Pages

Ads 468x60px

Wednesday, May 23, 2018

NGUVU YA NDOTO........


Nilichojifunza kwenye maisha kuna nguvu ya ndoto ndani ya muhusika........ wakati wengine wanaiangalia ndoto yako kwa jicho la pembeni wewe kwako huwa inajicho la kipekee....... Wakati mwingine huwa haikupi nafasi ya wewe kuielezea ili ieleweke kwa wengine maana  haitegemei uelewe wa mtu wa pembeni..... Ndoto wakati mwingine inausiri mkubwa sana lakini huwa inatoa nafasi kubwa muhusika kupenyeza, wakati mwingine mipenyo unayopitia huelewi kwa wakati huo ila kuna muda itakupa nafasi yakuelewa safari yake ni kukufikisha ndotoni.......


 Wakati mwingine unaweza ukahisi ndoto hiyo haipo tena maana ulishaikatia tamaa kinachonishangaza ni kwamba ndoto huwa haipotei usipoonyesha ushirikiano leo huwa inatengeneza mazingira ya wewe kuna na muhemko nao kwa wakati.

Ninachoweza kusema ndoto ni lazima ikamilike na mkamilishani ni muotaji ndoto japo kuna mazingira ambayo kuna watu lazima watumike katika kuikamilisha ndoto yako.Sifa yake kubwa huwa naipenda muda wa ukamilifu unapokuja utendaji wako huwa unakuwa tayari, yaani huwa kama umekaa mkao wakula hivi , huna papara kama mwanzo kitu ambacho kinakusaidia utendaji wako uwe makini na wakuzingatia nini likupasalo kufanya....



 kama hunielewi kamsome Yusufu na ndoto yake.....

 Tuendelee na mapicha

 Muotaji huwa kwenye mazingira yasiyokuwa na ushirikiano kabisa 



asiporuhusu mwiingiliano basi huwa jicho lake lakipekee juu ya ile ndoto

 wakati wengine wanaona haiwezekani yeye anatabasam kwa unyenyekevu


Nawapenda

No comments:

Post a Comment