya tatu. mara nyingi huwa natumia vigezo  vya second chance kama nitumike tena au nimpotezee.

 Baada ya kujieleza sana  nakuwatia moyo ni jinsi gani mtu anahitaji second chance tusaidiane hili

 Unataka kumsaidia Binti ambaye ametoka na zero.
 unaanzia wapi,  kumbuka  ni binti ambaye unataka kumvusha hili eneo  baada ya hapo hujui kama utaendelea au sio itategemea na Mungu atakapo kujalia. na jinsi atakapoitumia hiyo second chance.

 huyu binti ni yatima mwenye ndugu kama wewe,mimi na wengineo  ambao tutasaidiana hata kimawazo, yuko tayari hata kurudia form 2 ajipe mda mzuri. 

 Swali langu kama ni shule ni shule ipi huko Tanzania itamfaa, tunaipataje?? kutokana na mazingira ikiwezekana iwe bording. na kama una idea nyingine ni ipi? chukulia kama wewe ndo mtoa msaada kwa kuzingatia vigezo hivyo.Kama kwa namna moja ama nyingine una mtu wa dizaini hii mmemsadiaje????

MBARIKIWE

Saturday, March 8, 2014

THE LOOK

Wandugu nimejikuta natamani niwe na hizi sketi kadhaa hasa kwa weather inayokuja ila ndo nazipata kwakuzibahatisha any link please zinakopatikana nahitaji kama tatu tena tofauti na nyeusi na hii hapa please...........

 it is all well with my soul , i surrender all to Almight God, the begining and the end....... kama yeye akiwa upande wako hakuna atakae zuia!!!!!

niende wapi mimi kama sio hekaluni mwa Bwana.........pata muonekano wangu wa kanisani
 eti hivi kumbe kulikuwa na women's day!!! poor me!!! labda kwa sababu kila siku kwangu ninasherekea kuitwa mwanamke... napenda majukumu yangu kama mke nakuyafurahia.Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha nakutojutia nafasi yangu........Nawapenda Wanawake wenzangu.

Beyou love yourself and enjoy role.............

MBARIKIWE

Friday, March 7, 2014

TUZUNGUMZE....


Wandugu  mwenzenu mkiona siwajibu maswali mnayoni inbox  mjue nayafikiria niyajibuje na wakati mwingine nakuwa na jibu lakini huwa wasiwasi wangu nimapokeo ya muhusika....... ngoja leo nifunguke kidogo labda ntaeleweka. nilichogundua watu tunachanganya haya mambo

Wanasema pesa ni sabuni ya roho kwangu naichukulia kama pesa ni matokeo.....  nikiwa na maana hii pesa inatafutwa na hakuna aliyefikia kiwango  akasema mimi pesa basi, na ndo maana kila kukicha watu tunazitafuta. Kuna hili neno limeandikwa PESA NA DHAHABU NI MALI YA BABA NA SISI TUWARITHI . Sijui mpendwa huwa unalichukuliaje hili??? nijuavyo mimi  ni haki yangu kama mrithi kuwa na mali lakini  kuna namna inipasayo kufanya ili kuendeleza, usishangae nikawa mrithi nikashindwa kuendeleza urithi niliopewa. Kama hunielewe kasome habari ya mwana mpotevu.......... na je unajua kiwango cha pesa kipo machoni pa muhusika??? yaani pesa haitoshelezi wapendwa. Endelea kunisoma utanielewa

Ninaposema ni matokeo ninamaanisha pesa haikupi amani ya ndoa, pesa haikupi mume, pesa haimalizi kiu. usitumie pesa, kama  kigezo cha wewe kupata Mume/mke wapendwa. kwani hujasikia mke/mume hutoka kwa Mungu?? tumia muda kuomba Mungu akupe Mume aliyekuandalia kuliko kutumia macho yako  ya damu na nyama  sana, na kumnyima Mungu nafasi asiingie kufanya nafasi yake. Kwa kusema hivi naomba niwe muwazi  sisemi kwamba mama wawili nilifunga na kuomba kuomba Mume niliyenae, kiukweli ndo yangu mimi ilikuja tuu..........ninachokumbuka siku ambayo nilijikuta nimeingia kwenye mawazo ya ndoa jioni nikampigia mjamaa simu alikuwa mbali kidogo nakumueleza jinsi hilo wazo lilivyonijia tukajikuta wote hatuoni sababu yakutolitendea haki wazo, nafikiri hapo hapo tukaanza taratibu haikuchuka miezi minne nikawa tayari ROSE WA SLAY ni NEEMA TU (kwa wale mnaongojea mnaniulizaga haya maswali nafikiri hapa mnanielewa kwa nini huwa sijibu mkiwa mnataka msaada wa dizaini hii kwa kweli sijapitia kipindi hicho, huwa muoga kushauri kitu ambacho sijakipitia na  ni muhimu sana kwa mtu) na  pamoja na hayo yote sisema ndoa yangu mimi 100% ipo poua, wandugu ndoa yangu ya kawaida sana tuu, kikubwa  ni roho zetu sio hiyo wanayosema ni sabuni ya roho,  kwetu ni matokeo. 

