Pages

Ads 468x60px

.

Sunday, June 10, 2018

THE LOOK

Wapenzi kuna topic nakuja nayo soon naitafutia muda ..... otherwise mapicha yako mengi tuu tuendelee kusafisha macho Ha!ha1ha!
 usiombe kuwa mpiga picha wangu ntakupa maelekezo mpaka unizilie Ha!ha!ha! wanazila sometimes....
 mnuno vepe
 Pink haimkatai mtu eti eeh!
 Mama wawili

Anawapenda

Tuesday, June 5, 2018

KITAA.........

Kujitoa akili vepe ha!ha!ha!ha!

 Kabla sijahit kitaa ngoja tuji Canon.... Miondoka lazima iendane na mikato Ha!ha!ha!
Ila ujanja wote sizunguki kitaa hivi kama Baba wawili hayuko pembeni Ha!ha!ha!

 msijali kito.... kilikuwa all covered sema kwenye mapozi ya Canon ndo nimejiachia
Nawapenda

Wednesday, May 23, 2018

NGUVU YA NDOTO........


Nilichojifunza kwenye maisha kuna nguvu ya ndoto ndani ya muhusika........ wakati wengine wanaiangalia ndoto yako kwa jicho la pembeni wewe kwako huwa inajicho la kipekee....... Wakati mwingine huwa haikupi nafasi ya wewe kuielezea ili ieleweke kwa wengine maana  haitegemei uelewe wa mtu wa pembeni..... Ndoto wakati mwingine inausiri mkubwa sana lakini huwa inatoa nafasi kubwa muhusika kupenyeza, wakati mwingine mipenyo unayopitia huelewi kwa wakati huo ila kuna muda itakupa nafasi yakuelewa safari yake ni kukufikisha ndotoni.......


 Wakati mwingine unaweza ukahisi ndoto hiyo haipo tena maana ulishaikatia tamaa kinachonishangaza ni kwamba ndoto huwa haipotei usipoonyesha ushirikiano leo huwa inatengeneza mazingira ya wewe kuna na muhemko nao kwa wakati.

Ninachoweza kusema ndoto ni lazima ikamilike na mkamilishani ni muotaji ndoto japo kuna mazingira ambayo kuna watu lazima watumike katika kuikamilisha ndoto yako.Sifa yake kubwa huwa naipenda muda wa ukamilifu unapokuja utendaji wako huwa unakuwa tayari, yaani huwa kama umekaa mkao wakula hivi , huna papara kama mwanzo kitu ambacho kinakusaidia utendaji wako uwe makini na wakuzingatia nini likupasalo kufanya.... kama hunielewi kamsome Yusufu na ndoto yake.....

 Tuendelee na mapicha

 Muotaji huwa kwenye mazingira yasiyokuwa na ushirikiano kabisa asiporuhusu mwiingiliano basi huwa jicho lake lakipekee juu ya ile ndoto

 wakati wengine wanaona haiwezekani yeye anatabasam kwa unyenyekevu


Nawapenda

Saturday, May 19, 2018

TUPOGO.......

Wapendwa nimebanwa kidogo ... Tuna ugeni wa Billy Graham ministry ambapo mjukuu wake Willy Graham amekuja kutuhudumia..... basi sasa na sie Mungu katupa kibali chakuwa macounsellor wa event basi  ndo kukimbizana tuu.... topic yetu ya Mama sijaipotezea ntaipatia muda nivumilieni.


 Baba na Mama wa...............


 Tukishughulishwa tunajuaga kushughulika  ha!ha!ha!

 ndo nini sasa Ha!ha!ha!

 Haya tunawapenda

Sunday, May 13, 2018

MOTHER'S DAY TREAT


Kuna kitu chakiubunifu hapo lazima ujifunze eti eeh! binafsi nimependa combinations za colour na tray...... naamini aliyetengeneza hii gift aliangalia sana colour combination........... anyway! nimeshamjua aliyemtengenezea na alijua wapi atakaponikamatia.... i love everything aisee.

 Kaka zangu kama mnanisoma huko please vitu kama hivi means a lot kwa mwanamke aisee....... sometimes hata havihitaji bajeti ya hivyo  yaani......... Please do kwa mawifi zangu please. na ahsante kwa kufanya i know  how much hivi vitu vidogo vidogo vinavyoleta maana kwenye maisha ya mwanamke.


 Kwenye suala la shopping yes i trust him..... kuanzia mimi, wanae na hata grocery shopping ni mzuri mnooo...... am thankful


Zawadi ya mwangu Cristabell nimejieleza kwenye clip ila sema kwenye picha nimechanganya kikombe ni cha Careen

Big sister na ujumbe wake humo.

