Pages

Ads 468x60px

Friday, January 29, 2016

NYUMA YA PAZIA...........


Tulifika kihivi yaani???  kwa kweli ilikuwa surprise..... nature ya biashara yetu kweli inategemea upepo umekajee ... six days before ndo tukawa na uhakika wa safari hivyo hatukuweza kumshirikisha mtu mpaka nilivyokata ticket.....Ticket zenyewe ndo high season mkinga mie nilikuwa nahesabu mifuko ya cement tuu  ha!ha!ha!........ila nilikuwa sina jinsi ha!ha!ha! so 5day before kufika Tanzania ndo tukaanza kuwambia wazazi watoke mikoani kuja kutupokea na wengine kuwasafarisha tukakutane kijijini  zaidiiii ha!ha!ha!

ntakwambia kwa nini kijijini endelea kunichungulia...........nyie haya unafikiri kwa nini wenzetu wachaga tunasema wanaenda chimba dawa??? kuna baraka zake kuleeee. ila sema nene unafanyaje??? je inampa Mungu utukufu?? Ama ndo kuongeza maagano ???

 kutana na watu wangu basi.......

Mama Rose mnamfahamu na Mama Suleiman je??? jaza nafasi zilizo wazi ha!ha!ha!

(yahaya unaishi wapi??? mbona unafikia mahotelini?? yahaya weee yahaya ha!ha!ha!ha!)
ngoja nijitetee jamani kibandani hatukuona hekima kusumbua watu wanaishi jamani kha!!!kwa mda wenyewe wa siku kadhaa............

na shangazi yao mwenyewe mimi namuita Mama mwenye nyumba . jamani huyo ndo Dada ake Mama wawili yaani toka yeye mimi nafuata........... ila kanidunda huyo utotoni kha!!! 

 Mutu na sheji yake tunamwita  The Boss .......yee ndo bwana mipango yote ya mjini anatutoaje ushamba ha!ha!ha! Dogo tumekaa nae akiwa shule yaani ilikuwa kila kitu Dada Rose,Dada rose duu!! sa hizi nimerudi eti  namwita boss wangu ha!ha!ha! (haya huyu ndo nilimuachia ziwa kwa Mama yangu...... kuoa Bado lakini ....wapendwa maono vepe??? ha!ha!ha!)


Boss hivi ile kesi ya makontena vepe imeisha ama?? Ha!ha!ha!

Bwana wee hivi mnajua Mama Rose mapenzi kwangu hamna kabisa habari yote iko hapa yaani.......
akisikia sauti tuu mbona atachinja ng'ombe!! ha!ha!ha! ila kwa Rose akijitahidi sana Kuku tena mgonjwa ha!ha!ha! joke jamani ila kuna kaukweli kidogooo


Eneo langu lakujidai mimi lipo hapa....... asikwambie mtu Bwana, sikilizeni hakuna eneo muhimu kama hili,  Hili eneo linabaraka zake aisee,Tatizo lenu mnaingia fake mnataka kumaliza na  uhalisia. Maeneo km haya ingia kiuhalisia, misingi yako isiyobadilika iweke sawa, ijulikane km black black, white white Kikubwa unyesha upendo wa kweli huku ukisimamia kweli...............Mwanzo inasumbua naweza kusema tena sana.........(ni kawaida hata paka anajihami akiona sura ngeni)....... ila ukikaa sawa sawa mbona system itakaa sawa........ yaani utadeka  nakwambia..... mi mwenzenu hapa basi km ni mtoto  mi mziwanda ha!ha!ha! kaka yenu  atafuata badae.eee.....ha!ha!ha! Ila km uliingia Fake  halafu unataka kuleta uhalisia wako mbeleni best hilo unalo endelea  kuvumilia tuu ha!ha!ha! ndio maana ake si ulivumilia ili ndoa ikamilike basi tena, ndoa haishi mpaka kifo yaani tena ukicheza sana kuna baraka utajifungia....... otherwise omba Rehema ya ufunguzi kwao na utubu kwa nafasi yako.(wakubwa tuu ndo wanaelewa hapa na nyie watarajiwa kamata hii)

Kwa herini

Thursday, January 28, 2016

HODI HODIIIIIII............

