Pages

Ads 468x60px

Thursday, January 28, 2016

HODI HODIIIIIII............

Haya turudi jamani Mapumziko yameisha............... kiukweli nilikuwa na Muda mzuri sana Nyumbani..... aisee nyumbani ni nyumbani  kha!!! Amaaa mnajinoma chaa!! 

Ninachoweza kusema heshimu mahali ulipo kwa wakati huu.... unaweza kuwa na ndoto labda za kuwa sehemu nyingine............ wakati unachuchumalia hiyo taji ya kutimia ndoto zako, bado endelea kuheshimu nafasi na mahali ulipo. Kuna kusudi Mungu kukufanya uwe hapo ulipo......... hakuna kitu Bahati Bwana nani kakwambia??? (ila tuna neema ya Mungu ambayo pia inategemea nafasi yako umeichezaje?)haya mapicha picha yamitandaoni yanatuharibu sana akili, nakusahau kusudi mnajua??? mbaya zaidi asilimia kubwa ni fake fake tuu yaani tunawadanganyaaa...........(tufanyaje sasa na nyie mnapenda kudanganywa??? ha!ha!ha!)   Ninachotaka kusema ni hivi,Acha kulaani ardhi aliyokupa Mungu kwa wakati huu, wajibika sawa sawa kwa nafasi yako., Huku ukimkumbusha Mungu haja za moyo wako..........EE Bwana Mungu wetu ni mwaminifu asikwambie mtuu.....

Ni vizuri pia kumruhusu Mungu kuichunguza hiyo ndoto yako nakukupa amani maana, sio ndoto zote zinatoka kwa Mungu. Ni hivi wapendwa ndoto za kweli huwa hazi shut down yaani ...... zinaflow japo kuna kuwa  na ups and down lakini lazima kuna upenyo ambao unakuelekeza kuingia hatua baada ya hatua, yaani huwa inamuendelezo fulani ............Na wakati huo huo hauna uvivu wakufanya mambo mengine yaani kama ni uwajibikaji mahali ulipo unaendelea tuu......

 Ukiona una ndoto halafu imefikia hatua yaani haikufanyi kuendelea umebaki kulaumu tuu nakutamani tamani sijui fulani kawa hivi unaanza kuanza kujaribu nawewe kuwa yeye umesahau ndoto yako....... Mpendwa anza upya tuu hiyo ni dalili ya muovu kutaka kukumaliza.Ikiwezekana na utubu kwa kutoroka ndoto zako kutaka kuparamia ndoto za wenzio ha!ha!ha!

Namshukuru Mungu kwa ajili ya Tanzania yangu na watu wangu..... Eee Bwana watu wanakomaaa Bwana duu!! pamoja na kuwa mafisadi walitaka kujibebea nchi ...............Mungu anaangalia watu wake Bwana......... Mungu anamahesabu yake aiseee...  kweli nimeona mabadiliko makubwaaa........Yaani nahisi hasira za mabox zimeongezeka  ha!ha!ha! Unajua nini wengi hamyaoni labda kwa sababu tunaangalia mabaya tuu  mazuri hatuyaoni(tabia za kichoyo hizo ha!ha!ha!)  au labda mmezoea tuu yaani mnaona kawaida( mshindwa!!! hivi hamjipagi hata dakika kutafakari ukuu wa Mungu ndani ya maisha yenu???) au wengine ndo hivyo  tena kote wapo , ni lawama tuu kinachofanywa na wao ndo bora  kuliko cha wengine ha!ha!ha!( maisha ya kujikweza, umesahau Mungu anamuinua yeyote ampendae) 

Nimesema Hodi haya mnikaribisheee ha!ha!ha! 

  haya mapicha vepe.......
Mama mapicha nikiselfie

hebu angalia hapo utakubali mi muosha magari?? ha!ha!ha! labda unichunguze kucha zilivyo zakikazi ndo utashtuka ha!ha!ha!


Muke ya Slay


 hizi picha zilipigwa siku ya pili tulivyokuwa mjini tukienda kitaa wenyewe

Haya ntawarushia yaliyojili kama kuna yale niliyojifunza au km kuna kitu nataka kukizungumzia ama vepe???

 Nawapenda

1 comments:

  1. Ila ulitutupa sanaaa eeeh. Yaani una madeni balaa. Tukianza na Dubai, Dar, Sijui Iringa, Arusha, Zanzibar, Dar tena. hee mwee utaanza na ipi utaacha ipi. Ila tuweekee tu. This Blog give me life. So una deni na mimi yaani. Kila la heri uko mliko.

    ReplyDelete