Ahsante YESU

HAPPY MOTHER'S DAY


Proud Mama wawili

kununa sijaacha jomoniii ha!ha!ha


kamuonekano ka churchSaturday, May 12, 2018

TUMERUDI

Nimewamiss mnoo nawapenda mnoo........ nimejitetea sana pale chini kwenye videoHa!ha!ha! mnisamehe natusamehane.

 Haya hii nayo ni baby shower, Mama shughuli kama mnavyonijua Ha!ha!ha!  Its a boy....... kwa vile tulifanyia nje kwenye garden basi tukaona theme  green na blue lakini ili isiwe too much then tukaona soft greens na soft blues ziwe dress code............Basi sasa Mama shughuli ndo nikatoka kihivi ukizingatia mimi ndo mama shughuli kila kona nipo basi tena nikawa mwepesi ila viatu ndo nilitoa ha!ha!ha!
Jamani kwani wale wakipilipili wezangu mliishia wapi maana siwaoni tena Ha!ha!ha! mwenzenu kamchicha kamekubali


Yes wapenzi am back.....

 Deco
nimewafutafuta msiwaone wenyewe my idea muone hizo soft colours
Nawapenda!

Thursday, April 21, 2016

NYUMA YA PAZIA.................

Eeh bwana situkafanya boat cruise...... lengo kwenda tuu kuona wenzetu wanavyoishi.............  mi na Baba watoto wangu tumekutana yeye anapenda mnoo kucheza majini, yaani kunamichezo anachezaga mimi pembeni nahisi roho inatoka ha!ha!ha! lakini mi mkewe napenda view ya maji aisee ........ yaani ukinipeleka mafichoni  km ni eneo la maji maji naomba chumba kinachotazamana na  maji yaani kwa garama yoyote ntajitutumua (iwe ndani ya uwezo wangu lakini ha!ha!ha!) ila kuingia kwenye maji sasa ki!ki!kiii!

 Basi bwana tukafunga safari huko yaani nyumba zimejengwa  back yard mtu kapaki boat lake duuu!! we unafunga safari kwenda kuangalia dolfin mwenzio ndo nje kwake anapumzika ha!ha!ha!  tunajifungaga safari humu ndani kwenda fishing wenzetu wanafish nje ya nyumba ....... Duuu!!! ila kiukweli huku mafichoni ninakoendaga aisee kunanipaga mtazamo tofauti aisee..........

 na hii nimejikuta sina hela ila ndoto zangu zinakuwaga kubwa mpaka naogopa na pia imetusaidia sana kuona vitu kawaidaaa....... nakutokuwa na haraka zaidi kujipanga.... Yes inawezekana mbona nilivyokuwa umri fulani niliwahi kuaminishwa hapa nilipo  ningeweza kuona kwenye Tv pekee yake yaani ni ndoto kuwa !!! leo najiona ni zaidi ya ile ndoto basi na haya mengine yatawezekana Mungu atupe uzima nakuzidi kutuangazia neema yake.....


It is possible with Christ.........

nani hawaNdoto! andika ndoto yako.........
 Hapo Dolfin alipita ndo kumshangaaje sasa Ha!ha!ha!

 Yes  hii ndio ninayoizungumzia, Hizo nyumba za watu tuu kama mimi na wewe, tena nikuambiaje nilivyokuwa napewa historia niliambiwa wengi niwale walioretire ndo wamekuja na hela zako Bwana wewe why wait  mpaka huko kote????? Why why why...........


Tulivyokuwa wabishi mbona tuliwasiliana na wauzaji  ha!ha!ha! Mambo mengine yanatisha tuu kwa picha ila yanawezekana afanye akili yako iwaze tofauti............... na utakuwa tofauti

 Memory 


Tunawapenda

Wednesday, April 20, 2016

LA FAMILIA.............

Hamjambo humu kwetu??? kwetu  utukufu kwa Mungu kwa kweli, vyovyote ilivyo huwa tunaamini Mungu karuhusu   so we always go with the flow........ kama ni sad moment basi tunajitahidi sana kuomba amani ya Kristo ili turudi kwenye mstari na kama ni furaha time he!he!he! we always do our best to make memory...........

 Haya hizi picha za mafichoni kama kawa tukiwa mafichoni mapicha ya mtu nne hayakosekani ha!ha!ha! 

 haya twende kazi


Mama ake nani huyu???

Mapozi vepe


 na wawili wangu
 yaani hili pozi ni letu aisee mapicha huwa hayaishi km hatujafanya hivi ha!ha!ha!

 asikwambie mtu mtoto wa kike ni wa Baba yaani kikikikiii Jamani sijasema nataka maombi hapa kha!! hamchelewi kufunga na kuomba kwa ajili yangu ha!ha!ha! nikiwa tayari ntawambia msijitie kimbelembele  ha!ha!ha!

roho zangunani hawa etyi..........

kujibebisha vepe.........
Tunawapenda.............