Haya turudi jamani Mapumziko yameisha............... kiukweli nilikuwa na Muda mzuri sana Nyumbani..... aisee nyumbani ni nyumbani  kha!!! Amaaa mnajinoma chaa!! 

Ninachoweza kusema heshimu mahali ulipo kwa wakati huu.... unaweza kuwa na ndoto labda za kuwa sehemu nyingine............ wakati unachuchumalia hiyo taji ya kutimia ndoto zako, bado endelea kuheshimu nafasi na mahali ulipo. Kuna kusudi Mungu kukufanya uwe hapo ulipo......... hakuna kitu Bahati Bwana nani kakwambia??? (ila tuna neema ya Mungu ambayo pia inategemea nafasi yako umeichezaje?)haya mapicha picha yamitandaoni yanatuharibu sana akili, nakusahau kusudi mnajua??? mbaya zaidi asilimia kubwa ni fake fake tuu yaani tunawadanganyaaa...........(tufanyaje sasa na nyie mnapenda kudanganywa??? ha!ha!ha!)   Ninachotaka kusema ni hivi,Acha kulaani ardhi aliyokupa Mungu kwa wakati huu, wajibika sawa sawa kwa nafasi yako., Huku ukimkumbusha Mungu haja za moyo wako..........EE Bwana Mungu wetu ni mwaminifu asikwambie mtuu.....

Ni vizuri pia kumruhusu Mungu kuichunguza hiyo ndoto yako nakukupa amani maana, sio ndoto zote zinatoka kwa Mungu. Ni hivi wapendwa ndoto za kweli huwa hazi shut down yaani ...... zinaflow japo kuna kuwa  na ups and down lakini lazima kuna upenyo ambao unakuelekeza kuingia hatua baada ya hatua, yaani huwa inamuendelezo fulani ............Na wakati huo huo hauna uvivu wakufanya mambo mengine yaani kama ni uwajibikaji mahali ulipo unaendelea tuu......

 Ukiona una ndoto halafu imefikia hatua yaani haikufanyi kuendelea umebaki kulaumu tuu nakutamani tamani sijui fulani kawa hivi unaanza kuanza kujaribu nawewe kuwa yeye umesahau ndoto yako....... Mpendwa anza upya tuu hiyo ni dalili ya muovu kutaka kukumaliza.Ikiwezekana na utubu kwa kutoroka ndoto zako kutaka kuparamia ndoto za wenzio ha!ha!ha!

Namshukuru Mungu kwa ajili ya Tanzania yangu na watu wangu..... Eee Bwana watu wanakomaaa Bwana duu!! pamoja na kuwa mafisadi walitaka kujibebea nchi ...............Mungu anaangalia watu wake Bwana......... Mungu anamahesabu yake aiseee...  kweli nimeona mabadiliko makubwaaa........Yaani nahisi hasira za mabox zimeongezeka  ha!ha!ha! Unajua nini wengi hamyaoni labda kwa sababu tunaangalia mabaya tuu  mazuri hatuyaoni(tabia za kichoyo hizo ha!ha!ha!)  au labda mmezoea tuu yaani mnaona kawaida( mshindwa!!! hivi hamjipagi hata dakika kutafakari ukuu wa Mungu ndani ya maisha yenu???) au wengine ndo hivyo  tena kote wapo , ni lawama tuu kinachofanywa na wao ndo bora  kuliko cha wengine ha!ha!ha!( maisha ya kujikweza, umesahau Mungu anamuinua yeyote ampendae) 

Nimesema Hodi haya mnikaribisheee ha!ha!ha! 

  haya mapicha vepe.......
Mama mapicha nikiselfie

hebu angalia hapo utakubali mi muosha magari?? ha!ha!ha! labda unichunguze kucha zilivyo zakikazi ndo utashtuka ha!ha!ha!


Muke ya Slay


 hizi picha zilipigwa siku ya pili tulivyokuwa mjini tukienda kitaa wenyewe

Haya ntawarushia yaliyojili kama kuna yale niliyojifunza au km kuna kitu nataka kukizungumzia ama vepe???

 Nawapenda

Monday, January 11, 2016

NIPOGO

Hata mimi nimewamiss sana wadau laptop yangu sijui imekorofishaje sijui siwezi upload hata simu siwezi sijui ushamba 😀😀 otherwise tuvumiliane Mjage Instagram ndo kidogo naweza rusha mawili matatu.