Nazidi kusisitiza ni kweli kuna vitu vya kuangalia kwa nafasi yako kama mwanadam, kwa mfano badala yakuangalia pesa hebu angalia uwezekano wa yeye na wewe mkiwa pamoja kutengeneza hiyo pesa.Badala yakutamani kuishi ulaya ukaamua kukimbilia mzungu au yeyote aliyetoka nje ya nchi akuoe ili akupe makaratasi hebu  mwamini Mungu kwa hiyo ndoto yako akupe yule yule Mume alikuyepangia kwa pamoja  mkakamilisha hiyo ndoto yenu..... nakuhakikishia inawezekana tena sio utaondoka Tanzania kwa sababu maisha yamekushinda bali kwa sababu ni moja ya ndoto zako (NINA USHUHUDA WA HILI) kama hunielewi nenda kamsome IBRAHIMU alivyoambiwa aende nchi ya ahadi( wandugu MUNGU wetu haongopi akisema Ndio hakuna atakaye pangua)........

Najitahidi kukutoa kwenye neno Pesa kama sabuni ya roho. Kwa macho yangu nimeshudia ndoa zakutaka makaratasi  na wameyapata,ulaya ameiona, mwisho wa siku bado hana amani  nakuona makaratasi na pesa sio ndoa.( wahusika please msinielewe vibaya lakini naona ni nafasi nzuri yakutumia mifano yenu ili tuelemishe wale waliokusudiwa) juzi kati kuna kijana alikuja kuniomba kazi  ananiambia lengo kubwa kwa sababu anataka kulipa fine alikamatwa anaendesha amelewa otherwise yu ko poua kukaa nyumbani ale hela ya serikali, mwingine anakwambia anataka kwenda holiday ndo maana anatafuta kazi, sasa unajiuliza kijana kama huyu anaenda nyumbani(Tanzania) wale wanaolilia makaratasi wakayapata kupitia huyu wakaja huku halafu inakuwaje??? si bora yule binti akabaki nyumbani anauza nyanya. Wapendwa inauma sana sisi tuliopo huku tunaelewa  na ukweli hatuwapi tunawadanganya tuu Mitandaoni.

Niliposema kiwango cha pesa kipo kwa muhusika nilimaanisha hivi, Pesa haitoshelezi hivyo ukifanya kama ndo faraja yako kuliko chochote tegemea kuwa mtu wakukosa amani kila siku nielewe kwa kajimfano haka
 nakumbuka miaka minne iliyopita ( kama mjuavyo starehe yetu kubwa nikujificha kama familia) kujificha  ilikuwa inaweza kutugharimu  sana labda $1000 hiyo siku tatu mpaka nne ,chumba $100 per night inayobaki mlo, mpaka shopping  na bado tulikuwa na amani na tulikuwa  tumerudi tumerefresh wenyewe kutoka mafichoni, namshukuru Mungu sasa hivi tunaweza kwenda mpaka $ 700 per night bado hujala, na shopping hujafanya  lakini kwa sababu pesa kwetu ni matokeo hatuoni shida siku nyingine tukarudi kwa ile hotel ya miaka iliyopita bado amani itabaki pale pale isipokuwa tumecheza na matokeo ya pesa.lakini ukiwa hapo kwenye level hiyo nakuamini kama waaminivyo wengine itatufanya tuuishi kwa kukariri majengo na kukosa amani ya kile tunachokipenda (kujificha)... utakubaliana na mimi kwa nini naamini pesa nimatokeo.......na  hapa nilipo huwa najipiga picha siku moja nimelala kwa $2000per night na familia yangu, nimekusikia tuu in two years Bwana atafanya njia ( kwi! kwi! kwi!hii sasa naleta misifa eti?? mnisamehe) wandugu kikubwa nataka watu tuelewe pesa haina kiwango haitoshi hivyo haileti amani ifanye kama matokeo iwepo au isiwepo bora mradi mahitaji muhimu yanapatikana.