Nawapenda

Saturday, December 26, 2015

HELLO TANZANIA........

 Wapenzi huu ukimya  wa humu ndani wiki yangu ilikuwa busy sanaaa........... nilikuwa natakiwa nimeet mipango ya mabox kwanza  kabla sijaondoka so nguvu ilitakiwa iongezeke sana hii wiki akili yangu ilikuwa kihivi. Thank God tulimaliza ki hivi .........

last day @my workshop for 2015

kilichofuata ni safari Christmass yetu tuliifaidi Dubai. nilishindwa hata kuingia kuwa wish  ni matumaini yangu wote mlisherekea vizuri.
na mwisho kabisa naomba nipige hodi asubuhi nimeamkia nyumbani. Home sweet home jamani i love my coutry cha!!! nawaonea wivu aiseee. niko busy kubond ila ma bby seater wanabadilishana tuu na mimi na dad yake tuko busy kujihoney moon ha!ha!ha! nikubadilisha tuu viwanja ha!ha!ha!


 tunapokea mialiko ila bajeti yako kuanzia usafiri mpaka kulala ha!ha!ha!
 nawapenda

Thursday, December 17, 2015

BABA NA MAMA ...........

Tuiite TBT basi maana ilipigwa jumapili iliyopita ha!ha!ha! Tatizo muda wa kuingia humu aisee mpaka huwa natamani blog ndo iwe instagram or whatsapp maana huko huitaji ni moja kwa moja tukio tunaachia ha!ha!ha! haya basi mnifollow IG ili msiwe wamwisho kupata matukio mnaonja kule mkija huku  mnamaliza hamu am vepe............ @beyoublog ndo tunalotumia huko

Siku hizi bonding nyingi tunazifanyia kwenye maji aisee huku kwetu ni joto balaa ....... haya mtuone 

 naingia ingia siku hizi soon na mimi ntakuwa chura we ngoja ha!ha!ha!

Dah!! hebu tuangalie wenyewe ila kuna siku tukibadilikiana humu ndani utafikiri sio sisi ha!ha!ha!
mtajiju..................


 bukta vepeee ha!ha!ha! nyie mwenzenu bikini zimenishinda kabisa i must admit naona aibu aisee hasa kwa watoto .... yaani ikitokea wameingia chumbani kwangu wamenikuta na pichu watoto watatoka mbio km wameona sijui nini na am sorry mamii sasa huwa nawaza nikiwatokea nakabikini vepeee??? ha!ha!ha! ngoja kwanza niendelea kuwa mkulima kha!!

tunawapenda

Tuesday, December 15, 2015

MKONOOOO...

 Haha humu ndani dizaini km mnasahaulika  vile lakini nawapenda mnoo.... Sasa leo ,hii special kwa kijana wangu mkiingia huko chini kacomment sana sijui katokea wapi ???yaani halafu nimemiss ha!ha!ha1...... Kiufupi alikuja kupiga shule huku akakutana na Mama wawili  si nikamuweka mzigoni...... ha!ha!ha!ha1 tulipigaje mkono yaani .........maongezi yetu yalikuwa mkono baba mkono ushemeji baada ya kazi kikikikiii.... We jamaa nimekumiss umenifanya nikuletee hii post niliipost jana facebook hahahaa !!kaofisi ketu vepeee....... fanya kurudi huku niko na kijana wangu Kalist  bwana....... Stella  wa mgodini ahsante Mama kwakunitembelea huyo jamaa muongo fulani hivi amazing usimsikilize anayokwambia ha!ha!ha! joke joke.




 haya ntarudi wadau wangu maisha na bills duuu
  

Thursday, December 10, 2015

TUNAKUZA JAMANI......

Hii kwa kweli hata haikuwa yakupost...... ila nimeona nije nikutie moyo mpendwa ulie comment post iliyopita mamii.......

My dear  hii mbegu yenyewe iko hivi.......wee angalia  hao classmates wake nimepiga picha juzi walivyokuwa nakajisherehe kakumaliza darasa .......tofauti yao  hapo labda miezi tena kuna mwingine hapo same mwezi , mwingine kamzidi......... na hawa wengine ndo naona dizaini mbegu km mwanangu huyu mdogo ha!ha!ha!  so usione shida ni kawaida mnooo......We ni Mama bora bwana wee ........dont stress please .....

na huyo ndo aliyekuwa mwalimu wake wa Darasa .......na hilo ndo darasa atakalosomea Cristabell wangu mwakani ha!ha!ha! inaitwa bandika bandua aisee!!! chezea mapacha wewe???........ na uzee huooooo.......kikikiiii tufanyaje sasa???, nikukomaa tuu........ but am loving the journey aisee siku zinavyozidi kwenda ule umama na utoto naona km unapungua its more of BBF yaani naulizwa maswali yakikubwa tuu, najobolewaje sasa  na broken english yangu,????? nakosolewa na kusifiwaje???, yaani raha  tuu aisee..........Mungu aendelee kutupigania kwa kweli.

Habari nyingine hii  ha!ha!ha!


Bwana wee........ si nimekutana na  hii tena ,katika pita pita zangu duuuu!!! enzi zile yaani full kufuatana fuata yaani.... kusindikizana sasa duuu!! tulikuwa tunapenda kutembea khaaa!! hii kitu tulikatiza myfair pale ha!ha!ha!  nyie vijana wasiku hizi sidhani km photo point ya myfair mnaielewaaa ha!ha!ha!
kama sio miaka 9 basi 10 iliyopita  tulijiphoto point ha!ha!ha!

nimemwambia Baba wawili tukitia tuu timu bongo naomba kinyozi wake nimuone anirudishie hii look ya kijana wangu khaa!! na mimi mwenge  kwa wasusi itahusika aisee ha!ha!ha! ila sema nene Mama wawili sijui mkorogo au edit ilikubaleee ha!ha!ha! nikujisoap soap ilikuwa ha!ha!ha!

Nawapenda

Monday, December 7, 2015

MAMA NA TOTO KUBWA..............


Ukiwa na misele na wawili shurti bag kubwa na shughuli hizi za christmass basiiii bag full kujaa makololo
ananifundisha mapozi huyu mpaka concetration ya Camera huwa haipo ha!ha!ha!

ila nyie mwanenu kurefuka vepe....... 
hapo saba akifika kumi basi tena mdogo wangu ha!ha!ha! sema sura ndo zitaeleweka iliyokomaa itajulikana ya kikongwe labda nianze kutumia product za look young foreverha!ha!ha! zikigoma sasa kikikikiii

hili pozi letu ni lazima yaani....



ushamba vepe...

 tunawapenda

Monday, November 30, 2015

NIPOGO.......

 Kama nawaona vile kuingia nakutoka kumchungulia Mama wawili ha!ha!ha! nawapenda sana mjue yaani basi tuu ila sema nini ubusy haishi jamani kha!! kila siku bora ya jana ha!ha!ha!

 Haya tena  moja ya siku ilikuwa hivi yaani............


 Joto wenzenu kha!!




Ha!ha!ha! hii nilipiga nije niwachekeshe .........mnakumbuka mwaka jana nililamika mti wa jirani full kunichafulia  hako kaeneo??  maskini sidhani km na yeye analijua hilo maana hata hatujuani............ kikikiii!  last 2weeks kuna best wangu mmoja kanitembelea si ndio akanambia kumbe yale mapindigesi aisee  mi nilidhani sijui maua gani ha!ha!ha!  he kuyatest aisee matamuje??? basi tena siku hizi nikijirudia mzigoni naenda kutembelea lililoiva iva kidogo mali yangu ki!ki!ki!

simu nayo huwa inahusika sana siku hizi how i wish blog iwe km facebook,instagram yaani naunganisha tuu kupost ha!ha!ha! hii biashara yakuandaa muda kuja kupost mgumu nyie basi tuu ha!ha!ha!
penda sana nyie

Monday, November 23, 2015

TUENDELEEE........


 Poleni kwa kusubiri........ Tatizo Mama wawili  mambo mengi  kha!! mpaka natamani nipotezee ila sema kila nikikumbuka ilivyokuwa najisikia tuu kushare.......... 

haya tuendelee


  Lengo langu la watu wasiozidi kumi  lilikuwa ni hili gari. Nilipenda  nicruise around na waalikwa wote humu ndani, huku tukipiga story na kugonga glass kwa muda wa masaa mawili kabla hatujaenda dinner..............  Nilipenda kuwasuprise tuu hivyo niliwaambia  tunapoenda dinner ni suprise, hivyo tukutane nyumbani kwangu then wote tuelekee huko....... lakini namba ilivyobadilika to 17 tayari nikajua hili lisingewezekana, nikaruhusu akili yangu ikubari mabadiliko, ambayo niliamini lazima yawe yakuboresha  bila kupoteza ile kiu niliyonayo ndani yangu yakufanya nililoona najitendea haki..........