KHAA NIMECHOKA KUANDIKA NINAMIFANO MINGIIII

Angalizo
Sijasema makaratasi hayatakiwi ntakuwa mnafiki mbona mimi ninayo? sijasema usiolewe kwenye mgodi unaotembea ntakuwa nina wivu kwa sababu mimi naosha magari, kikubwa hivyo ndivyo ilivyotakiwa uwe?? unaishi kwa ndoto yako au unatembelea ndoto ya mwenzio yako iko pending?? au tumekukaririsha mitandaoni na mashauzi yetu tukasahau kukusaidia ni nini likupasalo kufanya na wapi tulikosea  ili na wewe usiingie.Mwisho wasiku wewe ndo ujikague maamuzi unayotaka kufanya ni sahihi au kwa sababu ya kile unachokiona kwa macho ya damu na nyama.

Mbarikiwe

Thursday, March 6, 2014

MY WAWILI....

Mpango wakupiga picha ulianza mara tu bidada kumvua  Baba yake kofia , nikamsikia Mumy look am matching!!!!  take me a photo........... mapozi ndo hayo


 mmmh!!! watoto wanakuwa nyie nikiangalia hii picha eti miaka mitano ishapita????


 na yeye huyo

 hivi  kuweka hivyo vidole maana yake nini???mshamba mie maana nisije nikawa naruhusu kumbe kuna maana sio nzuri.... hata sijui na wenyewe wamelipata wapi hili pozi....



Ahsante  Baba wa Rehema kwa ajili ya neema hii uliyotupa.

Wednesday, March 5, 2014

KUTOKA KWA MDAU............


Tafadhari rejea post  ya tarehe 18/02/2014 (SEMA NENO) ili kuelewa huu ujumbe..... 
MBARIKIWE
Asanteni kwa ushauri wenu mmenifanya niishi tena

Nachukua nafasi hii kukushukuru wewe dada Rose na wasomaji wako wote kwa ushauri wenu aisee nimefarijika kwa kiasi na kujiona nathaminiwa na kuna watu wana matatizo makubwa ila bado wanaishi kwanini mimi nikate tamaa mapema hii. Asanteni sana niko vizuri kiasi naanza kupata nafuu na machungu moyoni yanapungua pungua na imani yangu pia inazidi kuongezeka. Unajua wapendwa unaweza kumshangaa mtu na maamuzi yake n.k ila usiombe upate tatizo maishani mwako kanisani utaenda utaongea na watu, utashauriwa ila mwisho wa siku utabaki mwenyewe mwanzoni nilikuwa vizuri sana tena nikawa najifariji. Siku zikawa zinaenda ikiwa mwaka hadi mwaka wa sita umevumilia tu pekeyako unawaza unajaribu mpaka mwisho wa siku unatafuta solutions mwenyewe kichwani ndio maana nikafika hatua ya kutafuta msaada wa zaidi ninaoupata kwa watu wangu wa karibu. Wengine mlinishangaa eti najiua ni uamuzi mgumu sana hata binafsi yaani unakuwa umepitia mengi mpaka kufikia huko umeshachoka kichwa kabisa. Binafsi nilianza taratibu kukata tamaa bila kujijua taratibu nikawa sio smart tena kama zamani kichwa kinauma sana, stress ndio usiseme, nikanenepeana hadi sitamani kujiona yaan ni mambo kibao nimepitia lakini najipa moyo kwamba na hili litapita. Imani yangu ikaanza kupungua nikawa nasikia sauti inaniambia kwanini usife tu kila mara uwezi amini nimenusurika kugongwa na gari mara nyingi nimeshanusurika kupata ajali mara nyingi. Nakumbuka siku moja nikiwa naendesha gari naenda ofisini na mawazo yangu tele ile kustuka niko darajani nimenusuka ile sauti ikanirudia tena kwanini usikanyage mafuta tu kwa spidi uingie darajani kwa spidi? nikajipa moyo nikatoka eneo hilo mpaka ofisini, Ilifika wakati nikaacha hadi kuendesha gari jamani nasimulia haya yote ili watu nimepitia wapi mpaka kufika nilipokurupuka nakusema trh 28/2 najiua. Ni stori ndefu na ya kusikitisha ila nawashukuru sana mmenifanya niishi tena na naendelea vizuri na pia naombeni maombi yenu zaidi niweze kupata hao watoto jamani 

Tuesday, March 4, 2014