Nikajikuta nawaza  badala ya wao kuja kukusanyika hapa why nisimpitie kila mmoja nyumbani ??? all i wanted for that day..... dizaini kama Queen treat, ( ukitaka kujua hilo red carpet ilikuwaje duu!!! niachieni tuu mwenyewe yaani ha!ha!ha) Nasikupenda iwe kwangu tuu, bali kwa wale waalikwa wangu pia. Niliamini  itakuwa tofauti kidogo lakini pia sikutaka wajue ntawachukuaje??

 Nikatoka na wazo hili lakuwambia, Kwa sababu venue yetu ni surprise, nakusubiriana  mahala pamoja inaweza kutuchelewesha baadhi yetu wamejitolea kutupitia. Hivyo  tunaomba usiulize ulize nani dereva, we jiandae muda fulani nje dakika 5 kabla dereva atakupigia simu  (Hahahahaaa huu uongo hata mimi mwenyewe sikuuelewa aisee...... kikikiii  nakutubu badae nilitubu.....)

 Sasa basi ilinibidi niongeze  muda wakukodi hilo gari, maana trip ilibidi ziwe mbili tena na sio moja ukiongeza na kwenda door to door lazima muda ungeongezwa. Nilipita nilianza kumchukua wa kwanza  kwa hiyo yeye akampigia wapi nakuja kukuchukua, watatu nae...........,.....,......., it was fun humo ndani kwa kweli.........

Thank God hili lilifanikiwa....... Kiukweli mapokeo yake yalikuwa yakipekee mnoo......... Iko hivi wapenzi wangu, hapa  unapofanya sio unatafuta misifa ya Mama wawili, au umaarufu ha!ha!ha! bali inakuwa ile kiu iliyondani ambayo hujui matokeo yake, na uko tayari kukabiliana nayo kwa vyovyote vile yatakavyokuja.... 

Yanavyokuja kwa namna yakupondeka  na maelezo fulani  ambayo wewe binafsi unaona yamekuwa zaidi, wakati wewe lengo lako niku have fun  na waalikwa wako........ aisee ile feeling yake haielezeki zaidi yakumrudishia Mungu utukufu........

 Ikumbukwe haikuwa kumsaidia Mjane,yatima au muhitaji yoyote, ambaye mapokeo yake nikama umesave life..... hawa walikuwa ni watu ambao yawezekana wanauwezo zaidi yako ila labda kutokana na ubusy wa maisha   kuwaza vitu km hivi si rahisi...... Si hivyo tuu 

 Nina rafiki yangu mmoja ( Mteja wangu ila sasa nahisi nimekuwa km best wake eti ha!ha!ha! )
 Huyu Best ukizungumzia $$$ aisee ana mafarasi huko,  Biashara niliyojuana naye yakumuoshea magari  ana Car yard (anauza magari new na used), ana mainvestment balaa yaani............ kajipanga  haswaa, uzee wake anaumaliza pazuri mnoo ila kuoa mke sasa mweee!!! na nyimbo zangu zakumleta kanisani uwiii!!! hapo ndo najionaga sijakaza vyakutosha  ha!ha!ha! haiwezekani ananimwagia misifa weee halafu nikitaka  kumleta  kwenye lengo husika anagoma yaani atabadilisha na topic ha!ha!ha! sasa sijui injili yangu inakuwaga haina upako, au muda bado, au.......... aisee mi ndo maana nawaheshimu sana watumishi aiseee ..............hichi kipawa usiombe uwe nacho aiseee ha!ha!ha! Wapendwa tuu ndo wamenielewa hapa  )

Tuendelee...........

 Sasa siku moja alileta gari yake yakutembelea ifanyiwe kazi, nikajikuta, nimeifanyia mwenyewe kwa mikono yangu na ilivyofika muda wakumkabidhi, nilimkabidhi bila kuandikia invoice  ili anipe check. Aliponiuliza nilimwambia hii ningependa isifanyiwe mahesabu, kama kunilipa bei yake aliyokuwa anategemea $380 nilivyomjibu vile alionyesha hali yakustuka, nakutoamini vile, akaniuliza mara ya pili km  kweli........ kitu ambacho nilijifunza na ambacho labda alikizungumza kwa namna nyingine  ni hichi,

 Watu hawaelewi ni jinsi gani huleta maana kubwa, kwa mtu km yeye kununuliwa  hata chocolate  nakuletewa kwa kunia  kumbariki........... aliongeza,  kwa nafasi aliyonayo amejikuta yeye ndo wakupewa ahsante maana anategemewa kutoa zaidi kuliko kupokea...............Hivyo basi  nyakati km hizi ambazo anajikuta yeye anatakiwa kusema ahsante zinapomkuta huwa anajikuta na yeye ni binadamu. aliongea mengi ambayo nilijifunza sana.......

 Ikumbukwe labda mimi nilivyofanya ilikuwa tuu labda ni mbinu yakumbariki tuu mteja wangu, kwa mahusiano  mazuri yakibiashara tuliyonayo,  Narudia tena kiasi alichotakiwa kutoa kwake ni km hela ya sukari au  labda ya karanga ,hivyo  sikuwaza  yale mapokeo yatakuwa vile alivyo, ( Ila sasa sema amenifanya,  kila ninachomfanyia nijistukie je nafanya ili nipate misifa  tena au?? hata chocolate aliyoizungumzia haipati tena ha!ha!ha!  Misifa isiyo na maana nikupoteza muda mjue)

 Nimeleta huu mfano ili kukazia mazungumzo yetu  lengo  nikujifunza unapofanya kitu unafanyaje, lengo ni nini?? na jinsi gani unaweza ukazalisha kitu chenye uhai kutoka pande zote mbili........


 Mnataka kujua sasa ilikuwaje tena? maana trip zilikuwa mbili, nilijigawaje??

Tutaendelea

Wednesday, November 18, 2015

NYUMA YA PAZIA NO1.............

Haya bila shaka mnashauku yakujua kulikoni....... Ngoja leo tuanze na magauni hayo ilikuwaje??

Kiukweli sikuwa na wazo kabisa la kufanya chochote kwa habari ya birthday yangu........ hadi hapa wiki 3 kabla ya siku, ambayo nilienda kwenye shughuli moja nikamuona mdada kavaa gauni la dizaini hizi. sio kwamba ilikuwa mara yangu ya kwanza kukutana nalo, nimeliona sana ila nilikuwa naamini sio kwa mwili huu wangu ha!ha!ha!  lakini nilikuwa nayapenda mnoo, nakumbuka mpaka nilikuwa najisemea moyoni hili gauni likimpata mtu fulani atapendeza mnooo........ Basi nilivyomuona yule Dada nikajikuta tuu nawaza, Vipi km nimekaa mezani nimezungukwa na wadada wenye miili yao wamevaa hivyo ha!ha!ha!ha! yote mawazo lakini...

Ndipo wazo la kufanya kitu kupitia birthday yangu likaja, Nikawaza vipi nipate wanawake 7-10 wamevalia haya magauni?? huku nikijua mimi muhusika  ntakuwa kituko yaani  ha!ha!ha! ila kwa sababu natamani kuona nimezungukwa na watu wamependeza na maumbo yao. Nikawaza tena hiyo namba nikipata niwafanyie suprise fulani fulani ambazo ziko ndani ya uwezo wangu. Kiukweli uwezo wakuwanunulia nilikuwa sina na hata km nilikuwa nao sidhani km ningenunua  kwa sababu hizi........

Niliamini mualikwa hana shida na visenti vyangu ila utu  wakufaana ndio unaohitajika.........Niliamini nisingekosa watu 5-7 wakukubali ombi langu  kwa ajili ya siku yangu yakuzaliwa.

Pia  niliamini kwa hili ninalotaka kulifanya linahitaji utayari wa bila kushurutishwa............nilihitaji ile Yes movement, yakunionyesha kuwa Rose tupo tayari. japo kuwa hatu hang out mara nyingi pamoja, au hatuonani mara kwa mara lakini tupo pamoja  nawewe............

 Basi moja kwa moja nikajikuta nachat na yule Dada anihakikishie km anaweza kuongea na muuzaji tukapata hayo magauni ndani ya mda mfupi......... akarudi na jibu inawezekana nikamwambia naomba nikupe kazi hapo hapo  naomba unisaidie nipate wadada  5-10 ambao wako tayari kujinunulia hayo magauni kwa muda huu kwa ajili ya birthday yangu.

 Nilikuwa na watu ambao ningeweza kuwaface mwenyewe, nawangekubali ila kiukweli nilitaka wale watu ambao sijashibana nao sanaaa, ambao kukubali kwao kutakuwa kama kurudisha fadhira vile,au kunionea aibu kwasababu nimewaomba na pia nilitaka kile ninachotaka kukifanya nisifanye kwa sababu  ya urafiki wakushibana au undugu.( kama unanifatilia humu huwa nasisitiza ,,mara nyingine jisikie tuu kumbariki mtu tofauti yaani sio ndugu, wala yatima,  na mara nyingine sio lazima awe muhitaji ila pia uwe na hekima wengine hawachelewi kukumwagia chai yako unayombariki usoni, kwakuona unataka kumletea dharau ha!ha!ha! rejea kwa nini nisingeweza kuwanunulia magauni)

 Mimi nilichofanya kuna watu km wawili watatu nilihisi labda na wao wangealikwa kwa sababu zangu binafsi labda wangependa, lakini nilihisi mualikaji anaweza asiwafikirie au hana mawasiliano nao au vyovyote vile kwa hiyo nikatuma tuu ujumbe kwao, kuna birthday party yangu inakuja km ungependa kuniunga mkono naomba uwasiliane na mtu fulani (mwalikaji) atakupa utaratibu. Nilimshangaa Mungu ndani ya siku chache sana alinitumia ujumbe amepata watu mara tatu zaidi ya ninayoitaka, ila wengine wameomba wanamagauni yanayofanana na hayo wanataka wasinunue  ha!ha!ha!

 ( ngoja niwambie iko hivi, unapoishi maisha ambayo mtu akikuuliza who is your best friend au friend  huna jibu na bado ukiwa na kitu km hivi ukajikuta unasupport kubwa mnoo, usiichukulie poa aisee Mshukuru Mungu sana (ntarudi hapa tukimaliza hili la birthday  yangu kuwasimlia kitu kilichonifanya  bado hata ninavyoandika hili kina nitoa machozi)  Ila niamini ni Neema kubwa.

Kumbuka hawa watu hawakuwa wanategemea chochote toka kwangu zaidi ya kuambiwa ni birthday ya Rose ......Utaratibu wa  huku kwetu ukialikwa yaani maana yake usafiri, kula na kunywa juu yako we jiandae tuu uwambiwe garama yake itakuwa sh. ngapi kwa usiku huo, itategemea mnaenda wapi..............hicho ndicho ninachoamini walikuwa wanategemea kitafuata baada ya magauni..


Nikiwa nimeletewa hiyo namba bado sikutaka kujua ni nani na nani. ila nilichoweza kumwambia naomba uwambie ticket yakuingia ni kutoa order ya gauni. ili mipango itimie na pia naomba  maxmum namba iwe 16 mtanielewa kwa nini ilikuwa hivi..........( hahahaa nimeanza jeuri sasa mwee!!!)  

Ngoja niwambie,  Kwenye hizi sherehe iwe harusi au vinginevyo nimeona kuna watu wameamua  shughuli ifanyike vyovyote itakavyo kuwa  ili kuwafurahisha watu au labda kutoa lawama lakini hajafanya km vile angependa iwe .......mwisho wa siku  hauna furaha tena.(NIKOSA KUBWA MNOOO) nakubaliana, kuna wakati labda kuna marekebisho, au ushauri wa kuboresha zaidi lakini ikifikia hatua umekasirika umeamua vyovyote itakavyo kuwa  iwe.........BIG NO!!!

 BASI MAMA WAWILI NILIKUWA NA MIPANGO  ambayo labda ilitakiwa kuboreshwa bila kupoteza ile hadhi yake niliyotaka iwe ambayo mtanielewa badaye............  

Tumalizie mambo ya magauni  ha!ha!ha! Bwana siyakafika siku hiyo ya shughuli asubuhi  we!! watu sikupaniki hasa mimi nilihisi walihitaji wayapate mapema ili wajue watatokaje ...... lakini nilikuwa nina ile nguvu yakuamini km walichagua style inayofanana na maumbo yao bado watapendeza by that time tayari nilishajua nani anakuja. kwa upande wangu kama nilivyojua mwanzo yaani mimi hata iwaje sio type yangu..... ila it was about waalikwa hata nilikuwa sijali nilisema ntalivaa hivyo hivyo hata kama kituko ha!ha!ha! Kulifungua  bwana kha!! niliagiza mawili aisee ma Kubwaaa,mareeeefuuuu., hadi kutembea nashindwa yaani   yaani ningesema nikomae hivyo hivyo lazima ningeitwa chizi ninaejielewa ha!ha!ha! ilihitaji fundi haswaaa kumbuka yamebaki masaa tuuu.

 Ningeweza kutafuta moja ya Gauni lakipekee km birthday girl.....  lakini nilijisemea  moja ya lengo nikutokuwa tofauti na waalikwa  i mean yaani nilitaka iwe km ladies night out ........na hayo magold  ila kwa sababu kutembea nilikuwa na shindwa nikaona isiwe tabu nikatafuta mkasi nikakata hayo magold ya mkono na kifuani  kwenye nguo moja, nikaingia kwenye nguo zangu tafuta gauni inayoendana na hayo material ya magauni yao....... nilitaka kubandika mwenyewe na mkono ila kuna vitu nilitakiwa kufatilia  nikamtafuta Dada mmoja nikamwambia sikia chukua sindano ya mkono ninachotaka haya mavitu yakae hapo kifuani na mkononi nikamuachia na hela ya soda yakumtia moyo  ha!ha1ha! mwisho wa siku hilo ndo gauni....... mkiliangalia sana limefungwa fungwa mnoo maana hayo madude yalikuwa mazito kwa hiyo hata shape ya gauni ikapotea....... ha1ha!ha!


Ikumbukwe lengo ilikuwa nifanye kitu kwa ajili ya namba fulani ambayo ilikuwa iko ndani ya uwezo wangu. Haikuwa kufanya ili nionekane nimefanya, ni ile kutimiza hamu niliyonayo ndani ya moyo wangu .................

ITAENDELEA







Monday, November 16, 2015

ONJENI ...........



Haya basi Mama wawili kesho anaongeza mwaka mwingine......... heheheee uzee huo unakuja mwenzenu.....

 Basi leo onjeni mapicha kesho ntawaeleza ilikuwaje?? na kwa nini ilikuwa hivi?? nimejifunza nini??? labda na wewe utajifunza kitu kupitia hili.

Nilianza hivi........

VIP treat kama kawa..........
nikuwanyoosha tuu mwaka huu mtakoma ha!ha!ha!
nikapita nyumba moja baada ya nyingine kumchuka mualikwa..... kumbuka hii ilikuwa suprise mwalikwa aliombwa awe nje mda fulani kuna mtu anakuja kumchukua  bila kujua usafiri gani utatumika na wala hawakujua wapi wanaenda...............
 Eti Dada yake nani huyu??? mi namwitaga makubwa! nampendaga tuu yaani.............

Namshukuru Mungu suprise ilikuwa suprise kweli........... nyie angalieni nyuso zao  ....



Bwana weee sio kwa minyoosho hii ......hamchelewi kuniita disigner ha!ha!ha! au party plan kkkkkkkk

 The joy inside me jamani kuwaona warembo wamependeza hivi...... aisee Mungu mwenyewe anajua!!


nilivyomaliza kuwapitia nilikuwa nakuja kuwaleta kwenye venue kama kawa red carpet heshima yao ......... 






wapenzi siwezi weka kila mtu/kitu hapa......wale wafacebook bila shaka mmejionea wenyeweee.......
kwa sababu nilikuwa na trip mbili hapa palikuwa pakufikia nakusubiriana huku wahudumu wanaendelea kuwahudumia hahaha! kweli tulikuwa maqueen yaani.......

Basi tena wote tulipofika ndo nikawaongoza humo ndani.... na mengine yalifuata

na huu ndo muonekano wake......

kesho tena nimewambia mjiandae kusoma gazeti simnajua huwa siwezi kujieleza kifupi hahahaaa!